Sikusema kuwa mwanamke asipewe elimu na kuolewa akiwa na elimu si guarantee ya mahusiano kudumuMkuu this is Africa hata sheria tu za kumlinda “mama wa nyumbani” kwenye divorce ni kichefuchefu
Imagine binti yako injinia anakataa ajira au kujiajiri kwa taaluma yake ili ameneji familia yake kwa kuwa mama wa nyumbani halafu mumewe anakuja kum divorce na miaka 45
Narudia tena wajengee mabinti zako mentality za kuja kuwa maRais kama Samia madaktari au mainjinia au kuja kuwa wajasiliamali wakubwa .... nasio kuwaaminisha kuwa “mama wa nyumbani” ni kazi kama kazi zingine
Wazazi wangu wote walikua wanafanya kazi, mimi na mwenzangu tunafanya kazi i do hope my next generation to come will do the same
Point yangu ya msingi ni kuwa si sahihi kusema mama wa nyumbani hana Kazi, ni anayo Kazi tena kubwa sana( tena hizi extended families ) mama anaisimamia familia bado anapewa majina ya kejeli kama "goal keeper, sijuwi beki 3,..........
Mbaya zaidi jamii umefanikiwa kuwa brain wash hata wahanga wanaamini kuwa kumanage familia siyo kazi. Akiulizwa anasema "mimi sina Kazi!" Come on, wakati huo anaisimamia familia ya watu nane wakiwemo watoto wadogo, huku akimsubiria Shemeji yake Mgonjwa atakaye fika hapo nyumbani keshokutwa baada ya kupewa rufaa kutoka huko Kijijini kwao mme wake.