Badili sentensi hii kuwa ya Kiingereza

"Supply tap water to homes". Lugha haitafsiri neno kwa neno. Lugha inatafsiriwa kwa maana ya sentensi au hata aya.
Sawa,lakini tafsiri uliyoisema bado iko 'too general' maana haioneshi kwamba anayeletewa ahueni ni mwanamke.
 
Umejibu vizuri sana na kiuhalisia. Nahau inaelezea kitu kilichopo kwenye jamii. Kwa mfano huwezi kuuliza 'matobolwa' ya Mnyamwezi, au 'mbege' ya Mchaga, au 'msuli' wanaovaa Waislamu kwa Kiingereza ni nini? Waswahili tunasema 'mkunje samaki akiwa mbichi'. Mswahili akisikia hivyo ataelewa unamaanisha nini kwa kuwa utamaduni wa kukunja samaki tunao. Muingereza atasema 'gather hay while the sun is still shining'. Msukuma au Mmasai atashangaa unamaanisha nini kwa kuwa kila baada ya saa 12 jua linatokeza, na ng'ombe wake huwapeleka mbugani kuchunga.
Kwa ufupi, vitu vinavyotafsirika ni vile tu ambavyo viko katika jamii zote mbili ambazo unataka kuvitafsiri.
 
Kwani mwanamke wa UK hana ahueni? Lugha ya Kiingereza ni ya Waingereza. Mwanamke mwingereza ana shida ya maji pia? Anabeba maji kichwani pia? Ukiweka maji kwenye nyumba, ndio umemtua mama ndoo hivyo. Ukisema habari za ndoo, maji na kichwa kwa Waingereza ambao hawabebi maji kichwani, hautaeleweka.

Ni sawa na kuomba maana ya mtori ktk Kiingereza kwa neno moja tu. Hakuna mtori Uingereza, kwa hiyo hakuna neno la Kiingereza moja linalomaanisha mtori. Lazima utumie aya nzima kumwelesha Mwingereza mtori ni nini. Km hauelewi hili basi, shinda mechi zako mwenyewe sasa.
Sawa,lakini tafsiri uliyoisema bado iko 'too general' maana haioneshi kwamba anayeletewa ahueni ni mwanamke.
 
Farolito - Kama hii ni ngumu kwako kuelewa, basi baki hivyo hivyo.
 
Wakuu,
Hivi sentensi hii kwa kiingereza tunaweza kuisemaje?

"Kumtua mama ndoo kichwani"

Yaani kama vile unamwambia mgeni kwamba nchini kwetu tunataka kumtua mama ndoo kichwani.[emoji3]

Ahsante
Relieve the burden of women carrying buckets of water through reliable water supply.
 
Mkuu nimekuelewa ila nilichokurekebisha wewe ni kwamba maelezo yako yalikuwa hayagusi moja kwa moja kiini cha ujumbe,

Asante kwa mchango pia
 
Okay, hizi nadhani ndio tafsiri bora zaidi ya hiyo sentensi

"to relieve mother's head the bucket burden"

ama pia,

"to relieve the bucket burden from mother's head"

Sasa kama kuna tafsiri nzuri zaidi ya hii sijui,

Maana imetaja kila kitu, kutua=relieve, mama=mother, kichwa=head, ndoo=bucket
 
Kama ni motto, it makes more sense if you say " to relieve a mother's bucket-to-head water problem"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…