Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Labda EM zipi mkuu?
Za uchochoroni sawa lakini peleka mtoto zile za maana,ana gain vitu vingi sana kuanzia arts, technological advanced,tour nyingi zinazowajenga n.k
Sasa kama Kuna zinazompeleka mtoto mpaka nje,mambugani,na kila kitu unategemea exposure ya huyu mtoto itakua sawa na kayumba ambaye anakuja kujifunza chuo ama akiwa kazini/kaanza maisha.

Walosoma EM wametupita sana,ni vile TU tumekutana nao chuo class moja na kua mabest kibinadamu.Ila uhalisi wanakiangalia kitu kwa tathmini kubwa sana.
Hebu ona wanavyo buni ma-NGO'S,market company zinazofanya kazi na govt na makampuni makubwa.
Hebu ona jicho la fursa kwao lilivyo kubwa.
Wewe wajifunza kufungua company,wao wanafanya simple TU.

Nimeona,Nina hao marafiki yani jambo gumu kwa sisi wa kayumba wao ni simple sana hasa technology za Computer/IT,Magari,design,market,fursa,service company like security,sub-contractor, Accountant company,Law firms,big event preparations, consultant company ktk nyanja mbalimbalin.k
Hivi vitu sisi tunachukulia poa lakini wenzetu wamepata-exposure hizo na Zina run maisha Yao fresh sana
Uongo
 
Haipo hivyo japo umeongea kwa kejeli.
English medium schools are there kupunguza damage kwenye already damaged education structure ya kumfundisha mtoto masomo kwa kiswahili ambacho. Kina limitation kadhaa
Ni. Kama vile mgonjwa wa kisukari anapoambiwa asitumie vyakula vya wanga, haimaanishi kuwa atapona kisukari , bali anapunguza madhara tu.
Nakupa homework rahisi tu rafiki. Angalia idadi ya machawa walipo sasa hvi then nenda katazame walisoma shule zipi? Majibu yatakushangaza sana mkuu.
 
Kiufupi masikinini wa fikra watauona huu Uzi ni WA maana lakini mtu mwenye akili timamu atahakikisha mtoto anasoma shule nzuri angalau hata hizi English medium.wanasiasa wenyewe ambao wanawahamasisha wananchi wasomeshe watoto hizi shule za walala hoi lakini watoto wao huwezi kuwaona kwenye hizo shule maana wanajua hizi shule hazimwandai mtu kuwa na ujuzi mzuri utakaombeba kihadhi ya Dunia.
 
Ameanza 2023 mkuu, sema 2024 ndio emeweka nyuzi nyingi zaidi.

Na Mimi huu ni Uzi wangu namba 2 nilishawahi kupost Uzi hapa kuhusu faida nilizo zipata baada ya kuwatoa watoto wangu ENGLISH mediums.
Tupia linki ya huo uzi mwengine kama kweli hudanganyi
 
Nilifuata ushauri wa Likud Nina watoa watoto wangu shule ya English Mediums.

Niliwatoa mwaka jana katikati. So mwaka huu mzima watoto wangu wamesoma Kayumba.

1. Kwa mwaka huu mzima pamoja na kumalizia kibanda changu na kununua kiwanja kingine,nimeweza kuhifadhi shilingi milioni 8 na uchafu.


2. Hili limewezekana kwa sababu nimewatoa watoto wangu shule ya English Medium.

Nilikuwa nasomesha watoto wa3. Mtoto mmoja kwa mwaka ada tu ni milioni mbili, bado hajaweka usafiri na vikorokocho vingine tuseme ukihesabu na hivyo inakuwa milioni 3 na ushee.

So kwa watoto watatu maana yake ningekuwa nimetoa milioni kumi halafu pia nisingekuwa na akiba yani sasa hivi ningekuwa naumiza kichwa ntapata wapi hela za kuwalia wanangu.

But :

1. Nimehamia kwangu. Watoto wangu wanaishi nyumbani kwababa yao. Nisinge wahamisha hadi muda huu ningekuwa sijajenga wala nisinge kuwa na kiwanja cha ziada wala hiyo milioni nane.

2. Nina kimilioni nane changu ambacho kufikia mwakani mwezi wa kumi na.mbili kwa mipango niliyo iweka itakuwa imezalisha mara kumi yake.

3. Watoto wangu wanasoma shule kifalme. Wanaenda kwa miguu umbali wa kama dakika kumi. Wanakula vizuri, wanalala pazuri, wanavaa vizuri, shuleni wana sare pea tano tano viatu pea tano tano mabegi pea 3 tatu kila mmoja.


Nawasimamia vizuri.

Wanafanya vizuri darasani.

Nimewawekea programme za kitaaluma : home tuition; English, Hesabu na Sayansi plus programme za kitaaluma kupitia kwenye Tv ya nchi 40+ ambayo pengine nisinge weza kuinunua kama wangesoma shule ya Em coz hela yote ingeishia kwenye ada.


Asante sana Likud.

Watanzania wenzangu wenye kipato cha kawaida fikirieni mara mbili. Wacheni kujistress na ada kwenye shule za EM wakati uwezo wenu ni wa kuunga unga.

Kusomea EM at least uwe na networth ya kuanzia walau milioni 150 plus.
Mawazo yako Na yangu yanafanana
 
English Medium schools ni money making scheme kwa wamiliki wa hayo mashule..standard ya elimu ni ileile....unapambana huku chini ili mje kujazana at university level...mkishapata degree zenu mnarudi mtaani kuzungusha bahasha. Kama mzazi unajijua huna biashara, makampuni au assets unazotaka mwanao/wanao waje wazisimamie au waziendeleze basi usijisumbue kumpeleka mwanao huko English Medium. Ni upotezaji wa fedha....hizo 4/5M unazolipa kama ada ya mtoto ili asome EM schools ni bora ukamfungulia fixed deposit account mwanao ili akimaliza masomo apate mtaji wa kuanzia maisha yake mtaani.
Una wazo kama langu huwa nawaza hivihiv
 
Kiufupi masikinini wa fikra watauona huu Uzi ni WA maana lakini mtu mwenye akili timamu atahakikisha mtoto anasoma shule nzuri angalau hata hizi English medium.wanasiasa wenyewe ambao wanawahamasisha wananchi wasomeshe watoto hizi shule za walala hoi lakini watoto wao huwezi kuwaona kwenye hizo shule maana wanajua hizi shule hazimwandai mtu kuwa na ujuzi mzuri utakaombeba kihadhi ya Dunia.
How?
 
Jomba una stress kinyama. Huu ni uzi wako ukisema watoto wako umewarejesha English Medium. Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu.
 
Back
Top Bottom