mbeyakwetu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2016
- 723
- 398
hiki kimradi kipo pia mwanza wilaya ya ilemela mtaa wa gedeli yaan ukihoji Sana unaambiwa utalipa fain 50000 lakini sijawai kuona kazi yao hata siku moja maan.
nmekuelewa sana mkuu.AsanteCONTROLA mimi sio mtaalamu wa sheria lakini ninajua kidogo kwa uchache sana.
Kuna aina nyingi za sheria na zingine zinafanya kazi kwa baadhi ya maeneo husika tu,na kutungwa katika eneo hilo.
Mfano wilaya A inaweza kuweka kikao wakadhamiria mwisho kutembea ni saa 3 usiku na faini ni 50,000/ atayefuata sheria hii ni wale watao ishi eneo husika tu.
Turudi kwenye hoja yako hayo malipo ya elfu 3 yamepangwa katika mkutano na ni makualiano ya wakazi wa eneo unaloishi wewe hukudhuria itakuwa.
Inaenda wapi? Mara hiyo pesa iinatumika kununua mahitaji ya wanaolinda usiku(silaha za jadi) panga, rungu, jacket kwa ajili baridi na ingine inayobakia ni kama posho.
Sio lazima athari ya wizi ifanyike mahali ndio eti ulinzi uwekwe, sio wajibu kuacha kujilinda mwemyewe kwa kuwa et! Polisi wapo,jilinde kabla haujalindwa.
Kuna baadhi ya maeneoa nimewai kuishi hautozwi pesa yoyote mchango ni kila nyumba yenye kijana wa kiume atalinda kwa wiki mara 2 kwahiyo ni mwendo wa shift zamu kwa zamu leo hawa kesho wengine maisha yanaenda na sikuwa kulinda nilihama,sio sheria ya kitaifa kwamba haibadiliki.
Kupanga ni kuchagua kulipa au kutolipa,shiriki au kutoshiriki.
Hawalindi mkuu,mimi ni mtu wa kurudi kwangu usiku sanaHakuna kitu hapo, labda kama hujui kuhusu ulinzi shirikishi. Hao ni kulinda tu ila kuibiwa iko palepale na hulipwi au kusaidiwa.
Mfano niliwahi kuwa na ofisi magomeni na kukawepo na hao jamaa zako pamoja na kampuni ya ulinzi, ilitokea mwenzetu kuibiwa dukani kwake, mgogoro ulianzia hapo na mpaka mradi wa kulinda ukaishia hapo.
Na tulikuwa tunatoa 4000/= kila mlango mara milango 50.
Na haswa ukiwa siyo wa mtaa husika....ni kikundi cha wahuni Fulani wanajipanga kazi tu.Sungusungu ilikua zamani nyumba kwa nyumba zamu kwa zamu ...Ila Hawa wa Sasa ukiwa challenge kuhusu uhalali wao wanakufanyia mpango uibiwe ili uone umuhimu wao...Cha ajabu zaidi hao hao ulinzi shirikishi ndio vibaka wenyewe , wakikukuta usiku umelewa au umetembea na mali lazima wakupore.
Wengi wamejitahidi kukujibu. Na mimi naongeza kidogoKuna swala ambao hata mimi linaniumiza sana kichwa ki ukweli haya mambo ya ulinzi shirikishi hii nchi sijui yanatokea wpi yanaanzia wapi na yanaenda wapi, kuna hela zinachangishwa hizi hela anazila nani zinaenda wapi na kwanini tunachangishwa.
Mimi kama kawaida yangu n mzee wa kurudi nyumbani saa 7 usiku nikitoka n asubuh sana kwahyo mjumbe na vijakazi wake wanapokuja kudai dai hela wananikosa sasa naona wamentafuta wamechoka mwisho nmepokea msg et nadaiwa hela ya ulinzi shirikishi miezi 9 = 27,000 hivi hawa watu akili zao zina akili au vipi?
nikisema nisitoe kuna sheria yeyote itakayonibana? maana ki ukweli sielewi kazi ya JESHI LA POLISI hii nchi,kwani polisi kazi yao ni nini kama mwananchi anadaiwa na kulipishwa hela ya ulinzi? tena wengine tunakaa mitaa ambayo hata kibaka kupita tu anaogopa unajiuliza Huu ulinzi shirikishi sasa n wa kazi gani?
au ni miradi midogo midogo inayoratibiwa na wakubwa flani bila sisi wengine kujua? ki ukweli naombeni mnisaidie ufafanuzi maana nimejaribu kupitia thread hii hapa chini
Suala la Ulinzi Shirikishi ni la Kisheria?
sijaweza pata chochote kwenye comment labda n kwasababu thread n ya muda kidogo,basi kama n hivyo naomba mwenye kujua kuhusu hili swala anisaidie,ni haki kutoa hela za ulinzi? na ni nani aliyepanga kiasi cha kutoa? hizi hela zinaenda wapi mbona hata risiti n za mkono na sio mashine? kama kuingia choo cha stendi tu unapewa risiti ya mashine iweje ulinzi shirikishi risiti iwe ya mkono?
Wanasheria na Nyie wajumbe wa nyumba kumi najua mpo humu naomba ufafanuzi wenu kuhusu hili tafadhalini sana.
3000 kwa maskini kama mimi ni kubwa sana
kama wewe unayo ni wewe, mimi sina 3000
inaenda wapi hiyo 3000 ninayoitoa, inajaza gari mafuta au?
Story zenu za kitoto pelekeni huko fb! Ulinzi shirikishi upo maeneo mengi! Na hii huwa ni makubaliano ya wananchi sehemu husika pamoja na serikali zao za mitaa au vijiji! Tunachangia! Hawa uwezo wao ni kuwazuia vibaka! Majambazi wenye silaha wanadhitiwa na polisi
Mkuu mimi sio jinsia ya kikeTumekuelewa Mama Prisca
umemfundisha wewe kulinda usiku au unaongea tu bila kufikiria? suala la kukabiliana na wahalifu wamepewa jeshi la polisi sisi wananchi tunachotakiwa ni kuwapa ushirikiano! huyu ndugu yetu anataka haki yake ni ipi na wajibu wake ni upo!? sasa watz tulio wengi tunapenda kurahisisha vitu et kosa nmegoma kutoa elfu Moja ndio unishirutishe kukesha usiku!? Ishu sio elfu Moja ishu ni haki yangu kutoa? Au ni wajibu wangu kulinda mtaa?Chief kaa na balozi wa mtaa wako akupe maelezo kuhusu ulinzi wa mtaa wenu kama una maswali atakupa majibu.
Kama hutaki kutoa pesa unaweza kujiunga na walinzi kulinda.