Mkuu, huyo binti bado ni mdogo sana kiumri na anakosa tu uzoefu wa maisha sio kwamba ana akili ndogo, huo ni upepo wa ujana unaomsumbu kwa sasa, pointi kubwa hapa ni kwamba akikosea ukamuelekeza anakuelewa na habadiliki, hii unatakiwa kulizingatia sana.
Wanawake wengi wa sasa ni ngumu kumkosoa akakusikiliza na akabadilika, wengi vichwa ngumu lakini huyo wako anarekebishika, haombi hela, na anapenda ndugu zako, Kaka, huyo ni wife material kwa asilimia kubwa, tabia huwa haibadiliki kwa mtu asiyetaka kuelewa, lakini kwa mtu anayeonyesha improvement kila siku kama huyo kwenye kupika, huyo anabadilika kwa uzuri. Mlee vizuri kulingana na mfumo unaoutaka wewe, itakusaidia sana.