Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Hata mimi nilichukua uamzi huu. Masela wangu wananipongeza kila siku jinsi nilivyowazidi kete.

Unatema mshahara wako wote kulipia Nursery utakuwa huna akili.

Wacha walamba asali wafanye na kama una mpunga wa kutosha sawa. Ila kama unauza viwanja vya urithi na kuingia mikopo wewe ni Limbukeni tu.
Ndo hvyo mkuu mim Kuna mwenzangu nmemshauri hivyo akaniambia yeye mtoto wake anampeleka EMS Primary School alaf O Level anampeleka Shule za Kata
 
wanakutana wapi, wakati kila mtu anaenda shule yake? wenye A utawakuta Benjamin wakat wenye C utawakuta kerezange secondary
Hawa EMS mwisho wa siku inabidi tu wauze viwanja vya urithi maana wanaona aibu kurudi Kayumba. Ni kweli huwa hawakutani.
 
Wewe pia ni mwathrika wa hizi misconception.

Wachina, wafaransa, Warusi, hawajui hicho kinachoitwa Kingereza na utashangaa wanavyotoboa duniani.

Kingereza ni Lugha tu haipaswi kukucost mstakabali wako wa maisha mengine.
Wafaransa,wachina etl siyo levels zetu ,wao wanaindustries na commodities za kunadi lugha zao na bidhaa zao,( complimentary,joint demand,composite demand)iwe isiwe lazima uhitaji commodity ya huyo mchina,mfaransa nk,automatically ili uwe efficient lazima ujifunze lugha yake,kinyume na sisi watz,tuna export commodity ipi ya kuiattach na kiswahili ili kusudi hao wachina,wafaransa nk waone umuhimu wa kukipenda kiswahili,kimsingi mtoto ukimnyima lugha ya Dunia,umemtengenezea ukuta,wa kuzunguka hapa hapa nchini
 
Likud umekuwa ukiandika sana kuhusu hili. Uzi wako wa kwanza kabisa kuhusu swala hili nilimuwa miongoni mwa wasomaji wa mwanzo kabisa.
Pia katika muendelezo nimekuwa nakufuatilia, binafsi ninakuelewa vizuri sana ingawa kila unapojaribu kuli address unakuwa too general na hivyo kuimba na kucheza nje ya beat, na mimi nabaki kusoma comments vile mnashikana mashati na kupigana ngwala na wachangiaji.

Tatizo Una address ukiwa na machungu baada ya kuumzwa huko EMS, unasahau hata huko Kayumba kuna watu wamemizwa pia, hivyo ukitumia hisia na experience yako wakati wenzako pia wana za kwao, usitaraji kuwepo na muafaka.
Hii nayo pointi...mimi sipingi watu kupeleka watoto wao huko. Ila nashauri watu wasijiforce kama hawana uwezo.

Nina Marafiki wengi wameliwa pesa, wana mkopo balaa.
At the end anachoambulia mtoto ni kingereza kizuri tu nothing else.

Watoto wa vigogo wanafanikiwa sio kwa sababu wamesoma EMS bali wao hawa wasipoenda huko tayari wana Garantee ya Maisha mazuri.

Mfano Mo Dewj amesoma Tanganyuka IS na Marekani.

Yeye hata bila kupita huko tayari ana mafanikio ya ukoo.
 
Wafaransa,wachina etl siyo levels zetu ,wao wanaindustries na commodities za kunadi lugha zao na bidhaa zao,( complimentary,joint demand,composite demand)iwe isiwe lazima uhitaji commodity ya huyo mchina,mfaransa nk,automatically ili uwe efficient lazima ujifunze lugha yake,kinyume na sisi watz,tuna export commodity ipi ya kuiattach na kiswahili ili kusudi hao wachina,wafaransa nk waone umuhimu wa kukipenda kiswahili,kimsingi mtoto ukimnyima lugha ya Dunia,umemtengenezea ukuta,wa kuzunguka hapa hapa nchini
Mkuu uliza watu wanaoenda ulaya na kupata international opportunities sio kwa sababu ya Kingereza chao.
Unajichanganya.
Prof Ussoro ulimsikia Kingereza Chake?
 
Ni braza moja kati ya wasomi wa kitaani kwetu. He was born in 1980. He is 5 years older than me. Darasani alikuwa very smart. Ni wale the cream wa Azania wa Enzi hizo.

To cut story short. Jamaa alikuwa mtumwa mwaminifu wa Shule za Ems. Amepunwa ile kinoma Noma. Kwanza Watoto wawili wa kwanza . Hawa aliendelea kupunwa hadi seco kawapeleka shule wanalipa ada tu milioni 6. Dogo wa kiume kamaliza form four kagoma kwenda Advance kasema anataka kwenda college. Kozi Aliyo ichagua sasa " PROCUREMENT ". Ule utoto aliokuwa anamwambia baba ake alipokuwa primary " Daddy I want to be a pilot, lawyer, Doctor or Engineer blah blah blah" ukawa ume evaporate.

Jamaa alikuwa so much dis appointed . Nakumbuka wakati wa Corona aliwahi niuzia kiwanja kwa bei ya Chanika halafu hela yote akaenda kulipa ada shuleni. Sehemu yenyewe aliyoniuzia kiwanja ni very potential area. Japo kiwanja sio chake ni cha urithi but aliniuzia kwa bei ya chini.

Mwaka mmoja baadae akataka nimtafutie mteja amuuzie kiwanja chake kingine alipe ada za watoto.

Nikamkalisha chini nikampa somo kuhusu shule za Kayumba. Nikamwambia warudishe wanao Kayumba. Watoto watatu sio poa. Mapacha wawili wa kike plus mdogo wa mwisho, kwa kipato chako sio kweli bro. Hata hivyo hakuna umuhimu wowote wa wewe kulipa hela yote hiyo kwa ajili ya Elimu ya msingi ya mtoto.

Toa watoto wako Em walete Kayumba. Mbona Mimi nimewatoa na wako poa tu.

Jamaa akawa inspired na ushauri wangu. Akawatoa watoto wake wote watatu Ems akawaleta Kayumba. Hao mapacha wawili ndio wamefaulu wamepata A zote na mdogo wao anafanya vizuri sana shuleni.

Jamaa kuandika gazeti refu sana ananishukuru mdogo wake kwa ushauri ambao pia umemsaidia kusave pesa na kuinvest kwenye mambo mengine.

Comments za wadau sasa. Kuna comments za watu kama sita ambao nao pia waliwatoa watoto wao Ems wakawaleta Kayumba. Wadau hao wanasema walikuwa inspired na Mimi. Baada ya kuona hadi Mimi nimewarudisha watoto wangu Kayumba. ( Aina ya maisha ninayo ishi na vitu ninavyo vimiliki ambavyo watu wa mtaani kwetu wanavijua, wanaona watoto wangu hawastahili kusoma Kayumba. Mimi kuwapeleka watoto wangu Kayumba ni jambo linalo tengeneza sentensi " kama Likud kawatoa watoto wake Kayumba Mimi nani)

Wengi walio watoa watoto wao Ems na kuwaleta Kayumba wanashukuru sana na wanajilaumu kwanini hawakufanya hivyo mapema.

Hata wewe mzazi unae jistress kulipia mamilioni kwenye shule za Ems wacha mara moja. Haraka sana kimbia kawatoe watoto wako EMS walete Kayumba. Huna sababu yoyote ile ya kujistress kulipa mamilioni huko EMs . N real sense,Shule za Ems hazina umuhimu wala UPEKEE wa aina yoyote ile. Umuhimu na upekee huo umetengenezwa na Wamiliki wa shule za Ems ili waendelee kukupuna.

Mtu muhimu kuliko wote kwenye shule hizo ni wewe mzazi kwa sababu wewe ndo unaelipa ada na ndio sababu kuu kwanini mmimiki kaanzisha shule hiyo.

Kilaza atasema " Likud huna hela "

Situmii hela hovyo kwa sababu ninazo.

Enyi wazazi ambao watoto wenu wamefanya vizuri kwenye shule za Kayumba enyi wazazi ambao mliwatoa watoto wenu Ems na kuwaleta Kayumba na wamefanya vizuri,acheni ubinafsi. Hakikisheni mnashare hizo information kwa watu wengi iwezekanavyo ili kuwatoa usingizini wazazi ambao bado wamelala. Wazazi ambao wana jistress kulipa mamilioni kwenye shule za Ems
kila mtu alipe kwa uwezo wake ada ambayo anahisi ataweza kulipa.
 
Ni kupoteza pesa tu, wanaosoma kwenye hizo shule hawana ubunifu wowote, ni sawa na kuku broiler vs kuku wa kienyeji.

Kama pesa ipo, peleka mtoto kayumba mpaka kidato cha nne, baada ya hapo kamlipie kozi ya urubani na nyinginezo unazoona zinafaa; lakini kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kujifunza a for apple ni kupoteza pesa.​
Kama unashindwa kumlipia 2.5M kwa mwaka utaweza 15M ya urubani Tena ule wa private pilot?
Commercial pilot siyo chini ya 100M.
Unajua kiingereza muhimu kwenye masomo na kazi za urubani?
Acheni kuongopeana.
 
Mimi mwenzenu wa kwangu niliona ni ana akili ya wastani toka msingi. Nimeona aendelee kusoma kayumba na sekondari atasoma kayumba. Pia nimemwandikisha dojo anacheza michezo boxing na karate
Akimaliza f4 aende jeshini anaingia na fani ya ngumi.
 
Kama unashindwa kumlipia 2.5M kwa mwaka utaweza 15M ya urubani Tena ule wa private pilot?
Commercial pilot siyo chini ya 100M.
Unajua kiingereza muhimu kwenye masomo na kazi za urubani?
Acheni kuongopeana.
Hizi elimu za ada kubwa ni biashara tu, unavyolipa ada kubwa ndivyo mishahara ya walimu wao inazidi kunona, mwisho wa siku wanafanya mtihani wa taifa mmoja, wanaenda kukutana pale udom n.k​
 
Ni kupoteza pesa tu, wanaosoma kwenye hizo shule hawana ubunifu wowote, ni sawa na kuku broiler vs kuku wa kienyeji.

Kama pesa ipo, peleka mtoto kayumba mpaka kidato cha nne, baada ya hapo kamlipie kozi ya urubani na nyinginezo unazoona zinafaa; lakini kutumia gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kujifunza a for apple ni kupoteza pesa.​
ukizingatia walimu wengi wanaofundisha EMS asilimia kubwa ni felia hawaajiriki hata serikalini,halafu kiingereza siyo elimu ni lugha tu
 
Hii nayo pointi...mimi sipingi watu kupeleka watoto wao huko. Ila nashauri watu wasijiforce kama hawana uwezo.

Nina Marafiki wengi wameliwa pesa, wana mkopo balaa.
At the end anachoambulia mtoto ni kingereza kizuri tu nothing else.

Watoto wa vigogo wanafanikiwa sio kwa sababu wamesoma EMS bali wao hawa wasipoenda huko tayari wana Garantee ya Maisha mazuri.

Mfano Mo Dewj amesoma Tanganyuka IS na Marekani.

Yeye hata bila kupita huko tayari ana mafanikio ya ukoo.
100% Fact.
 
Back
Top Bottom