Badala ya kutapanya mali kwa wageni kwanini Rais asijikite kwenye kuwajengea wananchi wake uwezo?

Badala ya kutapanya mali kwa wageni kwanini Rais asijikite kwenye kuwajengea wananchi wake uwezo?

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Kila safari atayofanya Rais , lazima itaambatana na kisainiwa kwa mikataba ya kiuwekezaji kwenye Rasilimali zetu.

Dunia ya sasa idadi ya watu inaongezeka na hii inafanya rasilimali kuwa adimu.

Kwa kulitambua hili mataifa makubwa yamekuwa na sera kandamizi na kutumia mbinu za kila aina kuhakikisha kwamba mataifa yao hayapungukiwi na rasilimali muhimu.

Hapa Tanzania kasi ya ongezeko la watu bado ipo juu. Ingawa tunaona kwamba tuna rasilimali nyingi ila ukweli ni kwamba Rasilimali hizo ni chache, na itafika kipindi hazitakidhi mahitaji ya idadi ya watu itayokuwepo.

Kwa kuangalia hatari hiyo serikali inapaswa kuwekeza nguvu kwenye kuwajengea uwezo wananchi wake ili kuhakikisha kwamba wananufaika kwa asilimia kubwa rasilimali zilizopo nchini.

Hii ya kuacha milango na madirisha wazi ni kama kufanya suicide ambayo wakati ukifika hakutakuwa tena na kizuizi kwa hasira watakazokuwa nazo wananchi kwa wakati huo.
 
Nakubaliana na kauli yako. Kila safari ya Rais inapaswa kutumika kama fursa ya kuhakikisha kuwa nchi yetu inanufaika vyema na rasilimali zake. Hii ni kwa sababu idadi ya watu duniani inaongezeka kwa kasi, na jambo hili linaifanya rasilimali kuwa adimu zaidi.

Mataifa makubwa yanatambua hali hii na yameanzisha sera kandamizi na kutumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha kuwa yanaendelea kudhibiti rasilimali muhimu.

Tanzania haipaswi kubaki nyuma katika juhudi hizi. Ingawa tuna rasilimali nyingi, idadi ya watu inakua kwa kasi na rasilimali hizi hatimaye hazitatosheleza mahitaji ya watu wote.

Serikali inapaswa kuwekeza nguvu katika kuwawezesha wananchi wake ili waweze kunufaika kikamilifu na rasilimali zilizopo nchini. Hii itahakikisha kuwa wananchi wanaishi maisha bora na kupunguza hatari ya migogoro ya rasilimali katika siku zijazo.

Kuacha milango na madirisha wazi, kama unavyosema, ni sawa na kujiua. Tukiruhusu rasilimali zetu zipotee mikononi mwa wengine bila kudhibiti, tutaishia kukabiliwa na hasira ya wananchi ambao watakuwa wametengwa na fursa za maendeleo.

Ni wakati sasa wa kuchukua hatua madhubuti kulinda rasilimali zetu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Serikali, sekta binafsi, na wananchi wote kwa ujumla wanapaswa kushirikiana katika juhudi hizi muhimu.

Pamoja, tunaweza kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika vyema na utajiri wake wa asili na kujenga mustakabali bora kwa watu wote.
 
Kila safari atayofanya Rais , lazima itaambatana na kisainiwa kwa mikataba ya kiuwekezaji kwenye Rasilimali zetu.

Dunia ya sasa idadi ya watu inaongezeka na hii inafanya rasilimali kuwa adimu.

Kwa kulitambua hili mataifa makubwa yamekuwa na sera kandamizi na kutumia mbinu za kila aina kuhakikisha kwamba mataifa yao hayapungukiwi na rasilimali muhimu.

Hapa Tanzania kasi ya ongezeko la watu bado ipo juu. Ingawa tunaona kwamba tuna rasilimali nyingi ila ukweli ni kwamba Rasilimali hizo ni chache, na itafika kipindi hazitakidhi mahitaji ya idadi ya watu itayokuwepo.

Kwa kuangalia hatari hiyo serikali inapaswa kuwekeza nguvu kwenye kuwajengea uwezo wananchi wake ili kuhakikisha kwamba wananufaika kwa asilimia kubwa rasilimali zilizopo nchini.
Hii ya kuacha milango na madirisha wazi ni kama kufanya suicide ambayo wakati ukifika hakutakuwa tena na kizuizi kwa hasira watakazokuwa nazo wananchi kwa wakati huo.
Huyu mama uyu Mungu anmwonya sana ,mda mwalimu mkuu
 
Back
Top Bottom