Babu wangu wa hiyari kaninunia

Babu wangu wa hiyari kaninunia

Ila tusimwazie mabaya bana... Nahisi kwa umri wake alikosa japo mtu wa kumpa kampani...Ni wazi umri unapoenda na kama babu sio mcheshi sana inakuwa vigumu kupata maswahiba hasa vijana hivyo alipoona unamuunga mkono kwa uji akajua amepata rafiki japo wa kumpigisha story... Nakumbuka babu yangu aliniambia, nimekuwa mkiwa mjukuu wangu hata nikionekana bar wananishangaa hata kijiweni vijana wanaondoka hivyo tumia ujana wako vyema uzee ni tabu kubwa...Kufikiri hivyo naomba uongee naye na if possible mwambie nitakuwa nakupa kampani ya uji ila naogopa unene...Akikataa hii offer ujue basi ni mzee mtata hivyo jisogeze pembeni....
unalosema nadhani upo sahihi sababu mara nyingi namuona pekee yake , maskini nitajitahidi leo jioni nikamchokoze akinimind basi ndiyo mwisho
 
hahahahahahah, mwenzio nautafuta kweli unene si nasikia eti "wazee" wanapenda wanawake wanene hivyo nahofu nisije nikawa nje ya fashion, hahahahahahahahahahha. Ngoja nimuombe miss chagga anipe namba za huyo babu ni m convince ahamie Mwanza. hahahahahahahahahaha
ha haha ningeshauri ahame na mama wa uji pia
 
habari za asubuhi wapendwa wangu...

hapa napo tafutia vitu vya kuchafua meza yangu home basi miezi kama miwili iliyopita nilikutana na babu mmoja kwenye lift na dada wa uji ...... ndiyo hapa babu tukaanza kujuana sababu nilimchokoza babu unakunywa uji nikacheka baada ya kicheko nikamwambia msalimie bibi naye akacheka.....na kuniambia karibu uji kama utani, nikasema asante , babu akaamua kuninunulia uji nikaona aibu kukataa sababu yule muuza uji angeona nambania rizki.. me nilitakiwa kushuka kabla yao ila ikanilazimu kwenda hadi kwenye floor ya babu ili nipate uji.... uroho wangu wa uji tukanywa pale tukabadilishana mawili matatu basi nikaondoka...

khee kama bahati mbaya tena nikawa kila siku kama wiki nakutana na babu anaiona kwa mbali mjukuu njoo uchukue uji nami naenda ... offer ya babu ya uji imeenda sasa ni mwezi mmoja na nusu hivi yeye hunisubiri na naenda kunywa uji kwenye floor yake kwa nje tunakula na story huku nikisubiria mda wangu wa kuanza kazi , jumamosi nikapima uzito nimeongeza kilo 2 khee nikaamua jumatatu sasa ni muda wa kukimbia uji wa babu ... kumbe babu naye kaamua kuniwekea bili ya mwezi kabisa ndiyo akawa ananipa taarifa jumatatu mmh nikamjibu babu nimeongeezeka uzito na nahisi ni huu uji wa asubuhi na jioni kama mzazi.....embu nione nimeanza kuongezeka na ninaumbo baya akanijibu nitaacha baada ya kumaliza hii bili aliyoweka , nikasisitiza hapana hapa ndiyo nilipomkosea babu yangu ...

tokea jumaatatu jioni babu naona kaninunia hata nimsalimie haitikii, wala akiniona aniiti mjukuu kwa uchangamfu najisikia vibaya kumfanya babu anune ... lakini pia sipo tayari kunenepa sababu umbo langu nalijua nikijiachia tu nakuwa kama ufunguo.. sasa nawaza nifanyaje babu yangu awe na furaha tena , natamani kumwambia babu nitakuwa nakuja kukupigia story we huku ukinywa uji ila me sinywi ila sasa hata salamu hapokei....

hawa walinzi wa jengo wameniuliza leo babu yako mbona akusubiri tena , nikawaza wanaweza hisi babu alikuwa ananitongoza nikakataa jamani kumbe ni uji tu

siku njema
uji ziko nyingi ujuee
 
Back
Top Bottom