Mkuu nimepitia hizo documents.....Daah ushahidi umewekwa na victims live kabisa....Sijui kwa nini watu hawapendi kusoma?Watoto 10 waseme Uongo (bila kuchanganyana) mbele ya Mawakili, Mahakama n.k Rehearsal ya aina gani ilihitajika mpaka waweze kukariri??Watu wanafikiri kundi la watu 10 kubuni uongo na kuutetea mahakamani ni rahisi tu sembuse kwa Watoto??Watoto wamewatambua watuhumiwa bila Shaka pamoja na kuelezea mazingira ya nyumba/chumba walichokuwa wanafanyiwa ubakaji (ikiwemo kubainisha vitu vilivyopo chumbani kwa usahihi)Kwa ushahidi uliowekwa Sioni namna akina Babu Seya wangeshinda,hata wangekata rufaa Mara 1000........KWANZA NIMESHANGAA HUKUMU NYEPESI WALIYOPEWA......
Mkuu mimi kinacho nisikitisha sana ni kuona baadhi ya Watanzania wenzetu wanajaribu kutetea watu wanao abuse watoto wetu wadogo kwa ngono za kishenzi, mnawezaje kutetea MONSTERS kama hao - nchi za wenzetu wafungwa kama hao mara nyingi unyongwa na wafungwa wenzao gerezani wakipata tetesi kwamba walifungwa kutokana na ubakaji wa watoto wadogo; yaani hatujali kwamba victims walipata kilema cha kisaikolojia kwa maisha yao yote. Binafsi na vipa pongezi vyombo vyetu vya DOLA kwa kushughulikia suala hili kwa nguvu zao zote, sijui kwa nini baadhi yetu tunachukulia kimzaa mzaa suala ili ovu - au kwa kuwa victims hawakuwa watoto wetu tunaona sawa tu. Tujaribu kutafakali kiundani ubakaji (mpaka wanaingiliwa kinyume ya maumbile!) wa watoto wadogo una madhala gani kisaikolojia, tusipofushwe na ushabeki/umaharufu wa wanamziki wanatumia mwanya huo kufanya mambo mengine ya ziada kwa imani kwamba umaharufu wao ni kinga kamili i.e si rahisi watu kuamini kwamba wanaweza kufanya mambo ya uharibifu kwa watoto wadogo vile vile na wake za watu; baadhi yao tabia zao sio nzuri - wanaonekana ni wapole na wastaarabu lakini chunga sana!