Babati town na Dodoma ipi sehemu nzuri ya kufanya biashara ndogo ndogo na penye unafuu wa maisha?

Habari zenu wadau.
Nashukuruni kwa maoni yenu nilifanyia kazi pande zote mbili na nilifika kabisa kila eneo.
Naomba nitoe mrejesho kwa upande wangu binafsi Babati ni sehemu nzuri sana.
Wana Babati naomba mnipokee soon tutakua pamoja.

Kwaraa,maisaka.[emoji736][emoji736][emoji736]
 
Bora hata umechagua huko. Dodoma ni mji mgumu sana kuishi. Ingawa natambua fika Dodoma gang watanipinga.
 
Kama unaangalia unafuu wa maisha dodoma hapakufai..aisee dodoma ni mji ghali haswa..nenda babati ufanye hizo biashara zako ndogo ndogo..ila kama unataka kukua njoo dodoma ila ujibane haswa..
Unamaanisha kukua kivipi?
 
Habari za majukumu wadau? Natumai mpo shwari.
Kama title inavyoonekana, jamani naombeni muongozo kati ya Babati town na Dodoma ipi sehemu nzuri ya kufanya biashara ndogo ndogo na penye unafuu wa maisha.?
Kuhusu biashara ni yoyote ile naangalia fursa kwenye eneo.

Karibuni kwa maoni, ushauri.
Nenda Dodoma.
 
Mzunguko wa hela ni mkubwa muda wote. Haukuna msimu wa kupumzika biashara. Pia mji unapokea wageni wengi sana. Dodoma hata kuchuuza biashara ya machnugwa kwa mkokoteni utapiga hela. karibu Dodoma.
Hali ya hewa na maji vipi, wanasema eti Kuna vumbi na upepo mkali wa kuumiza macho ni kweli??
 
Mzunguko wa hela ni mkubwa muda wote. Haukuna msimu wa kupumzika biashara. Pia mji unapokea wageni wengi sana. Dodoma hata kuchuuza biashara ya machnugwa kwa mkokoteni utapiga hela. karibu Dodoma.
Mimi ni mtumishi, nataka kuhamia Dodoma.

Kikubwa ni fursa tu na angalau unafuu wa maisha nisije kustafu Sina kitu.
 
Mtumishiiiiii!!!!1!!!!!1!!!111.
subiri mafao ya kustaafu ule uzeeke.

Biashara kama hujawahi kuifanya usihame kwa ajili ya kufanya biashara. kama una wazo hilo fanyia hapo ulipo maana unaweza kuhama usipate huo muda kufanya biashara. Biashara ni kazi kuliko kazi ulionayo Unatakiwa kuamka alfajiri na kulala usiku sana huku akili na macho yakiwa active muda wote kufatua fursa mpya na kulinda maharamia wasipite na mtaji wako.
 
Nahitaji unishauri kuhusu maisha ya Dodoma kama mkaazi.

Sijasema naenda Dodoma kufanya biashara. Vile vile, nadhani naijua biashara kyliko wewe unavyodahani. Tena biashara, siyo umachinga.
 
Kama umeshavuka level ya umachinga humu hutapata ushauri. kawafuate wafanya biashara wakubwa mtaani kwako wakupe mikakati na uzoefu wao.
 
Nahitaji unishauri kuhusu maisha ya Dodoma kama mkaazi.

Sijasema naenda Dodoma kufanya biashara. Vile vile, nadhani naijua biashara kyliko wewe unavyodahani. Tena biashara, siyo umachinga.
Maisha ya Dodoma ni ghali, nadhani inaingia top 3 ya vimiji ghali Tz after Arusha, Nazungumzia Dodoma mjini.

Nyumba decent ya familia labda kuanzia 300k, 400k na kuendelea. (Hapa nazungumzia standard fulani) Viappartment vya kibachela vipo kuanzia 150k-250k hiki unakuta ni kiko katika standard nzuri. Sina uhakika na kule uswahilini kwetu bei za nyumba/vyumba zikoje ila napo nadhani vyumba havipungui 50k. (Sina uhakika)

Gharama za usafiri wa uma ni zile zile mfano daladala nadhani ni 400/500 (sina uhakika) Ila nina uhakika na boda na bajaji maana huwa napanda inapobidi, ambapo bei sehemu nyingi ni 2000 kwa boda na 4000/5000 kwa bajaji kwenda maeneo mengi. Kwa kuongezea mitaa mingi haina route za daladala.

Gharama za chakula ziko juu kidogo, ukiwa na familia ndogo ukizama majengo sokoni au sabasaba na laki utatoka na mifuko isiyozidi miwili ya vimizigo ulivyonunua. Hapa kama umetoka mikoa kama mwanza/Iringa/Moro/ mbeya utapamis sana 😀

Mzunguko wa pesa ni mkubwa kwa sasa, Inamaana watu wenye uwezo wa kufanya manunuzi wameongezeka. Nazungumzia watu wa kawaida angalau wenye uwezo kiasi wa kufanya manunuzi, Sizungumzii matajari maana ni wakuhesabu 😀

Sehemu za starehe zinajaa mara nyingi, vijiwe vya chakula vinajaa hasa jioni nadhani huu mji unamabachelor wengi walioacha familia mikoa mingine labda wapo kikazi, Huwa naona vijiwe vya chakula vya barabarani Area C,D, Chako ni chako na makole etc vinajaa sana jioni/Usiku.

Hali ya hewa ni mbaya kama kawaida, vumbi kama kawaida, Maji Sehemu nyingi za mjini yapo walau ma4 kwa wiki kama una matenk ya maji unakua uko salama zaidi.

Bei za fremu mjini zinaanzia 250k (haka kanakua kadogo sana) ya angalau inaanzia 300k na kuendelea, mitaani bei za fremu zinaanzia 100k/150k
 
Maisha ya Dodoma ni ghali, nadhani inaingia top 3 ya vimiji ghali Tz after Arusha, Nazungumzia Dodoma mjini.
Dodoma kilo ya Nyama, dagaa na Unga ni bei gani?
Nyumba decent ya familia labda kuanzia 300k, 400k na kuendelea. (Hapa nazungumzia standard fulani) Viappartment vya kibachela vipo kuanzia 150k-250k hiki unakuta ni kiko katika standard nzuri.
Okaya
uhakika na kule uswahilini kwetu bei za nyumba/vyumba zikoje ila napo nadhani vyumba havipungui 50k. (Sina uhakika)
Uswahilini kwa Dodoma ni sehemu gani?
Gharama za usafiri wa uma ni zile zile mfano daladala nadhani ni 400/500 (sina uhakika) Ila nina uhakika na boda na bajaji maana huwa napanda inapobidi, ambapo bei sehemu nyingi ni 2000 kwa boda na 4000/5000 kwa bajaji kwenda maeneo mengi. Kwa kuongezea mitaa mingi haina route za daladala.
Bajaj ni bei gani kwenye route zisizo na daladala?
Gharama za chakula ziko juu kidogo, ukiwa na familia ndogo ukizama majengo sokoni au sabasaba na laki utatoka na mifuko isiyozidi miwili ya vimizigo ulivyonunua. Hapa kama umetoka mikoa kama mwanza/Iringa/Moro/ mbeya utapamis sana 😀

Mzunguko wa pesa ni mkubwa kwa sasa, Inamaana watu wenye uwezo wa kufanya manunuzi wameongezeka. Nazungumzia watu wa kawaida angalau wenye uwezo kiasi wa kufanya manunuzi, Sizungumzii matajari maana ni wakuhesabu 😀

Sehemu za starehe zinajaa mara nyingi, vijiwe vya chakula vinajaa hasa jioni nadhani huu mji unamabachelor wengi walioacha familia mikoa mingine labda wapo kikazi, Huwa naona vijiwe vya chakula vya barabarani Area C,D, Chako ni chako na makole etc vinajaa sana jioni/Usiku.
😨
Hali ya hewa ni mbaya kama kawaida,
Ubaya wa Hali ya hewa ukoje?
Baridi Sana, Joto Sana, vumbi Sana kuliko Kigoma na Kilimanjaro?

Dodoma Hali ya hewa ni mbaya kuliko Dar?
vumbi kama kawaida, Maji Sehemu nyingi za mjini yapo walau ma4 kwa wiki kama una matenk ya maji unakua uko salama zaidi.

Bei za fremu mjini zinaanzia 250k (haka kanakua kadogo sana) ya angalau inaanzia 300k na kuendelea, mitaani bei za fremu zinaanzia 100k/150k
Ahsante
 
Back
Top Bottom