Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Kwa wale wasioamini kwamba Babu seya alionewa, kwa kawaida kila binadamu kaumbiwa nafsi ya kukiri kosa (Guilty Conscious) ndio maana kwa mfano mtu akishikwa ugoni hawezi kujibu mashambulizi kutoka kwa huyo aliyemfumania hata kama angekuwa anamzidi nguvu, hii ni kutokana na kwamba nafsi inamwambia ni kweli umekosa. Lakini hata kibaka hwa anakubali kichapo pale anapobambwa akikwapua tofauti na pale anapokuwa amesingiziwa atapambana kweli kujitetea.
Babu Seya licha ya kutoa walaka kupitia gazeti pendwa muda nmfupi kabla ya hukumu yake akielezea hatima ya kesi hiyo, tunaona tangu kutiwa hatiani ameendeleza mapambano kupinga hiyo hukumu, hii ndio namna ya mfungwa kuuelezea umma yanayomsibu kwakuwa hana uwezo wa kuitisha press conference.
Huu ndio uwe msukumo wa kutufanya kuamini kwamba alionewa, alibambikiwa kesi kama ilivyo jadi ya vyombo vya dola kutumiwa hovyo na wakubwa na itabakia kuwa anatumikia personal vendetta kwa huyo aliyemzulia kesi hii.
Hapa cha kuangalia ni facts na evidence za plaintfull na defendant.
Huku kuonewa kutathibitishwa na mahakamani na kwa ushahidi na kama ushahidi ulio pelekwa mahakamani unatia shaka basi kuna nafasi ya kuhojiwa kwa facts.
Nina amini katika hili kila mtu atapata haki yake, mahakamani hakuna ujanja ujanja sana ukweli utakuwa wazi tuuu.