Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Mkuu.
mchango wako poa tu lakini umeutia kasoro hapo penye rangi ya buluu. Katika hao wanaokwenda kwa babu wamo wanaokwenda msikitiki. Pia ni wananchi na watanzania wenzako.

Naelewa kuwa maamuzi mengi ya serikali iliyopo hivi sasa yanaudhi na yanaumiza wananchi lakini huwatendei haki hao wanaoingia msikitini kwa kauli yako. Wao pia wanaumia na maamuzi ya "hawa majuha". Na kauli yako hiyo ni kiashiria cha ubaguzi au unahubiri mgawanyiko wa wananchi wenzako?

hujamuelewa mdondo we mtu, seems wewe watokea mikoa ilee isikijua kiswahili vyema
 
Lazima wamzuie, Semina na makongamano ya ukimwi na kansa zitaisha huko wizarani, kakobe atafurahi sana atajua ni maombi yake
 
Ndugu yangu usemayo ni sawa lakini ili huduma yoyote ya kiafya iweze kuwa authorized mahali popote duniani ni lazima ithibitishwe na mamlaka husika ya afya,zipo traditional medicine therapy nyingi duniani kama kule china,india hata ulaya lakini zote hizi zinakuwa zimepata baraka kutoka mamlaka husika,hata hapa nchini kwetu regional hospitals na referral hospitals zina vitengo vya wataalamu wa tiba asilia na wote wana baraka kutoka wizarani,hivyo wizara inafanya hivyo ili kujiweka on the safe side na vile vile ni kuhakikisha kuwa hiyo dawa iko salama isije wadhuru consumers baadae kwa sababu dawa uliyokunywa leo unaweza kuona madhara yake even 5-10 yrs later,mimi nafikiri sio jambo baya ili mradi huo utafiti ufanyike kwa haraka na ikithibitika dawa ni nzuri na haina madhara babu aendelee kutoa huduma.

we babaa utafiti watanznia tuna uwezo gani wewe bana? miti shamba haidhuru, after all wagonjwa wenyewe washadhurika na ugonjwa so hakutakuwa na jipya itakuwa ktk kujaribu, hapa tunataka tu uje kusikia dawa ya ukimwi imevumbuliwa MAREKANi kumbe ndo hiyooo ya Loliondo kwa Babu, TFDA hawana uwezo huo, i know them ni watu wa low caliber sana, they acts more like a police but not scientific authority! 24formula , hatuna jeuri ya kustart from scrach na utafiti wa dawa bana!
 
Sasa huo unga watajuaje umechanganya mizizi gani? lazima waone kitu original.
Nliweka kila aina ya dawa kwenye chombo maalumu,nikaweka namba.
So walitakiwa wapime na majibu watoe kufuatia namba.
Si kunambia niwape sample kilo moja .
Huo ujanja bado hawajafaulu.
Hata hivyo wanaonijua wanafurahia huduma hiyo.
Watu wakisukari wanapewa masharti mengi lakini wakitimia dawa hiyo wanafurahia sana.
Pia nimeiboresha sasa unaipata kwa juice na hukaa muda mrefu bila kuharibika.
Kuna mtaalam aliniomba nimpe kanuni ili aifanyie PhD.
 
Serikali ina jukumu la kutunza afya za watu wake. Hawa 6 ambao wameshakufa wakiwa njiani ni alarm ya kutosha kuwa lazima hatua zichukuliwa haraka. kwanza kuangalia mazingira halisi ya wagonjwa na huduma zilizopo kama maji, vyoo nk. Kwa kitalaamu, wale wagonjjwa waliopata dawa wanahitaji kujitoa wafanyiwe uchunguzi ili kukubali au kupinga haya anayodai huyu Mzee. Nina wasiwasi, kwa sababu kama kweli kuna watu waliopona wangekuwa wameshatoa ushuhuda
 
Yule babu wa Loliondo aliyepata umaarufu kwa muda mfupi kutokana na dawa yake kutibu magongwa sugu amefungiwa kuendelea ma kutoa dawa kwa wagonjwa na wizara ya afya,wizara imesema inataka kuifanyia utafiti dawa hiyo pia wamemsauli mchungaji huyo mstaafu kuisajili dawa yake mamlaka ya chakula na dawa(TFDA). Source.Channel ten habari ya saa 7 mchana.

Hii taarifa ingesuburi Aprili 1. Kwani utoaji wa dawa ni sehemu ya ibada kwa
Mchungaji Mwasapile.
 
SERIKALI IMEKOSEA. Haikupaswa kusimamisha huduma za babu. Walichotakiwa kufanya ni

1. Kuchua sample ya dawa na kupima kama ina vitu vyovyote ambavyo ni toxic kwa binaadamu, kazi ambayo huweza kufanyika siku moja tu.

2. Wakithibitisha kuwa haina sumu yoyote ile then wangetoa tamko lifuatalo : Serikali haina uhakika wala uthibitisho wa dawa hiyo kuponyesha, kwa kuwa Tanzania ni nchi huru, na tumeona kuwa kunywa dawa hiyo haina madhara kiafya, basi wakati serikali inaendelea na utafiti wake mtu yeyote atakaye enda kunywa dawa hiyo afanye hivyo kwa hiyari yake na imani huku akijua kuwa serikali haijathibitisha uwezo wa dawa hiyo kuponya.

3. Serikali itaendelea kuratibu hali ya amani ya watanzania watakaotaka kuelekea huko kwa ridhaa yao kwani jukumu letu kulinda usalama wa raia na mali zao. Kuhakikisha hilo linafanyika serikali inaomba watu watakaotaka kuelekea huko wajiandikisha mikoani ili tuweze kuwapa utaratibu wa jinsi ya kutimiza uhuru bila kuhatarisha usalama wao.

4. Serikali inatahadharisha kuwa kwa kufanya mambo haya haina maana kuwa imekubaliana na dawa ya mchungaji kwani hilo litathibitishwa kitalaam katika maabara, hatua hizi zinachukuliwa kuhakikisha usalama wa raia watakataka kwenda huko huku wakijua fika kuwa dawa hiyo haijathibitika kitaalam kuponya mpaka hapo serikali itakapokuwa na matokeo ya kisayansi.

KUMPIGA MARUFUKU BABU KUENDELEA KUTOA DAWA KISAIKOLOJIA KWA UPANDE WA WAGONJWA SI JAMBO JEMA, NA ENDAPO MTU ATAPOTEZA NDUGU YAKE KATIKA KIPINDI HIKI AMBACHO SERIKALI IMEMPIGA MARUFUKU BABU, ATAILAUMU SERIKALI MUDA WOWOTE ATAKAOKUWA ANAMKUMBUKA MPENDWA WAKE ALIYEMTOKA NA KUSEMA "HUENDA ANGEKUNYWA MAJI YA BABU ASIMGEFARIKI". SERIKALI IACHE FREE MARKET IFANYE KAZI, KAMA WATU WALIOKUNYWA BAADA YA MWEZI AU MIEZI MIWILI WAKITHIBITISHA KUWA HAWAJAPONA BASI WATU WATAACHA KUELEKEA HUKO.

HUKU NI KUKURUPUKA NA KUONESHA KUWA SERIKALI BADO INA MAWAZO YA ENZI ZA UJIMA ZA KU-CONTROL MAISHA YA WATU.
 
Mi naona aibu kwenda coz ni mtu mzito sana halafu kwenda natamani sasa nifanyeje?

Mkuu kwenye maradhi hakuna kitu kama utu uzito, nenda kajaribu huwezi jua labda wakati wako wa kupona ndo umefika. Kuna msemo unasema " mficha maradhi, mauti humuumbua" , nenda sasa na tena uwahi maana dawa inaweza kuisha!
 
hujamuelewa mdondo we mtu, seems wewe watokea mikoa ilee isikijua kiswahili vyema
Mkuu.
Inawezekana mie si mweledi wa lugha ya kiswahili.
Pia ungenisaidia kama ungenielewesha kwa lugha rahisi ili nipate ujumbe uliokusudiwa.
Nitafurahi sana ukifanya hivyo.
jee ule katika rangi ya buluu ni msemo mpya katika kiswahili? Kama ndiyo..maana yake nini?
 
Yule babu wa Loliondo aliyepata umaarufu kwa muda mfupi kutokana na dawa yake kutibu magongwa sugu amefungiwa kuendelea ma kutoa dawa kwa wagonjwa na wizara ya afya,wizara imesema inataka kuifanyia utafiti dawa hiyo pia wamemsauli mchungaji huyo mstaafu kuisajili dawa yake mamlaka ya chakula na dawa(TFDA). Source.Channel ten habari ya saa 7 mchana.

Niliwaambia mimi hapa asubuhi ya leo. Wizara ya afya ipo zaidi kisera na sio kimaslahi ya wananchi. Hata kama sera zitakuwa butu watazikomalia tu kwa sababu ndicho walichoajiriwa kukilinda. Labda zikiwemo kwenye upatu wa uchaguzi. Hayo ni matokeo ya wale aliowatolea nje, sasa wanaonyesha ubabe tu, hawana kipya. Wagonjwa wa ukimwi wakipona wengi watu wa wizara watakula wapi wakati kila kukicha kauli za ukimwi ndizo zinazowapa kula? Mzee wa Loliondo kawashika pabaya serikali na kwa kawaida hawatakubali. Hapo ndio mwisho wa tiba yenyewe mpaka Mungu afungue njia mbadala.
 
Nilijua kua hawa majuha watafanya hivyo baada ya wao kupata dawa.
Basi tena tumain limepotea kwa wagonjwa

Ndio, hukumbuki DECI, watu wa serikalini walipovuna wao na kujinufaisha sana wakatafuta visingizio na kuizima, maana kila mwana-DECI alikuwa na hela ya uhakika na walikuwa wanashindana na watu wa serikalini kufungua miradi mikubwamikubwa kwa mitaji ya DECI waliyijipatia. Hata hapa si umesikia vigogo kadhaa wameenda kutibiwa na sasa wanazua mambo ili wasipone wengi nao waendelee kuishi kwa migongo ya wagonjwa hao? Tangu lini kupona kwa sala kunatungiwa sera serikalini?
 
kwa wale wanaofikiria Nje ya BOX ...This is pure case of placebo effect. Huyu babu he is a priest "man of god" claim he saw this herb in his dream.. wht u except..? if u know about placebo effect u will have ur answer why people who are going to see him thy are getting better!!... P.L.A.C.E.B.O !! ... !
 
Kwa kuwa huna imani nakushauri usiende, endelea kutumia dawa za hosp. Pia kama ulikuwa hujui Babu hachukui hata senti katika 500 inayotolewa 300 inakwenda kanisani 200 ya wasaidizi wake 6. Yeye anakula chakula wanachopika wasaidizi wake.
 
Mi naona aibu kwenda coz ni mtu mzito sana halafu kwenda natamani sasa nifanyeje?

Watu wazito hao wanaumwa na hata kufa kwa hiyo hakuna atakayekushangaa na hata akishangaa ni wewe na maisha yako. Mungu wako ndio anajua atatumia njia gani kukusaidia. basi mwombee akutie nguvu.
 
Jamani mi nimeona vitu lakini hiki cha loliondo kimenishtua sana, kwasababu Mzee huyu ni wa ajabu na ameweza kujipatia njia nzuuurii ya kutafuta Pesa bila kutumia unyang'anyi wala Ndumba, bali kwa kutumia Akili yake.
Hakuna uthibitisho wa kisayanxzi kwamba dawa hiyo inaponesha, na kimachoshangaza Eti Dawa hiyo huponi ukichota mwenyewe mpaka achote kwa mkono wake.
naomba tuwege makini, na naomba uthibitisho ili na mimi niende bana

Eti wadau ni njia ya kutafuta Ela au Dawa kweli?
JE WEWE NI TAJIRI KAMA KUNA NJIA NYINGI?
pale ni swala la imani yako a sio physiological manupulation ili upone.
INGEKUWA NI KUTAFUTA UTAJIRI basi angeuza dawa kwa laki kadhaa kwani nani angemzuia wala kumgomea?
 
Ina maana babu hajatoa hata namba ya account tuchangie huduma! Anyway tenda wema nenda zako usitizame nyuma. Anachofanya babu ndiyo utumishi wa kweli yeye hayuko kibiashara na hii inadhihirisha babu kweli katumwa na Mungu kuokoa watu. Zidumu harakati za babu. Vipi mustakabali wa akina ndodi??

ndodi na mafisadi wenzie(kakobe, gwajima ,lusekelo, getrude,etc wameanza maombi ya kufunga ili kumumaliza nguvu babu.............., si mchezo.
 
kwa wale wanaofikiria Nje ya BOX ...This is pure case of placebo effect. Huyu babu he is a priest "man of god" claim he saw this herb in his dream.. wht u except..? if u know about placebo effect u will have ur answer why people who are going to see him thy are getting better!!... P.L.A.C.E.B.O !! ... !

Do you REALLY KNOW the meaning of PLACEBO and what it has an effect on?......au umekurupuka tu?.....nenda kasoma uelewe.
 
Nashangaa dawa ya babu lazima ifanyiwe utafiti. Mbona kuna dawa nyingi sana tunakunywa hazifanyiwi utafiti. Kamba kombe mtu akipiwa anywe unajuaje kama ni salama. Yote unakubali kutokana na imani tu. Sasa watafanya utafiki yote haya na mengi tu ambayo watz wanakunywa kwa ajili ya kuhangaika kujitibu baada ya kukosa huduma za afya za kutosheleza na zinazowatosheleza kutokana na kipato chao. Serikali iache tu watu wawe huru kama mtu anavyojisikia. Isije kuwa kwamba kwa sababu wao wameshakunywa sasa wanafanya fitina kwa wengine. Tuelewe vipi - hospitali nyingine zinasemekana wagonjwa wengi wameenda kwa babu wakapona hawakurudi tena. Kwa waombaji nao wagonjwa baada ya kupona hawakurudi tena kwa vile inaonyesha walikwenda kwa shida tu si imani. Wasije ikawa dawa zao sasa zinadoda kwa hiyo watakosa fedha za kujikimu ndiyo wameamua kumpiga stop babu! Yangu macho nazini kutafakari bila majibu.
 
Kumbukeni kuwa Mungu hadhihakiwi, ya Mungu mpe Mungu na ya Kaisari mpe Kaisari.
 
Nashangaa dawa ya babu lazima ifanyiwe utafiti. Mbona kuna dawa nyingi sana tunakunywa hazifanyiwi utafiti. Kamba kombe mtu akipiwa anywe unajuaje kama ni salama. Yote unakubali kutokana na imani tu. Sasa watafanya utafiki yote haya na mengi tu ambayo watz wanakunywa kwa ajili ya kuhangaika kujitibu baada ya kukosa huduma za afya za kutosheleza na zinazowatosheleza kutokana na kipato chao. Serikali iache tu watu wawe huru kama mtu anavyojisikia. Isije kuwa kwamba kwa sababu wao wameshakunywa sasa wanafanya fitina kwa wengine. Tuelewe vipi - hospitali nyingine zinasemekana wagonjwa wengi wameenda kwa babu wakapona hawakurudi tena. Kwa waombaji nao wagonjwa baada ya kupona hawakurudi tena kwa vile inaonyesha walikwenda kwa shida tu si imani. Wasije ikawa dawa zao sasa zinadoda kwa hiyo watakosa fedha za kujikimu ndiyo wameamua kumpiga stop babu! Yangu macho nazini kutafakari bila majibu.
Mod naomba nisahihishe neno la nne kutoka mwisho liwe "nazidi".
 
Back
Top Bottom