Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Namie nkupe ushauri uongeze kipato???
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri wa maana kabisa huu na ndicho ninacho washauri watu wafanyeMkuu cha kuzingatia ni tuition tu,tafuta mwalimu mmoja ambae ni kichwa kwenye english na hesabu,awe anawabrush kila siku hata kwa masaa mawili tu,ukimpa laki kwa mwezi hawez ikataa
Ni ule uelewa wa mambo ndiyo maana hata anajua kujieleza! Vitu vingi sana vimefichwa kwenye lugha ya Kiingereza sasa hawa wenzangu na mimi tunateseka sana!kumbe unalipa mamilioni ili mtoto wako ajue kujielezea? Like awe mtangazaji
Kweli kabisa.Nilifuata ushauri wa Likud Nina watoa watoto wangu shule ya English Mediums.
Niliwatoa mwaka jana katikati. So mwaka huu mzima watoto wangu wamesoma Kayumba.
1. Kwa mwaka huu mzima pamoja na kumalizia kibanda changu na kununua kiwanja kingine,nimeweza kuhifadhi shilingi milioni 8 na uchafu.
2. Hili limewezekana kwa sababu nimewatoa watoto wangu shule ya English Medium.
Nilikuwa nasomesha watoto wa3. Mtoto mmoja kwa mwaka ada tu ni milioni mbili, bado hajaweka usafiri na vikorokocho vingine tuseme ukihesabu na hivyo inakuwa milioni 3 na ushee.
So kwa watoto watatu maana yake ningekuwa nimetoa milioni kumi halafu pia nisingekuwa na akiba yani sasa hivi ningekuwa naumiza kichwa ntapata wapi hela za kuwalia wanangu.
But :
1. Nimehamia kwangu. Watoto wangu wanaishi nyumbani kwababa yao. Nisinge wahamisha hadi muda huu ningekuwa sijajenga wala nisinge kuwa na kiwanja cha ziada wala hiyo milioni nane.
2. Nina kimilioni nane changu ambacho kufikia mwakani mwezi wa kumi na.mbili kwa mipango niliyo iweka itakuwa imezalisha mara kumi yake.
3. Watoto wangu wanasoma shule kifalme. Wanaenda kwa miguu umbali wa kama dakika kumi. Wanakula vizuri, wanalala pazuri, wanavaa vizuri, shuleni wana sare pea tano tano viatu pea tano tano mabegi pea 3 tatu kila mmoja.
Nawasimamia vizuri.
Wanafanya vizuri darasani.
Nimewawekea programme za kitaaluma : home tuition; English, Hesabu na Sayansi plus programme za kitaaluma kupitia kwenye Tv ya nchi 40+ ambayo pengine nisinge weza kuinunua kama wangesoma shule ya Em coz hela yote ingeishia kwenye ada.
Asante sana Likud.
Watanzania wenzangu wenye kipato cha kawaida fikirieni mara mbili. Wacheni kujistress na ada kwenye shule za EM wakati uwezo wenu ni wa kuunga unga.
Kusomea EM at least uwe na networth ya kuanzia walau milioni 150 plus.
Halafu wewe wa kwako unasomesha shule za maana!Ushauri wa maana kabisa huu na ndicho ninacho washauri watu wafanye
Hiyo ni propaganda tu mkuu wala usiogopemm huwa napenda kuangalia vipindi vya shule vile vinavyorushwa kwenye tv. kwakweli ukiona watoto wa kayumba wanavyoulizwa maswali na majibu yao huwezi kufanya maamuzi kama haya labda km hauna uwezo inaeleweka.
Nilitaka kucoment haya uliyoyaandika, lakini nikaona bora nipitie comments za wenzangu kwanza niepuke duplication.Hesabu zinakataa. Watoto watatu kwa mwaka milioni 9, sasa wewe umewatoa katikati ya mwaka ina maana ela ambayo ulipaswa kusave ni milioni nne na nusu.
Tuseme kweli umesave ya mwaka mzima. Yani milioni 9 ndiyo ikufanye ujenge, ununue kiwanja, na uwe na saving ya milioni 8.
Wewe ulikuwa hujafanya hayo yote si kwa sababu ya watoto kusoma english medium ila kwa uzembe wako tu.
Laki kwa mwezi, masaa mawili halafu mwalimu kichwa? Labda walimu wa serikalini, au wasome kama kundi (si one-on-one) plus, mwalimu awe average.Mkuu cha kuzingatia ni tuition tu,tafuta mwalimu mmoja ambae ni kichwa kwenye english na hesabu,awe anawabrush kila siku hata kwa masaa mawili tu,ukimpa laki kwa mwezi hawez ikataa
Mbona hesabu ndogo sana hiyo. Hiyo pesa ambayo alikuwa haitoi ada maana yake ni kwamba alikuwa anaizungusha kwenye biashara.English Medium schools ni money making scheme kwa wamiliki wa hayo mashule..standard ya elimu ni ileile....unapambana huku chini ili mje kujazana at university level...mkishapata degree zenu mnarudi mtaani kuzungusha bahasha. Kama mzazi unajijua huna biashara, makampuni au assets unazotaka mwanao/wanao waje wazisimamie au waziendeleze basi usijisumbue kumpeleka mwanao huko English Medium. Ni upotezaji wa fedha....hizo 4/5M unazolipa kama ada ya mtoto ili asome EM schools ni bora ukamfungulia fixed deposit account mwanao ili akimaliza masomo apate mtaji wa kuanzia maisha yake mtaani.
Mafundi nyumba pia nao wasinge pata kazi za ujenzi kutoka kwake, lakini bank pia zimepata kuaminiwa na jamaa kaweka 8m bank, dukani wameuza pia TV na mafundi cherehani nao wameshona uniforms za watoto wake; mwamba kazungusha pesa kwa wengine as wellHizo English medium kuna watanzania wenzako wameajiriwa huko na wanaendesha maisha yao na kuhudumia familia zao.
Kampeni na ushuhuda huu si afya Kwa taifa.
English Mediums hizi hizi?Kuna exposure kubwa sana English medium ambayo ni standard,mtoto anakua ktk Dunia ya kwanza ktk utambuzi WA mambo.
Tumekutana nao chuo,wamegusa kidogo TU ma-solid work na wengine ma-platform makubwa ya kibiashara wakati sisi tunahangaika na introduction to computer,Wao wanapiga project za mamilioni.
Ushauri,jikune unapoweza ila kama utapamudu EM mpeleke,hizi kayumba za sasa si zile za miaka ya 2005 kurudi chini,Watoto wanatoka mazezeta sana.
Bora akajifunze hata kuchora huko EM awe kua artist au architect wa mchongo badae apigepige hela kabla watu hawajasanuka
😂😂😂😂Mafundi nyumba pia nao wasinge pata kazi za ujenzi kutoka kwake, lakini bank pia zimepata kuaminiwa na jamaa kaweka 8m bank, dukani wameuza pia TV na mafundi cherehani nao wameshona uniforms za watoto wake; mwamba kazungusha pesa kwa wengine as well