Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30

Babu Seya/Papii Nguza kweli walibaka? Tukielekea kureview kesi yao oct 30

pitia mahakama ya kisutu usome mwenendo wa Kesi Yao ....walichowafanyia watoto ni cha kusikitisha. Habari za vijiweni zinaporudiwarudiwa zinakua ukweli hasa kwa wajinga an wavivu wa kufuatilia mambo Kama Watanzania.

na kwanini hizi the so called habar za vijiwen ziwe hot??nani alizusha??
Lisemwalooo...........
 
Hadi leo bado mnaumiza vichwa kuhusu hii kesi?... Aliyewafunga yupo pale magogoni... "Mzee wa visasi"....
 
Hii kesi hii itamjambia babaake na nanihii...! Nguza alikamua demu wa mtu jamaa akashangaa yeye akiwa anakamua mwanamama anaimba "seya wa mivalo" jamaa akaona isiwe taabu.. kwa hasira hata panya hakubaki...

daaa hii kali aisee.....
 
hii ni njia ya kuwaachia huru,baada ya watuhuniwa kutumikia hukumu kipindi kirefu.
 
ipo nyingine kutoka CONGO inaitwa Mbago Kasuku,hiyo ni noma,ninayo naiuza buku 15000.
 
Hao watu wawili wote wananunulika kwahiyo sio ishu sana mkuu.

Sikatai...thibitisha kwamba watoto waliobakwa na daktari aliyewachunguza walinunuliwa uwasaidie mabazazi wale watoke waje kubaka binti yako sasa!
 
ipo nyingine kutoka CONGO inaitwa Mbago Kasuku,hiyo ni noma,ninayo naiuza buku 15000.

Kuna moja unapaka kwenye kichwa unazamisha ndani, hii kazi yake ni kuhakikisha hiyo nyapu hagusi mwingine, na hata ukiita usiku wa manane inakuja hata kama ni geti kali.

Ila hii ujiandae kung'ang'aniwa. Nahisi Dogo Domo ndo aliitumia kwa Wema, inapatikana sehemu moja inaitwa Basanza - Uvinza (Kigoma), hii ni noma.
 
Wakuu je hii inaweza kusaidia - yaani wale watoto wajawe na roho ya "u-mama", kama kweli hawakubwakwa basi waende wakaimbie mahakamani ukweli.

Maana kwa sasa watakuwa ni washichana wa miaka 15 -17 hivi.
 
watu wanapopata mashaka kama kweli ilithibitika kuwa wote wa4 walilawiti watoto kwann waliachiwa wawili wakabaki wawili gerezani?hiyo inaleta picha kuwa waliokuwa wanatikiwa ni nguza na papii kocha na sio wale ndugu zao wengine...wake up guyz
Kosa la Nguza ni kufaidi mali za wenzake bila idhini - Kosa jingine ni kuanza majigambo kwamba mama Seya ni balaa kwa viuno - Papi kosa lake ni kushirikiana na babake kuimba wimbo wa majigambo.
 
Hawa jamaa hawakubaka subiri jk aondoke madarakani tuitishe mafaili upya labda awaue kwa sumu huko jela vinginevyo ukweli utawekwa hadharani na kila mwenye sikio atasikia.


Hivi walihukumiwa wakati wa utawala wa nani? Kama wamewekwa ndani kisheria hakuna rais atakaepindisha sheria hasa kwenye tukio kama hili.
 
ipo nyingine kutoka CONGO inaitwa Mbago Kasuku,hiyo ni noma,ninayo naiuza buku 15000.
hakuna cha kutoka kongo wala kishasa, we piga supu ya Pweza uone kama mama nanihii hatakimbilia sebureni, au chumba cha watoto - ngoma ni balaa mwanzo mwisho - mpera mpera hadi kunakucha.
 
mi pia nahitaji hiyo dawa nataka nikatoe shooo embu niapatie hiyo dawa ya kongo mweeh.ya Ngoswe mwachie ngoswe na ya babu seya mwachie babu seya mwenyewe kwanza akitoka sijui kama operesheni kimbunga itamwacha? mweh.
 
Mwenendo mzima wa kesi unapatikana wapi kuanzia madaktari , mashaidi na wanaosemekana ni wahanga ili tuweze kuchangia hoja vizuri.
Mzigo ulikuwa kwa waendesha mashtaka kudhibitisha pasipo shaka kwamba walihusika.

Now unaongea kisomi nipe email address yako nikutupie mzigo...
 
Kazi ipo ,jamani lakini hawa walifingwwa mwaka gani kwani rais alikuwa nani ,just asking
 
Kuna moja unapaka kwenye kichwa unazamisha ndani, hii kazi yake ni kuhakikisha hiyo nyapu hagusi mwingine, na hata ukiita usiku wa manane inakuja hata kama ni geti kali.

Ila hii ujiandae kung'ang'aniwa. Nahisi Dogo Domo ndo aliitumia kwa Wema, inapatikana sehemu moja inaitwa Basanza - Uvinza (Kigoma), hii ni noma.

Watu mna xperience na hizi dawa za kienyeji!
 
Open and read this manual you will get the all proceeding of the case and final judgment
http://www.tawjatz.org/wp-content/uploads/2013/02/Case-Law-Manual.pdf
Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Rufaa, Babu Seya alitiwa hatiani kwa makosa matano ya kubaka na Papii Kocha alitiwa hatiani kwa makosa mawili, wakati Mbangu na Francis hawakupatikana na hatia kwa makosa yote.

“Mrufani wa kwanza amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji kosa la 7 na la 12 kinyume cha kifungu cha 130 (2)(e) na 131A vya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) kama vilivyorekebishwa na vifungu vya 5 na 7 vya SOSPA (Sheria ya Makosa ya Kujamiiana),” ilisema hukumu hiyo na kuongeza:

Kwa kosa la 10 na 18 warufani namba moja (Babu Seya) na namba 2 (Papii Kocha) wamepatikana na hatia ya ubakaji kinyume cha kifungu cha 131A cha Kanuni ya Adhabu.

Hata hivyo katika kosa la 1,3,5,14, 20 na 22, warufani wote hawakupatikana na hatia, wakati katika kosa la 7 na 12 mrufani namba 1 mpaka namba 4 hawakupatikana na hatia huku kosa la 10 na 18 yakiwaondoa mrufani wa tatu (Mbangu) na wa nne (Francis).

“Hatimaye, hatia kwa mrufani namba tatu na wa nne inatanguliwa na hukumu pamoja na amri ya fidia inatupiliwa mbali. Wamewekwa huru isipokuwa kwa sababu nyingineyo. Na kwa mrufani wa kwanza na wa pili amri ya fidia bado inasimama tu kwa makosa ambayo yamewatia hatiani na inatupiliwa mbali kwa makosa yaliyobaki ambayo hayakuwatia hatiani,” ilisisitiza hukumu hiyo.

Mara baada ya Chusi kusoma hukumu hiyo majira ya saa 4:22 asubuhi, baadhi ya warufani hao waliangua kilio wakiwa kizimbani hususan Francis ambaye aliangua kilio kwa sauti kuu, huku Papii Kocha machozi yakimtiririka, lakini Babu Seya na Mbangu wakionekana kujawa na huzuni.

Chusi alianza kusoma hukumu hiyo kwa kuelezea kumbukumbu za mwenendo mzima wa kesi hiyo, akielezea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote katika kesi ya msingi, hukumu ya rufaa ya kwanza ya Mahakama Kuu na hoja zilizotolewa na pande zote katika rufaa zote.

Kisha alisema; “Suala lililoko mbele yetu sasa ni kama ushahidi katika kumbukumbu ulithibitisha utendaji wa kosa. Kama ambavyo tayari imeshaonyeshwa PW 9 (Shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka alikuwa ni mtoto wa miaka saba na alitoa ushahidi bila kiapo, ushahidi wake ulihitaji kuungwa mkono."

Katika ushahidi kwenye kumbukumbu hakuna mashaka kuwa PW9 alibakwa. Alithibitisha na kulikuwa na ushahidi wa PW20 kuwa PW9 alibakwa na PW9 alisema waomba rufaa ndio walimbaka.

Alisema jambo la msingi lilikuwa ni kuthibitsha kama waomba rufaa ndio walimbaka.

“Tumekwishatoa maoni juu ya mashahidi wa upande wa mashtaka na hatuhitaji kurudia kile ambacho tumekwishakisema. Inatosha kusema kwamba, kwenye kumbukumbu kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa watoto walikuwa na uwezo wa kuingia katika nyumba ile bila kuonekana,” alisema Chusi.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa hali ya nyumba iliyodaiwa kufanyika makosa yale kupitia kwa PW13, unaonyesha kuwa kulikuwa na mlango ambao ungeweza kutumiwa na watoto kuingia ndani ya nyumba ile namba 607 bila kuonekana.

Alisema kilichounga mkono ushahidi huo ni mazingira ya chumba cha mrufani wa kwanza (Babu Seya) ambamo ndimo kulimodaiwa kufanyiwa ubakaji, ambapo PW9 alieleza kuwa kuna godoro kitandani na godoro lingine ukutani na kwamba watoto wengine walikuwa wakilazwa kitandani na wengine kwenye godoro sakafuni.

“Tumesema mwanzoni mwa hukumu hii kuwa waathirika wa makosa ya ubakaji walikuwa ni watoto 10 na ushahidi wao katika maelezo yao kuhusu chumba cha mrufani wa kwanza unafanana,” alisema.

Akizungumzia utetezi wa Babu Seya kuwa alikuwa na matatizo ya nguvu za kiume na hivyo asingeweza kutenda kosa kama hilo na kwamba upande wa mashtaka ulikataa kwenda kumpima ili kuthibitishwa na daktari kama ana uwezo au hana uwezo wa kutenda kosa la ubakaji, mahakama iliutupilia mbali.

“Kwa maoni yetu upande wa mashtaka haukuwa na wajibu wa kufanya hivyo,” alisema Chusi katika hukumu hiyo na kuongeza:

“Tunasema hivyo kwa sababu katika kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ushahidi (LEA) sura ya 6 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 suala la uwezo wa nguvu za kiume za mrufani ilikuwa katika ufahamu wake na suala la kuthibitisha lilikuwa juu yake kuthibitisha kuwa uume wake haukuwa ukifanya kazi”.

Mahakama pia iliongeza kuwa ingawa kulikuwa na mazoezi katika nyumba hiyo(wanamuziki wa Bendi ya Akudo) haikuwa sababu ya kumzuia mrufani wa kwanza kutenda makosa kwa kuwa, kwa mujibu wa ushahidi matukio hayo yalikuwa yakifanyika kwa muda mfupi sana wakati wa mapumziko na wakati watoto hao wakitoka shule.

“Zaidi hakuna sababu kwa nini watoto wote hao waseme uongo dhidi yake na alikiri kuwa hakuwa na uhasama na mmoja wapo,” iliongeza.

Kuhusu mrufani wa pili Papii Kocha, mahakama katika hukumu hiyo ilisema utetezi wake kuwa hakuwepo hauondoi uwezekano wa kutenda kosa.

“Tunasema hivyo kwa sababu kama ambavyo tumekwishaonyesha makosa yalikuwa yakitendeka kwa muda mfupi kama saa moja tu. Hii ina maana kwamba, hata kama mrufani wa pili alikuwa akifanya shughuli za kutumbuiza nje ya Dar es Salaam, lakini kuna wakati ambao alikuwa Dar es Salaam;

Kwa mujibu wa utetezi wake alikuwa akitoka nje ya Dar es Salaam kwa vipindi na si muda wote. Kwa namna hiyo hatuoni sababu yoyote PW8 ( mmoja wa watoto waathirika) kutengeneza ushahidi dhidi yake. Alikuwa ni mtoto mdogo ambaye hakujua hatari iliyokuwa mbele yake kwa kujihusisha katika, matendo ya ngono katika maisha yake”.

Katika hukumu hiyo mahakama ilichambua ushahidi wa kila mtoto na kueleza jinsi ulivyoweza kuungwa mkono na mashahidi wengine, wakiwemo madaktari waliowafanyia vipimo baadhi ya watoto hao na kuthibitisha kuwa walikuwa wameingiliwa.
SOURCE: MWANANCHI Imeandikwa na James MAGAI na HUSSEIN Kauli

Soma zaidi: Mzee wa Mshitu: Babu Seya, Papii basi tena!!!
 
Back
Top Bottom