Badili sentensi hii kuwa ya Kiingereza

Badili sentensi hii kuwa ya Kiingereza

Ndio nilichosema utatafsiri moja kwa moja kulingana na kinachotakiwa kusemwa mfano, We will ensure reliable water supply all over
Au we have a serious campaign to supply clean water countrywide

Yani sentensi itategema na context iliyopo wakati huo lakini kinachotakiwa kueleweka na huyo wa kiingereza ni kwamba tuna mkakati wa kutatua changamoto ya upatakanaji maji
Asante
 
Utakapotaka tafsiri ya kijapani unistue?

Kwanini kila kitu kiwe kiingereza tu?
Kiingereza ndio Kiswahili cha dunia mkuu,Ni rahisi zaidi kukutana na mtu anayezungumza kiingereza kuliko kijapan
 
Ina maana wazungu hawajawahi beba maji kichwani? Hii kusema hawajawahi kuwa na shida ya maji napinga, wote tumepitia hatua hizi ila wao wametutangulia hatua kadhaa ndio maana mpaka leo tuko huku na ndoo za kichwani wakati hayo wameshayaacha toka karne ya 17/18 huko.

Mwalimu hapo sijaelewa, nifafanulie vizuri, TEACHER KONDE.
Waliwahi ndio maana nikasema kwa muda mrefu hawana hilo tatizo.
Halafu hata kama walikuwa nalo au wanalo sio lazima waendeshe campaign kama yetu kutatua hivyo utamaduni utatofautiana hapo
 
Hii imekaa vizuri,ila itabidi kumueleza zaidi ili ajue mantiki
Hicho ndio hakitakiwi sasa, ulitakiwa kwenda kwenye mantiki moja kwa moja ila unaweza mwisho wa hiyo mantiki ukarudia huo msemo wa kiswahili

Mfano The government is ensuring reliable water supply countrywide through a campaign "mtue mama ndoo kichwani"
 
Wakuu,
Hivi sentensi hii kwa kiingereza tunaweza kuisemaje?

"Kumtua mama ndoo kichwani"

Yaani kama vile unamwambia mgeni kwamba nchini kwetu tunataka kumtua mama ndoo kichwani.[emoji3]

Ahsante
Huu ni msemo na hivyo ulitakiwa uulize kuhusiana na "synonym" yake kwa kiingereza, yaani msemo wa kiingereza ambao unamaanisha sawa na msemo huu. Direct translation ya msemo huu kwa kiingereza inaaweza isilete mantiki sana kwa sababu msemo huu waingereza wao hawana
 
Huu ni msemo na hivyo ulitakiwa uulize kuhusiana na "synonym" yake kwa kiingereza, yaani msemo wa kiingereza ambao unamaanisha sawa na msemo huu. Direct translation ya msemo huu kwa kiingereza inaaweza isilete mantiki sana kwa sababu msemo huu waingereza wao hawana
Sawa hebu taja hio synonym inayoendana maana lengo ni kutafsiri ili unayewasiliana nae aelewe
 
Sawa hebu taja hio synonym inayoendana maana lengo ni kutafsiri ili unayewasiliana nae aelewe
You can simply google. Muda huo sina. Kwa kipindi hiki kuuliza watu msawali haya madogo madogo ni uzembe; na hata makubwa makubwa pia kwa sababu google is everything!
 
Ukikutana na Mzungu mtwishe Ndoo tu,Tembea nae mita 100 aonje ladha yake mtue....Muulize umejisikiaje?
 
Back
Top Bottom