Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake.

Mojawapo ya tukio la ajabu ni pale Diddy alipowakaribisha juu ghorofani wakaangalie runinga. Lakini mwenyeji wao waliyeenda naye, Produza Swizz Beatz aliwakataza kata kata. Na hata wakati wanaondoka hawakuagana na P Diddy.

Pia soma: Kitendo cha Diamond Platnums kwenda nyumbani kwa P. Diddy kimemlipa

Kesho yake Swizz alikuwa na party pia, walienda kushiriki na baada ya kumaliza Swizz aliwaonya tena wasije wakajaribu kwenda nyumbani kwa Diddy, Swizz aliwakabidhi kwa dereva awarudishe hotelini, huku akimpa maonyo makali dereva asije akajaribu kuwapeleka mahali popote.

Akihojiwa na Rick Media, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja wa msanii nguli Diamond Platnumz, Mh. Hamis Taletale au kwa jina maarufu Babu Tale amekiri walipoenda kumtembelea msanii P.Diddy, alionesha viashiria ambavyo wao hawakujua maana yake.

Mojawapo ya tukio la ajabu ni pale Diddy alipowakaribisha juu ghorofani wakaangalie runinga. Lakini mwenyeji wao waliyeenda naye, Produza Swizz Beatz aliwakataza kata kata. Na hata wakati wanaondoka hawakuagana na P.Diddy.

Kesho yake Swizz alikuwa na party pia, walienda kushiriki na baada ya kumaliza Swizz aliwaonya tena wasije wakajaribu kwenda nyumbani kwa Diddy, Swizz aliwakabidhi kwa dereva awarudishe hotelini, huku akimpa maonyo makali dereva asije akajaribu kuwapeleka mahali popote.

View attachment 3106362
Hizi nyingne Sasa ni kutafuta Kiki sio Bure🤔
 
Didy did it
1000220261.jpg
 
Back
Top Bottom