Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

Asante,Mimi niliandika Uzi wa kuomba msaada jinsi ya kumtoa mtoto wangu toka shule binafsi ya sekondari kurudi ya serikali,wadau wakanijibu haiwezekani.
Mtoto yupo kidato cha kwanza
 
Kwangu mm na Jinsi navyoona Kayumba ni shule nzuri ila kuanzia Form 1 na kuendelea ni vyema ukampeleka english medium kuanzia darasa la kwanz mpka la Saba then baada ya hapo tafuta shule moja ya Serikali ya Bweni yenye manzingira Mazuri mtoto asome ila ukiangalia kwa namna moja zile shule za private zimekaaaa kiupigaji ila Kidogo English medium itamtengeneza mtoto kwenye namna Fulani Bora uwezo wake wa kuongea Kingereza na kujieleza mbeleni Coz watoto wengi Tunaosoma kayumba kuanzia msingi mpk chuo tunakosa hicho kitu lakni japokuwa uwezo wa mtoto kujielezea na kuongea kingereza utategemea na yy mwenyew ila English medium zinampa mtoto msingi Mzuri
 
ttwende taratibu likud. unasema uliwarudisha,nauliza uliwarudisha st kayumba wakitokea ems darasa la ngap? tuanzie hapo
 
Naishi na jamaa mmoja hapa ni graduate, alisoma kayumba,kaingia serikalini ,vizuri kafaulu vizuri Hadi amemaliza chuo kikuu, Yuko mtaani,Sasa akajiongeza kidogo ,akapata mtaji kidogo akafungua kampuni,katika harakati za kukuza mtaji wake,aliomba kuandikiwa project proposal/ business plan,akaomba fedha kwa investor mmoja uingereza $300,000/- investor akamkubalia lakini akamwambia kwanza wafanye zoom meeting ya mtandaoni,jamaa ni graduate lakini English speaking Yuko poor Sana ,akaanza kuhangaika kuazima mtu aseme kwa niaba ya mradi wake,shida ikaja aliyemwazima,haiwezi kuyachanganua kwa hoja Yale mahesabu yaliyo andikwa humo, kwenye proposal,ikabidi akaazime mtaalamu mwingine tu ,tena akaomba aipitie ile document kwanza,na wote Hawa aliwalipa pesa,Sasa unaweza kuona hasara ya kujifungia kayumba,inakuwa unafunga na fursa zingine za nje,hapo ndipo msemo wa Nyerere ulipo dhihirika "IF YOU THINK EDUCATION IS EXPENSIVE TRY IGNORANCE " ndugu level moja wapo ni muhimu kuibalance iwe private either primary au sekondari elewa "always cheap is bitter and bitter is cheap"
 
Embu Mkuu Elezea vizuri kwanza
 
Angalia matokeo ya Darasa la saba fanya comparative analysis na shule za KAYUMBA.
wanaiba mitihani au kuonyeshwa majibu... kuna mdogo angu alisoma shule hizo alisema drs la 7 walionyeshwa majibu....shule moja maarufu huko himo klm...
 
😂😂😂😂😂😂😂
 
Wewe pia ni mwathrika wa hizi misconception.

Wachina, wafaransa, Warusi, hawajui hicho kinachoitwa Kingereza na utashangaa wanavyotoboa duniani.

Kingereza ni Lugha tu haipaswi kukucost mstakabali wako wa maisha mengine.
Wachina Wangapi Compared na Population yao ? Umewahi kufika China ukaona au ukafahamu the magnitude ya wao kutumia Kiingereza?

Wafaransa Wangapi Compared na Population yao ? Umewahi kufika France ukaona au ukafahamu the magnitude ya wao kutumia Kiingereza?

Changamoto ya mijadala mingi humu ipo more of a feelings na sio Facts

Wa china Competitors wao wa kwanza ni USA, sasa wewe unakuja unasema hawajui kiingereza na hawana mpango nacho are you serious?
 
Unatumia nguvu nyingi mkuu, pointi ni uwezo... kama huna uwezo automatically wataenda kayumba kama unao wape kile unaona vijana wako wanastahili, case closed!
 
Labda Kama mtu hana uwezo wa kulipa ada za private schools.
Kingereza cha wanafunzi wengi waliosoma shule za serikali huwa sio kizuri.

Kingereza ni lugha ya dunia na kinafungua milango ya fursa nyingi (hasa za ughaibuni).

Au nimeandika uongo wakuu.
Upo sahihi, wakwangu nilimrudisha kanumba off course amepata A tano lakini kwenye English ametepeta amepata B, infact ame lose kidogo!, naimani atakapoanza form one, ata recover tu.
 
wanaiba mitihani au kuonyeshwa majibu... kuna mdogo angu alisoma shule hizo alisema drs la 7 walionyeshwa majibu....shule moja maarufu huko himo klm...
Wanaiba mitihani nchi nzima maana yake
 
Tupate mitaala inayosaidia watoto wetu na kayumba isonge mbele,
Heri mwanangu akaazq carpentry from primary to secondary akitoka apo ni lulu sokoni kuliko miaka 11 na hakuna fani anayoijua mwisho anakuja kuhaha mtaani
 
Msichanganye mambo kuna ems na inernational schools like DiS ukiweka mwano maeneo hayo hutajuta anasoma huku anaendelezwa kipaji chake.na slyabus ya cambrigde. We unapeleka mtoto shule ya kata ems ni kata iliyochangamka in the name of kingereza.peleka watoto dis hutajuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…