Badala ya kushughulika na elimu inavyoharibiwa shule binafsi, unashughulika na nyimbo za Zuchu ili nawe uonekane unafanya kazi!

Badala ya kushughulika na elimu inavyoharibiwa shule binafsi, unashughulika na nyimbo za Zuchu ili nawe uonekane unafanya kazi!

Mkungunero

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2023
Posts
401
Reaction score
569
Ukienda private schools kuna manyanyaso mengi sana mpaka unajiuliza hivi wizara husika IPO kweli au hawajui wafanye nini!

1. Mishahara ya baadhi ya shule kwa graduates haizidi laki mbili kwa mwezi wakati serikali imeahaweka kima cha chini na cha juu na graduates anapaswa kuanzia laki saba.

2. Private schools 90% huwa hawatoi mikataba ambapo unyanyasaji wa kufukuzwa ni mkubwa. Mwajiri anaweza kukuota vibaya usiku kesho asubuhi akakufuza bila sababu yoyote.

3. Privates schools nyingi mpaka simu wanakunyanganya inawekwa kwa mlinzi utaiona wakati wa kwenda nyumbani. This is totally enslavement. Mfano ni shule ya Nyahili pale Arusha Morombo eneo la Intel kwa chini hivi na tena inamilikiwa na mbunge aliyechikuwa Jimbo la Tarime Mjini.

4. Kutukanwa matusi ya nguoni ni mwajiri ni kitu cha kawaida sana.

5. Hakuna likizo kwa wafanya kazi walimu nk.

6. Kazini unaingia sa kumi na moja alfajiri unatoka saa mbili usiku. This is ridiculous kabisa. Halafu mshahara laki mbili.

Mpaka unajiuliza serikali hii inafanya kazi gani! Human welfare iko wapi ambayo ndio moja ya kazi za serikali kulinda maslahi ya umma?

Ukienda Kenya huwezi tofautisha mfanyakazi wa private schools na public schools. Wote wanakuwa treated sawa kabisa, wala mwajiri private hawezi kujisikia tu kumfukuza mwalimu, ni process kubwa mno.

Mkenda nilikuwa nakuona wewe ni Professor kumbe galasa tu.
 
Elimu yetu ina matatizo mengi sana kuliko kushughulika na muziki tena wa siku moja watu wakiwa kwenye shughuli nje ya masuala ya taaluma.
 
Law of Demand and supply ndio inapanga mashahara.

Demand and supply kati ya fursa za ajira zilizopo sehemu X na idadi ya wanaotafuta ajira sehemu X ndio zinaamua mshahara uwe shilingi ngapi.
 
Law of Demand and supply ndio inapanga mashahara.

Demand and supply kati ya fursa za ajira zilizopo sehemu X na idadi ya wanaotafuta ajira sehemu X ndio zinaamua mshahara uwe shilingi ngapi
Nini kazi ya serikali. Serikali kazi yake ni kulinda maslahi ya uma. Ndo mana Kuna price ceiling and price floor. Kama hujui nyamanza. Kenya is strong in allocating resources. Tanzania tunajiendea endea tu kama hamana serikali vie.
 
Mkenda tunamlaumu bure tu. Tatizo letu Tz mpaka leo hatujapata watu wenye weledi, commitment na vission ya kufanya mapinduzi kwenye mfumo wote wa elimu. Mfumo wetu wa elimu ni hovyo. Mfumo wa kufaulu wa mitihani badala ya kusimika weledi kichwani ili kutawala mazingira kikamilifu. Tunachoona ni siasa tuna uhuni mwingi wa kuhadaa umma.
 
Ukienda private schools kuna manyanyaso mengi sana mpaka unajiuliza hivi wizara husika IPO kweli au hawajui wafanye nini!

1. Mishahara ya baadhi ya shule kwa graduates haizidi laki mbili kwa mwezi wakati serikali imeahaweka kima cha chini na cha juu na graduates anapaswa kuanzia laki saba.

2. Private schools 90% huwa hawatoi mikataba ambapo unyanyasaji wa kufukuzwa ni mkubwa. Mwajiri anaweza kukuota vibaya usiku kesho asubuhi akakufuza bila sababu yoyote.

3. Privates schools nyingi mpaka simu wanakunyanganya inawekwa kwa mlinzi utaiona wakati wa kwenda nyumbani. This is totally enslavement. Mfano ni shule ya Nyahili pale Arusha Morombo eneo la Intel kwa chini hivi.

4. Kutukanwa matusi ya nguoni ni mwajiri ni kitu cha kawaida sana.

5. Hakuna likizo kwa wafanya kazi walimu nk.

6. Kazini unaingia sa kumi na moja afajiri unatoaka saa mbili usiku. This is ridiculous kabisa. Halafu mshahara laki mbili.

Mpaka unajiuliza serikali hii inafanya kazi gani! Human welfare iko wapi ambayo ndio moja ya kazi za serikali kulinda maslahi ya umma?

Ukienda Kenya huwezi tofautisha mfanyakazi wa private schools na public schools. Wote wanakuwa treated sawa kabisa, wala mwajiri private hawezi kujisikia tu kumfukuza mwalimu, ni process kubwa mno. Mkenda nilikuwa nakuona wewe ni Professor kumbe galasa tu.
Haya uliyoandika ni sahihi na ukweli ni kwamba nchi inayotegemea private schools kwa excellency ya elimu yake, ujue hiyo ni hovyo tu!

Pamoja na hayo huwezi kusema hakuna maana ya kupambana na upuuzi wa miziki ya hovyo mashuleni. Hiyo ndo inalawiti elimu yetu na ni kuonesha ubovu wa waalimu tulionao na wanasiasa tulionao. Kwa nini mwanasiasa akaribishwe shuleni kucheza na watoto wadogo mziki wa kiseng kama huo. Kwani hajui miziki ya watoto?

Halafu angalia upuuzi wa spika pia. Naye kwa nafasi yake anajipanga kupambana na waziri bungeni eti kwa sababu hata wao na yeye huwa wanacheza. Ina maana upuuzi wao ndo standard ya wa-TZ?
 
Law of Demand and supply ndio inapanga mashahara.

Demand and supply kati ya fursa za ajira zilizopo sehemu X na idadi ya wanaotafuta ajira sehemu X ndio zinaamua mshahara uwe shilingi ngapi
Kuna mambo hutakiwi kuachia market forces za demand and supply ziyaamue. Some vulnerable groups must be protected by law and policy.
 
Law of Demand and supply ndio inapanga mashahara.

Demand and supply kati ya fursa za ajira zilizopo sehemu X na idadi ya wanaotafuta ajira sehemu X ndio zinaamua mshahara uwe shilingi ngapi
Hapa umetumia ulichofundishwa darasani na hutaki kujiongeza kujua uhalisia wa Dunia. Jitahidi kutumia akili.
 
Laki mbili private au kujitolea bure serikalini. Maana hata serikali ina wafanyakazi vibarua wa kujitolea karibia na bure
 
Laki mbili private au kujitolea bure serikalini. Maana hata serikali ina wafanyakazi vibarua wa kujitolea karibia na bure
Nchi hii ni shida sana. Mkiambiwa ccm ni janga muwe mnaelewa. A graduate being paid laki mbili si lazima afe kwa stress tu
 
Nchi hii ni shida sana. Mkiambiwa ccm ni janga muwe mnaelewa. A graduate being paid laki mbili si lazima afe kwa stress tu
Cha kushangaza ni graduate kukaa muda mrefu bila ajira au kiingiza kipato. Akipata 200,000 kwa mwezi ni hatua kuelekea mafanikio.

Wasio na ajira wako wengi,anayepata 200,000 ana uafadhali
 
Nini kazi ya serikali. Serikali kazi yake ni kulinda maslahi ya uma. Ndo mana Kuna price ceiling and price floor. Kama hujui nyamanza. Kenya is strong in allocating resources. Tanzania tunajiendea endea tu kama hamana serikali vie

Serikali inatumikisha watu bureee kwa kujitolea.

Kuna walimu kibao serikalini wanajitolea miaka zaidi ya mitano hawalipwi hata hiyo laki mbili
 
Back
Top Bottom