Bado 18% Ujenzi wa Bwawa la Nyerere kukamilika

Bado 18% Ujenzi wa Bwawa la Nyerere kukamilika

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Desemba 22,2022 Mhe. Rais Samia Suluhu alizindua zoezi la kuanza ujazwaji maji kweny Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere. Hadi sasa mradi umebakiza asilimia 18 kukamilika huku ujazo wa maji ukiwa ni zaidi ya mita 133 kutoka usawa wa bahari.

Ujazo wa Bwawa la Nyerere lina ujazo wa lita za maji bilioni 33 ambazo ni mara kumi ya ujazo wa Bwawa la Mtera lenye ujazo wa bilioni 3. Sambamba na hilo tayari mtambo unaojulikana kama Runner umewasili. Mtambo huu una uzito wa tani 79 ambayo mingine 8 iko njiani inakuja.

FpegjGMXoAA6WfO
 
Bongo kitu kikishapanda bei hua hakishuki ,hiyo ndio kanuni nchi ya ajabu sana aisel

Hapa bongo sijui kama meme utakujaga kushuka bei
Hautashuka bei, ila kipato cha mtu mmoja mmoja kitaongezeka - hivyo kumudu kununua umeme kwa bei hiyo itakayopangwa. Hapo tukilinganisha na kipato cha sasa, utaona umeme bei poa.
 
Hapa napo tutegemee Marehemu kusimangwa kila ikitokea dosari kwenye uzalishaji wa umeme kwenye hili bwawa!
 
Wakina rope na mabepari walisema itachukua miaka 3 hadi 4 bwawa hilo kujaa maji na linaweza liweze kujaa milele kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi. Wangeanza kulijaza mwezi Septemba masika ilipoanza, saa hizi lingalikuwa limejaa top.
 
September Vuli ilipoanza
 
Desemba 22,2022 Mhe. Rais Samia Suluhu alizindua zoezi la kuanza ujazwaji maji kweny Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere. Hadi sasa mradi umebakiza asilimia 18 kukamilika huku ujazo wa maji ukiwa ni zaidi ya mita 133 kutoka usawa wa bahari.

Ujazo wa Bwawa la Nyerere lina ujazo wa lita za maji bilioni 33 ambazo ni mara kumi ya ujazo wa Bwawa la Mtera lenye ujazo wa bilioni 3. Sambamba na hilo tayari mtambo unaojulikana kama Runner umewasili. Mtambo huu una uzito wa tani 79 ambayo mingine 8 iko njiani inakuja.

View attachment 2525319
FpegjGMXoAA6WfO
Habari yako si ya kitaalam sana, na una copy na kupaste bila kujua technical details zilizopo.
Bwawa lina kina cha 131m, sasa hiyo 133m juu ya usawa wa bahari ndiyo kitu gani?
Kutakuwepo turbines 9 za kuzalisha umeme, kila moja ikizalisha 235MW, jumla 2115MW.
Sasa hicho kifaa "runner" ndio nini?
 
Upatikanaji wa umeme usiokatika ni kitu muhimu sana kwa afya ya akili ya binadamu waliostaarabika na kwa maendeleo ya kiuchumi.

Bei iwe ndogo au kubwa kama kawaida yao Hilo sio muhimu umeme kwanza Bei tutajuana mbele kwa mbele.

Tunakuomba ewe Mh Marope malizia mradi haraka tufungue salon zetu na kuchomelea Huku kitaa maana Maisha yenyewe mafupi na yamebana sana wenzako huku kitaa hatuna mshahara kama nyie huko
 
Hautashuka bei, ila kipato cha mtu mmoja mmoja kitaongezeka - hivyo kumudu kununua umeme kwa bei hiyo itakayopangwa. Hapo tukilinganisha na kipato cha sasa, utaona umeme bei poa.
Kipato kitpandishwa na Nini ?
 
Hivi umeme wa gass uliishia wapi, tusubili tuone huo umeme maana maneno yasiwe mengi tutalaumiana sana na kusifiana hovyo ila kila mtu anakua sahihi Mfano nikikumbushia gass ntalaumiwa maana tuliaminishwa kama haya haya ya bwawa mwisho wa siku hovyo na sasa bwawa tuacheni maneno tusubilini tuone, ila nachojua mimi uendeshaji wa mitambo mikubwa kama hii ni gharama kubwa hivyo tutegemee gharama za umeme kua kubwa, watu wasitegemee kabisa umeme kua rahisi utakua wa uhakika ila utakua ghali na kwahali ya uchumi wa nchi hii watu watapiga kelele sana.
 
Back
Top Bottom