Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Kimsingi Kumpeleka Mtoto Shule ya Kulipia au ya Serikali kunatakiwa kuzingatia mambo matatu:

Kwanza Kiwango chako cha Kipato
Uwezo wa Mtoto Darasani
Kiwango Cha mzazi kielimu
Malengo ya Mzazi kwa mtoto wake
Malengo ya Mtoto
Aina na Ubora wa shule Husika
Uwezo wa mzazi kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya Mtoto

All in All baada ya Kuhitimu masomo Kwenye Game ya maisha huwa Rules zinakuwa zile zile.So Kabla hujamlipia mwanao Ada Milioni 50 Jiulize Hio Milioni 50 unaweza fanya nayo nini Kingine.
 
Labda Kama mtu hana uwezo wa kulipa ada za private schools.
Kingereza cha wanafunzi wengi waliosoma shule za serikali huwa sio kizuri.

Kingereza ni lugha ya dunia na kinafungua milango ya fursa nyingi (hasa za ughaibuni).

Au nimeandika uongo wakuu.
Kwahiyo tulipe milioni 6 kwa ajili ya kingereza 😂😂😂😂
 
Kimsingi, NECTA ni NECTA.
Content ya curriculum ni ile ile.
Tofauti ni lugha tu.
Sasa, kama unampeleka mtoto English Medium ambayo walimu Wana kiingereza kibovu, hakuna extracurriculars, hakuna activities ambazo zina lengo mahsusi la kukuza positive personality ya mtoto, basi muache tu Kayumba.

Alternatively, ukiwa na uwezo mpeleke mtoto shule za mitaala ya kimataifa kama IB na Cambridge. Tofauti itakuwa obvious.
 
Ni kupoteza pesa tu, wanaosoma kwenye hizo shule hawana ubunifu wowote, ni sawa na kuku broiler vs kuku wa kienyeji.

Kama pesa ipo, peleka mtoto kayumba mpaka kidato cha nne, baada ya hapo kamlipie kozi ya urubani na nyinginezo unazoona zinafaa; lakini kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kujifunza a for apple ni kupoteza pesa.​
 
Mie vijana wangu wote nmewapeleka EM ila gov school, ada laki 4 kwa mwaka, wanakula asubuh na mchana hapo shule, hiyo laki 4 huwa naona kama nimechangia tu hela ya chakula
Ni braza moja kati ya wasomi wa kitaani kwetu. He was born in 1980. He is 5 years older than me. Darasani alikuwa very smart. Ni wale the cream wa Azania wa Enzi hizo.

To cut story short. Jamaa alikuwa mtumwa mwaminifu wa Shule za Ems. Amepunwa ile kinoma Noma. Kwanza Watoto wawili wa kwanza . Hawa aliendelea kupunwa hadi seco kawapeleka shule wanalipa ada tu milioni 6. Dogo wa kiume kamaliza form four kagoma kwenda Advance kasema anataka kwenda college. Kozi Aliyo ichagua sasa " PROCUREMENT ". Ule utoto aliokuwa anamwambia baba ake alipokuwa primary " Daddy I want to be a pilot, lawyer, Doctor or Engineer blah blah blah" ukawa ume evaporate.

Jamaa alikuwa so much dis appointed . Nakumbuka wakati wa Corona aliwahi niuzia kiwanja kwa bei ya Chanika halafu hela yote akaenda kulipa ada shuleni. Sehemu yenyewe aliyoniuzia kiwanja ni very potential area. Japo kiwanja sio chake ni cha urithi but aliniuzia kwa bei ya chini.

Mwaka mmoja baadae akataka nimtafutie mteja amuuzie kiwanja chake kingine alipe ada za watoto.

Nikamkalisha chini nikampa somo kuhusu shule za Kayumba. Nikamwambia warudishe wanao Kayumba. Watoto watatu sio poa. Mapacha wawili wa kike plus mdogo wa mwisho, kwa kipato chako sio kweli bro. Hata hivyo hakuna umuhimu wowote wa wewe kulipa hela yote hiyo kwa ajili ya Elimu ya msingi ya mtoto.

Toa watoto wako Em walete Kayumba. Mbona Mimi nimewatoa na wako poa tu.

Jamaa akawa inspired na ushauri wangu. Akawatoa watoto wake wote watatu Ems akawaleta Kayumba. Hao mapacha wawili ndio wamefaulu wamepata A zote na mdogo wao anafanya vizuri sana shuleni.


Jamaa kuandika gazeti refu sana ananishukuru mdogo wake kwa ushauri ambao pia umemsaidia kusave pesa na kuinvest kwenye mambo mengine.


Comments za wadau sasa. Kuna comments za watu kama sita ambao nao pia waliwatoa watoto wao Ems wakawaleta Kayumba. Wadau hao wanasema walikuwa inspired na Mimi. Baada ya kuona hadi Mimi nimewarudisha watoto wangu Kayumba. ( Aina ya maisha ninayo ishi na vitu ninavyo vimiliki ambavyo watu wa mtaani kwetu wanavijua, wanaona watoto wangu hawastahili kusoma Kayumba. Mimi kuwapeleka watoto wangu Kayumba ni jambo linalo tengeneza sentensi " kama Likud kawatoa watoto wake Kayumba Mimi nani)

Wengi walio watoa watoto wao Ems na kuwaleta Kayumba wanashukuru sana na wanajilaumu kwanini hawakufanya hivyo mapema.

Hata wewe mzazi unae jistress kulipia mamilioni kwenye shule za Ems wacha mara moja. Haraka sana kimbia kawatoe watoto wako EMS walete Kayumba. Huna sababu yoyote ile ya kujistress kulipa mamilioni huko EMs . N real sense,Shule za Ems hazina umuhimu wala UPEKEE wa aina yoyote ile. Umuhimu na upekee huo umetengenezwa na Wamiliki wa shule za Ems ili waendelee kukupuna.

Mtu muhimu kuliko wote kwenye shule hizo ni wewe mzazi kwa sababu wewe ndo unaelipa ada na ndio sababu kuu kwanini mmimiki kaanzisha shule hiyo.


Kilaza atasema " Likud huna hela "

Situmii hela hovyo kwa sababu ninazo.

Enyi wazazi ambao watoto wenu wamefanya vizuri kwenye shule za Kayumba enyi wazazi ambao mliwatoa watoto wenu Ems na kuwaleta Kayumba na wamefanya vizuri,acheni ubinafsi. Hakikisheni mnashare hizo information kwa watu wengi iwezekanavyo ili kuwatoa usingizini wazazi ambao bado wamelala. Wazazi ambao wana jistress kulipa mamilioni kwenye shule za Ems
 
Ni kweli shule za private ni hard na za kayumba ni hard so choose your hard . Uncle alipeleka wanae wote private ila mpaka sasa wamempa maumivi million na ushenzi mmoja alipofika six kaolewa na mzungu, mwingine kaenda kwa bwana , mwingine kaenda nae hivyo last kapull off wote pesa zimepotea na hana kitu
Aisee 🤔
 
Back
Top Bottom