Bado 18% Ujenzi wa Bwawa la Nyerere kukamilika

Bado 18% Ujenzi wa Bwawa la Nyerere kukamilika

Hautashuka bei, ila kipato cha mtu mmoja mmoja kitaongezeka - hivyo kumudu kununua umeme kwa bei hiyo itakayopangwa. Hapo tukilinganisha na kipato cha sasa, utaona umeme bei poa.
hiviii mara ya mwisho hizi MBUZI zako ziliongeza mshahara mwaka gani vilee?
 
Se
a rope na mabepari walisema itachukua miaka 3 hadi 4 bwawa hilo kujaa maji na linaweza liweze kujaa milele kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi. Wangeanza kulijaza mwezi Septemba masika ilipoanza, saa hizi lingalikuwa limejaa top.
September masika ya wapi nchi hii!?
 
Naomba kufahamu ndugu, hivi mnaposema bwawa nakua sielewi mbona huwa halioneshwi hilo bwawa ? Au bwawa lipo vp?

Nikiangaliaga kwenye TV sioni bwawa zaidi ya maeneo husika. Ufafanuzi
 
Wakina rope na mabepari walisema itachukua miaka 3 hadi 4 bwawa hilo kujaa maji na linaweza liweze kujaa milele kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi. Wangeanza kulijaza mwezi Septemba masika ilipoanza, saa hizi lingalikuwa limejaa top.
Acha uongo walisema misimu miwili mpaka mitatu ya mvua.... Naona chuki tu zimekujaa. Ulitamani angefeli ushabikie!!!

Kuna watu kama wachawi vile
 
Hivi umeme wa gass uliishia wapi, tusubili tuone huo umeme maana maneno yasiwe mengi tutalaumiana sana na kusifiana hovyo ila kila mtu anakua sahihi Mfano nikikumbushia gass ntalaumiwa maana tuliaminishwa kama haya haya ya bwawa mwisho wa siku hovyo na sasa bwawa tuacheni maneno tusubilini tuone, ila nachojua mimi uendeshaji wa mitambo mikubwa kama hii ni gharama kubwa hivyo tutegemee gharama za umeme kua kubwa, watu wasitegemee kabisa umeme kua rahisi utakua wa uhakika ila utakua ghali na kwahali ya uchumi wa nchi hii watu watapiga kelele sana.
Umeme wa gesi?? Hvi una taarifa umeme wa pale Kinyerezi 1 na 2 unazalisha zaidi ya 65% ya umeme wa Tanzania?! Wanajenga Kinyerezi 2 extension hivyo umeme wa kutegemea gesi utafika zaidi ya 70%!!

Muwe mnatafuta facts kabla ya kulalamika
 
Acha uongo walisema misimu miwili mpaka mitatu ya mvua.... Naona chuki tu zimekujaa. Ulitamani angefeli ushabikie!!!

Kuna watu kama wachawi vile
Mbona tunaongea lugha moja. Misimu ya mvua (aka masika) miwili hadi misimu mitatu ni sawa na miaka miwili hadi mitatu. Lakini bwawa limejaa top ndani ya msimu mmoja tu na walianza kulijanza miezi 3 baada ya msimu wa mvua kuanza. Masika huanza mwezi Septemba kumalizika mwezi Mei.
 
Mbona tunaongea lugha moja. Misimu ya mvua (aka masika) miwili hadi misimu mitatu ni sawa na miaka miwili hadi mitatu. Lakini bwawa limejaa top ndani ya msimu mmoja tu na walianza kulijanza miezi 3 baada ya msimu wa mvua kuanza. Masika huanza mwezi Septemba kumalizika mwezi Mei.
Screenshot_20230222_220229.jpg
 
Hivi umeme wa gass uliishia wapi,
Yule fisadi si alituingiza chaka gesi yetu akawagawia wachina baada ya kulamba cha juu, halafu akataka gesi ya kufua umeme tuwe tunainunua toka uchina kwa bei wanayotaka wao. Mungu na amlipe kabisa kwa ufisadi wake!
 
Hapa bongo sijui kama meme utakujaga kushuka bei
Ni Hivi, mkuu 'balimar', kama bado hujaisoma ramani ya Makamba na wenzake akina Maharage na Bodi iliyojaa walafi:

Umeme wa JNHP utakuwa nafuu sana, lakini nafuu hiyo hutaiona wewe na watumiaji wengine.

Kwa nini? Vikampuni vya hao jamaa na wanaowakaribisha kuja kuwekeza kwenye miradi ya umeme vitameza unafuu wote unaotegemewa na mradi huu, kwa wao kuzalisha umeme wa ghali ili waingize faida.

Ubaya wa umeme wa vikampuni hivyo ni kwamba, vizalishe au visizalishe umeme, bado vitakuwa vinalipwa.

Kwa hiyo wewe mtumiaji wa umeme ni lazima ukamuliwe, ili akina Makamba na mafisadi wezake wanufaike.

Ndiyo maana unasikia kelele nyingi sana siku hizi, kuhusu zile Megawatt 5,000 kabla ya 2025; hata kama hakuna shughuli zinazohitaji umeme wa kiasi hicho kufikia wakati huo.

Kwa hiyo hili inafaa ulielewe kungali mapema, uondoe matumaini yako ya kupata unafuu wa gharama za umeme
 
Hiyo asilimia 18 sasa itachukua miaka 6 kukamilika.
 
Hautashuka bei, ila kipato cha mtu mmoja mmoja kitaongezeka - hivyo kumudu kununua umeme kwa bei hiyo itakayopangwa. Hapo tukilinganisha na kipato cha sasa, utaona umeme bei poa.
Wewe unaangalia kipato cha mtu mmoja mmoja kwa maswala ya umeme?

Umuhimu wa umeme ni kuwezesha uzalishaji wa viwandani kuwa nafuu, ili bidhaa zinazozalishwa ziweze kuwa na ushindani katika soko.
Ethiopia wanazalisha umeme wa senti 30 za dola ya kimarekani, ndiyo maana wawekezaji wanakimbilia huko, kuliko kwenye nchi ambako kilowati inauzwa mara mbili au zaidi ya bei hiyo.

Hata sasa bei ya umeme Tanzania iko juu, kulinganisha na mataifa shindani, kwa hiyo ukisubiri watu wawe na uwezo wa kununua umeme ghali, eti kipato kimeongezeka, bado bidhaa zako hazitauzika sokoni.
 
Hapa napo tutegemee Marehemu kusimangwa kila ikitokea dosari kwenye uzalishaji wa umeme kwenye hili bwawa!
Mbona mnaweweseka sana?!!!!!!!! Vp, maombi yenu ya 'ashindwe' yanaelekea kushindwa nini?!!!
 
Back
Top Bottom