Baba yetu amefariki lakini hakuacha wosia wowote

Kwa haya maelezo yako ni wazi kabisa huna nia njema na hao watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa haya maelezo yako ni wazi kabisa huna nia njema na hao watoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nina nia njema maana kama wataamua kuuza kule walikoishi na wazazi wao ina maana kabisa wameweka utengano na kama wataweka utengano sisi hatutahangaika nao .

Pia sitakuwa tayari kushirikiana nao .
 
Lazima ujue warithi hawana wosia. Pili wote nyinyi ni warithi na laana itawajia nyinyi wakubwa mtakapo wanyanyasa wadogo zenu, Msisahau hilo..

Hekima iwe juu yenu..
 
Lakini ndugu yangu naona inakuwa ngumu umefafanua vzr na nimekuelewa .

Shida ni moja kwanza mpaka sasa watoto wa kwa mke mdogo wamekaa kwa upande wa mama yao alikozaliwa.

Kaka yangu mkubwa ameomba watoto wasisambaratishwe wakae sehemu moja lakini imeshindikana .

Maana baba zetu wakubwa wanadai kwamba mtoto anawajibu wakuchagua wapi aende kulelewa ila mimi kuna kauli nainukuu ¶YATIMA HACHAGUI MLEZI¶

Sasa mbona watoto wanaanza kuchagua wakae kwa upande wa mama yao wakati upande wa baba yao wanajiweza na wapo tayari kuwalea watoto ?

Mimi kuna kitu nimehisi kuwa wale watoto wamepandikizwa sumu yakuuchukia upande wa baba yao.

Je wale watoto wote tukiwahitaji wakae kwa kuwalazimisha kwetu kwa sababu ni wadogo zetu hivi inakataa kweli ?

Naombeni ushauri.
 
Shida ni moja ndugu yangu sisi tulipenda tukae na wadogo zetu lkn chakushangaza ilishindikana wamechagua wenyewe etii wakae kwa mama zao wadogo , je tutawalazimisha tuwe wamoja ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…