Bado nahitaji majibu kuhusu Ulinzi Shirikishi, Wanasheria nawaomba tafadhali

Bado nahitaji majibu kuhusu Ulinzi Shirikishi, Wanasheria nawaomba tafadhali

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,167
Reaction score
24,129
Kuna swala ambao hata mimi linaniumiza sana kichwa ki ukweli haya mambo ya ulinzi shirikishi hii nchi sijui yanatokea wpi yanaanzia wapi na yanaenda wapi, kuna hela zinachangishwa hizi hela anazila nani zinaenda wapi na kwanini tunachangishwa.

Mimi kama kawaida yangu n mzee wa kurudi nyumbani saa 7 usiku nikitoka n asubuh sana kwahyo mjumbe na vijakazi wake wanapokuja kudai dai hela wananikosa sasa naona wamentafuta wamechoka mwisho nmepokea msg et nadaiwa hela ya ulinzi shirikishi miezi 9 = 27,000 hivi hawa watu akili zao zina akili au vipi?

nikisema nisitoe kuna sheria yeyote itakayonibana? maana ki ukweli sielewi kazi ya JESHI LA POLISI hii nchi,kwani polisi kazi yao ni nini kama mwananchi anadaiwa na kulipishwa hela ya ulinzi? tena wengine tunakaa mitaa ambayo hata kibaka kupita tu anaogopa unajiuliza Huu ulinzi shirikishi sasa n wa kazi gani?

au ni miradi midogo midogo inayoratibiwa na wakubwa flani bila sisi wengine kujua? ki ukweli naombeni mnisaidie ufafanuzi maana nimejaribu kupitia thread hii hapa chini
Suala la Ulinzi Shirikishi ni la Kisheria?

sijaweza pata chochote kwenye comment labda n kwasababu thread n ya muda kidogo,basi kama n hivyo naomba mwenye kujua kuhusu hili swala anisaidie,ni haki kutoa hela za ulinzi? na ni nani aliyepanga kiasi cha kutoa? hizi hela zinaenda wapi mbona hata risiti n za mkono na sio mashine? kama kuingia choo cha stendi tu unapewa risiti ya mashine iweje ulinzi shirikishi risiti iwe ya mkono?

Wanasheria na Nyie wajumbe wa nyumba kumi najua mpo humu naomba ufafanuzi wenu kuhusu hili tafadhalini sana.
 
Utakuta unafanya kazi au biashara alafu unakatwa Kodi ambayo inatumika kuwa lipa hawa walinzi halali wa kikatiba wanaolipwa mishahara na kulishwa kutokana na Kodi unazokatwa alafu anatokea mtu mwingine kwa kutumia matope yake kichwani anasema changia 3,000 ya ulinzi shirikishi, lundo la mambo ya ajabu Tanzania sijui litaisha lini...
 
Bahati mbaya kiuwezo flan ambacho kinakupa jeuri flan na hata mashuleni tumefundishwa mambo ya social skills ulinzi unaanza kwako mwenyewe kabla ya kufika kwa walinzi wa kikatiba ambao kiuhalisia hawawezi kulinda kila mtaa, kitaa kulikuwa na hilo zoezi kuna jamaa mmoja yeye yupo njema full gate masai yupo getini yeye mwenyewe anakamguu ka kuku aligoma kuchangia 5k per month na shit kibao kwa madai yeye tayari anamlinzi hivyo hawezi kuchangia

siku ya siku kwenye issue zake huko wazee wa kazi wakamfatilia mpaka kwake walianza na masai kipigo akafungwa kamba mbwa wakatulizwa yeye akukuruke mbata mbili akatulia akachezea mapanga wazee wakabeba mzigo walinzi shirikishi walisikia timbwili ila jamaa alishawapiga mkwara wasije wakasogea kwake hivyo hawakutoa msaada wowote sasa hivi jamaa kawa muumini wa mambo ya kijamii sana
 
Utakuta unafanya kazi au biashara alafu unakatwa Kodi ambayo inatumika kuwa lipa hawa walinzi halali wa kikatiba wanaolipwa mishahara na kulishwa kutokana na Kodi unazokatwa alafu anatokea mtu mwingine kwa kutumia matope yake kichwani anasema changia 3,000 ya ulinzi shirikishi, lundo la mambo ya ajabu Tanzania sijui litaisha lini...
Hii nchi kuna kiongozi anahitajika nadhani tukimpata wa kufukurunyua haya ma ujinga nchi itakaa sawa.
 
Na ukiibiwa hao ulinzi shirikishi hawafidii chochote,kuna sehem wanachukua elf5 kwa frem ,ukijumlisha hiyo pesa inafika mill4 na ushee kwa mwezi.hii ndio TZ
hapo tu ndio wanaponichosha...
 
Inaudhi sana.

Kuna biashara kidogo nilikuwa nayo. Pia nina mlinzi. Wakija ulinzi shirikishi kuuliza nawaambia nina mlinzi. Wakaniandikia barua kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa wakinihitaji ofisini. Nikasema usumbufu wa kwenda ofisini kisa 3,000 hauna maana. Nikawalipa malimbikizo yao kwa masharti kuwa siku vurugu ikitokea wasipofika sitalipa.

Hazijapita siku nyingi timbwili likatokea. Wakati linaanza nikasema ngoja niwapigie kuwapa taarifa. Nikaongea nao huku nawarekodi. Bahati nzuri walikuwa maeneo ya karibu tu. Wakasema wanakuja. Haikupita muda wakaja.

Wamefika na virungu vyao. Nikawaambia sasa shughulikeni nao. Hawadhubutu hata kusogelea. Wakajishauri na kuniambia wapigie polisi. Nikawaambia majuzi nimewalipa hela, fanyeni kazi yenu. Wakasema ngoja tukusanye nguvu ikawa tiketi, hawakurudi. Tukafanya namna hali ikatulia.

Kesho nikatimba ofisini kwa mtendaji. Nikamuambia wakirudia kuja tena kudai watanifahamu.

Hawajawahi tena kuja mpaka sasa.

Hiyo ni miradi ya upigaji
 
Utakuta unafanya kazi au biashara alafu unakatwa Kodi ambayo inatumika kuwa lipa hawa walinzi halali wa kikatiba wanaolipwa mishahara na kulishwa kutokana na Kodi unazokatwa alafu anatokea mtu mwingine kwa kutumia matope yake kichwani anasema changia 3,000 ya ulinzi shirikishi, lundo la mambo ya ajabu Tanzania sijui litaisha lini...
Hii hoja muzuri sana.
Kwangu mimi nafikiri swala zima la ulinzi ndani ya mipaka ya nchi liachiwe jeshi la polisi.

Sababu kadhaa ni hizi
1. Jeshi la polisi wamefundishwa weledi katika kazi yao. Huku ulinzi shirikishi ni uhuni mtupu.
2. Swala la ushahidi ni rahisi kukusanywa kama kazi wanafanya jeshi la polisi tofauti na ulinzi shirikishi.
3. Ulinzi wetu umebadilika kwa kuongezewa teknolojia lakin hili limekuwa vigumu kutekelezwa nchini kwetu. Naamini hizi rasilimali za kuchangishana zikitumika kuwekeza katika teknolojia basi tutaboresha ulinzi. Teknolojia inawezesha kujua nyendo za wahalifu
 
Mkiwa humu mnajitapa na mabiashara yenu ila shilingi 3000 kwa mwezi inskushinda kwa ulinzi wa mali zako.


Poor You.
Nakusikitikia kwa sababu hujui thamani ya senti unayoitafuta usiku na mchana

katafute tajiri/boss unaemuona wewe ana hela kweli,halafu mwambie akupe 1000

uone atakupa au hatokupa? akikupa Kaa baada ya mwezi tena mfate muombe 1000 tena

asipokupa muulize kwann hajakupa na ana mali za kutosha,hela za kutosha,kwann akunyime 1000 tu.
 
Back
Top Bottom