Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

sitashangaa nikisikia ni mradi wa CCM kurudisha hela za uchaguzi....
 
NoNoNonononono wadau naona mumeninukuu vibaya, ni nacho kifanya hapa ni kutoa angalisho maana wagonjwa wa Ukimwi wanawatukana Manurse na Madactari bila kuthibitisha sasa haya yana Effects kubwa ukitaka kurud tena

we umeambiwa nyosha goti mpaka loliondo ukaone mwenyewe au kama hauna ukimwi kaa utulie wenye nao waendelee kupona hiyo ni miujiza. waswahili bwana mbongo akigundua dawa tapeli.... akigundua mzungu utasema hiyo ya kweli ...nyie vipi?????
Babuuuuuuuuuuuuuuu kamuaaaa kamuaaaa

watu wanapona bwana si mchezo
 
Ungepeleka kwenye complain ingeshafanyiwa kazi sio huku haitaonekana kabisa
 
Mwanadamu ana njia nyini za kuuliza au kuuamini ukweli wa jambo fulani,sas ndugu mbona unazunguka sana,wewe nenda tuh,kama una amini nenda kama huaminibasi basi usiende ,usitumie kisingizio cha kusema kuna njia nyingi za kupata utajiri.
 
Kama huamini kaa na maradhi yako au nenda muhimbili ukapate joto ya jiwe.Matusi ya manurse na wataalamu wetu wasio na wito wa kazi.Lkn serikali ndio ya kulaumiwa mishahara ya hawa watu mmmh! Aibu kusema.Jamani twendeni kwa babu
 
Jamani mi nimeona vitu lakini hiki cha loliondo kimenishtua sana, kwasababu Mzee huyu ni wa ajabu na ameweza kujipatia njia nzuuurii ya kutafuta Pesa bila kutumia unyang'anyi wala Ndumba, bali kwa kutumia Akili yake.
Hakuna uthibitisho wa kisayanxzi kwamba dawa hiyo inaponesha, na kimachoshangaza Eti Dawa hiyo huponi ukichota mwenyewe mpaka achote kwa mkono wake.
naomba tuwege makini, na naomba uthibitisho ili na mimi niende bana

Eti wadau ni njia ya kutafuta Ela au Dawa kweli?

Ingekuwa ni dili ya utajiri basi angetoza pesa nyingi sana kama wanavyofanya akina Ndodi sio hicho kiwango cha sh. 500 anachotoza. Kwa hiyo sh. 500 anazotoza ukitoa gharama za uendeshaji unadhani yeye anabaki na sh. ngapi.

Kuhusu suala la dawa yake kuwa ya kweli ama si ya kweli:
1. Nadhani ule umati unaweza kuwa jibu la swali lako
2. Muulize Mahita anaweza kukujibu hilo
3. Akofu Martin Shao na Thomas Laizer wamethibitisha kuwa walishawahi kunywa dawa hiyo na wakapona magonjwa yaliyokuwa yakiwatatiza.
4. Mzee ameanza kutibu kwa dawa hiyo kuanzia mwaka 1991 na waliokunywa wote wanadai wamepona.

Jukumu la kuamini ama kutoamini liko mikono mwako lakini nadhani ukienda utaweza kuthibitisha kirahisi kama ni kweli ama si kweli badala ya kuuliza humu jamvini.
 
wasijidai wanatujari saaaaana, mbona mabomu walitulipua na kutuulia ndugu zetu,na walijua hatari iliyokuwepo. wameona hawana umaarufu tena, wakizani babu kachukua nafasi zao ndio wanaleta ujinga huuu, labda waseme watu ni wengi eneo hilo kuwe kuna utaratibu maarumu wa kufika eneo hilo. ili na babu nae apate muda wa kupumzika. Kwa waliopona na kupata nafuhuu babu ataendelea kuwa shujaa wa Taifa milele.
 
Hii ni sawa, lakini kama serikali inabidi/ni muhimu ijiridhishe pia kwamba dawa hiyo licha ya kuponya kama inavyodaiwa haina madhara mengine makubwa kwa mtumiaji (sasa na baadae). kumbuka ni maelfu ya watu wanapatiwa tiba hii na wengine wanatolewa mahospitalini kwenda huko kwa ajili ya tiba, sasa kama ina madhara ni watu wengi wataathirika na serikali ina jukumu la kulinda afya na maisha ya watu wake.
...yap tupo pamoja ktk kuhakikisha tunamaliza au kupunguza magonjwa haya makubwa yanayotutesa.mawazo yetu wengi ni mazuri ila nadhani kama dawa hiyo ilianza kutumika zaidi ya mwaka naamini kutokana na wingi wa wanaokwenda huko unatokana na wingi wa waliopata nafuu kama si kupona.hivyo nadhani pamoja na nia nzuri ya serikali nadhani kuwa si vyema kusimamisha utumiaji bali ni kuwatumia hao waliotumia kuona wanaendeleaje na wawafanyie check up kisha wawafatilie na hawa wanaotumia hivi sasa tangu hali zao kabla hawajatumia na hadi watakavyokuwa wanaendelea baada ya kutumia
 
Watakapopigana na watu waliopeleka wagonjwa wao huko serikali itasema wamefanya fujo au wamevamia polisi? ama kweli tanzania ni shida tu, kama Mungu akitaka kuikomboa kwa njia yoyote ile, shida inaingizwa, dawa walizonazo hospitalini nyingi zimechakachuliwa, hazitibu tena, zenyewe kufanyiwa uchunguzi, aka! ama kweli mtu masikini kwa tanzania kujikomboa ni mpaka atakapokufa!
 
mpeleke tu gharama zimeshuka nafikiri baada ya yeye kutoa angalizo kwa wale wanopandisha bei
 
Tanzania imejaliwa vitu vingi vya thamani.
1. Mlima Kilimanjaro ulioko kwenye ukanda wa tropiki lakni unatengeneza barafu
2. Serengeti
3. Ngorongoro crater
4. Tanzanite madini pekee yanaypatkana sehemu moja
5. Mchungaji aliyekirimiwa na Mungu dawa ya kutibu magojwa sugu yasiyo na tiba kama:-
i) Ukimwi kwa siku 21 tu
ii) Kisukari - kwa siku moja mtu amepona
iii) Saratani kwa majina yake yoote - kwa siku moja
iv) Pumu
v) Kifafa
Hakuna madaktari wenye tiba ya magonjwa hayo bali hapa Tz vimepatikana kwa gharama nafuu kabisa.

Viongozi wa serikali waliwahi kufikiria kumkamata na kumfunga ili asieneze kitu walichokiita uvumi lakn sasa wanakwenda kuomba kikombe cha tiba yenye upako wa damu ya Yesu.

Nimeenda nikashuhudia mwenyewe watu waliokuwa hawawezi kwa kansa sasa wanasimama kwa miguu yao na kutembea.

BWANA YESU ASIFIWE!!!
 
do you really know the meaning of placebo and what it has an effect on?......au umekurupuka tu?.....nenda kasoma uelewe.

soma nyakati kijana wewe ndio umekurupuka... theres is a Big battle between Virus & science .... unajuwa structure ya virus? unajuwa viral replication ni nini?!! unajuwa stages za cancer? unajuwa cancer ni nini? je kirusi cha HIV unakijuwa..?!! Science inakataa kabisaa explanation za babu na dawa yake ya kuoteshwa .. ndio maana nakwambia ni placebo..!

nakupa mfano... mzee flani alimleta mke wake trauma center mke wake mjamzito... yule mzee akawa anadai na yeye apewe dawa akidai B.P ... alipewa Normal saline!!!! after 5min akawa swaafi kabisaa!!! na kudai dawa imemsaidia! sometimes placebo works ni kiasi cha kuamini tu! but haina maana inaponyesha
 
Kufuatia ujumbe uliotumwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwenda Loliondo kwenda kuangalia uhalali wa matibabu yanayo tolewa na babu inasemekana babu hakuwa tayari kuruhusu wataalam hao kuipima dawa yake. ndugu wanajamii je hiyo imekaaje?

mm ni mkazi wa loliondo na ujumbe huo ulikua haujawasili mida hiyo ya sa2 asubuhi mm nlipotoka kwa babu samunge kurudi loliondo mjini.na suala la kupmwa dawa ya babu, yupo confort na anasema that is spiritual matters,pia katoa onyo jwa wanaopandiha bei ya bdhaa kuwa hakika hawata nufaika,kwani hata amekataa suala la ushuru wa sh2000 eti utakaotozwa kila ajae kunya dawa,pia ukiingilia foleni ametoa onyo kua itakua hujanywa dawa bali ni maji.
Mengi ya kwa babu nmeshuhudia ila kuandika duh!
4more details nipigie kwa 075423809-
 
:A S 13:Kupima waliotumia dawa ndio njia ya kujua ufanisi wake, bila shaka kuna ambao imewapa nafuu ndio sababu wa wengi kufurika kupata dawa hiyo:decision:
 
hata kama ningekuwa ni mimi ningekataa.....wale jamaa wenyewe wamefika kule wakaomba juice ya babu wakanywa na wakapona.....na tena ilikuwa vurugu sana ili wachaguliwe waingie kwenye kamati hiyo
 
mpeleke tu gharama zimeshuka nafikiri baada ya yeye kutoa angalizo kwa wale wanopandisha bei

Ama kwa hakika acheni Mungu aitwe Mungu...amzidishie uhai mrefu huyu babu,,ama kwa hakika sote tuposafarini kuja huko Loliondo..
 
Hawana mamlaka ya kuzuia kazi ya Mungu. Atawaangamiza wote watakaojaribu kuzuia kwa namna yoyote uponyaji huu unaoleta matumaini mapya kwa Watanzania wanaoteseka kwa maradhi sugu.
 
Back
Top Bottom