Don't jump into conclusions...ile kesi imeshasikilizwa mara 2 wakaonekana wana hatia. Na ninvyofahamu mimi (kwa uelewa wangu mdogo wa sheria), kesi ya kubaka watoto/mtoto unahitajika ushahidi wa aina 2 tu kukutia hatiani...1 - Mtoto mwenyewe kusema kwamba ni mtu 'huyu' ndio kambaka (wale watoto walipoint kuwa babu Seya na wanae wamewabaka wakahadithia kwa ufasaha walivyofanyiwa), 2 - Daktari kuthibitisha kwa watoto wametendewa kitendo hicho (Daktari alithibitisha hilo, namfahamu Daktari aliyewafanyia uchunguzi wale watoto na ni kweli walifanyiwa hivyo, ripoti na picha ya athari walivyoharibiwa zipo kwenye mafaili yao)....Sioni jinsi gani Babu Seya na wanae watatoka hapo.
zaidi ya hapo, mmoja kati ya majaji wanaoreview hiyo kesi ni jaji Nathalie Kimaro...soma historia yake wakati yuko mahakama ya Kisutu kuhusu kesi za ubakaji na kunajisi watoto!