CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,167
- 24,129
- Thread starter
- #21
wala sikupingi mkuu ila hii nchi bado kuna mijitu kwao haioni kama inapigwaInaudhi sana.
Kuna biashara kidogo nilikuwa nayo. Pia nina mlinzi. Wakija ulinzi shirikishi kuuliza nawaambia nina mlinzi. Wakaniandikia barua kutoka kwa afisa mtendaji wa mtaa wakinihitaji ofisini. Nikasema usumbufu wa kwenda ofisini kisa 3,000 hauna maana. Nikawalipa malimbikizo yao kwa masharti kuwa siku vurugu ikitokea wasipofika sitalipa.
Hazijapita siku nyingi timbwili likatokea. Wakati linaanza nikasema ngoja niwapigie kuwapa taarifa. Nikaongea nao huku nawarekodi. Bahati nzuri walikuwa maeneo ya karibu tu. Wakasema wanakuja. Haikupita muda wakaja.
Wamefika na virungu vyao. Nikawaambia sasa shughulikeni nao. Hawadhubutu hata kusogelea. Wakajishauri na kuniambia wapigie polisi. Nikawaambia majuzi nimewalipa hela, fanyeni kazi yenu. Wakasema ngoja tukusanye nguvu ikawa tiketi, hawakurudi. Tukafanya namna hali ikatulia.
Kesho nikatimba ofisini kwa mtendaji. Nikamuambia wakirudia kuja tena kudai watanifahamu.
Hawajawahi tena kuja mpaka sasa.
Hiyo ni miradi ya upigaji
na haiumii wala kuuliza inachukulia kawaida,nikiona mijitu ya namna hii kwenye comment
huwa naskia kuuma meno kwa hasira maana hii mijitu ipo mingi kuliko watu wanaojitambua.