Bado nahitaji majibu kuhusu Ulinzi Shirikishi, Wanasheria nawaomba tafadhali

hiki kimradi kipo pia mwanza wilaya ya ilemela mtaa wa gedeli yaan ukihoji Sana unaambiwa utalipa fain 50000 lakini sijawai kuona kazi yao hata siku moja maan.
 
nmekuelewa sana mkuu.Asante
 
Hawalindi mkuu,mimi ni mtu wa kurudi kwangu usiku sana

nimeshawahi wakuta mahali hawa shirikishi wamejifunika

mashuka wamelala usingizi mzuri sana kiasi kwamba ingekua

nataka kuwadhuru basi ningeweza wafanya chochote kile

Usiku wanalala tofauti n kwamba wao wanalala nnje na sio ndani.
 
Hizo sheria ndogo si zinatambulika kisheria.

Yawezekana wakazi wa eneo husika waliketi wakakubaliana hivyo ila kwa kuwa unarudi home usiku wa "manani" huna taarifa.
yawezekana...
 
Cha ajabu zaidi hao hao ulinzi shirikishi ndio vibaka wenyewe , wakikukuta usiku umelewa au umetembea na mali lazima wakupore.
Na haswa ukiwa siyo wa mtaa husika....ni kikundi cha wahuni Fulani wanajipanga kazi tu.Sungusungu ilikua zamani nyumba kwa nyumba zamu kwa zamu ...Ila Hawa wa Sasa ukiwa challenge kuhusu uhalali wao wanakufanyia mpango uibiwe ili uone umuhimu wao...
 
ulinzi shirikishi ni mradi ya kipigaji tu
hukuna ulinzi kwa hawa vibaka wanaokuwa walinzi usiku
mtaani kwangu nyumba nane zimeibiwa betri za gari, cha kushangaza ni nyumba gari zao hazina security system,
mwenye security hazijaguswa kabisa, kama sio walinzi ni nani kafanya?

mtoa mada usiwape mishahara hao wajumbe wa ccm, waambie waende lumumba wakadai mishahara
 
We elewa ulinzi shirikishi ni kwamba unaweza kuwakata WAJUMBE na kuwaweka chini ulinzi kwa dakika thelathini 30 (citizen arrest)
 
Ulinzi shirikishi ni utaratibu uliowekwa ili kuwalipa vibaka wa mtaani kwako mshahara wa kila mwezi ili kuwarubuni wasikuibie/ kukudhuru.

Ndio maana utasikia maeneo kama ya Manzese watu wanajitapa vibaka wamepungua sana.
 
Wengi wamejitahidi kukujibu. Na mimi naongeza kidogo

1. Mchango huo sio wa kisheria, ni wa kijamii - hulazimiki kuchanga

2. Waliopanga mchanga na kiwango cha huo mchango ni nyie wenyewe kupitia mikutano ya mtaa, kutakuwa na mukhtasari wa kikao ofisi ya mtendaji wa mtaa

3. Fedha matumizi yake ni kama mlivyokubaliana kwenye mkutano wa mtaa. Hayafanani kwa mitaa yote

4. Hupewi risiti ya mashine sababu hiyo sio shughuli ya serikali bali ya kijamii. Mapato yake hayaingii serikalini kama kodi.

NB:
Kuna haki ya kijamii (moral right) inayokuwa wajibu kwa mtu mwingine na kuna haki ya kisheria (legal right) ambayo ni lazima kuitekeleza na utekelezaji wake unaweza kudaiwa mahakamani.

Mfano: Mzazi asiyejiweza kutunzwa na Mtoto wake mkubwa mwenye uwezo wa kujitafutia kipato - moral right, sio lazima mtoto kuitekeleza, haina adhabu ila jamii itakushangaa kwa kumtelekeza mzazi

Mfano 2: Mtoto kusomeshwa na mzazi wake au kupewa chakula na malazi - legal right - ni lazima mzazi kuitekeleza, ukikaidi mtoto akikupeleka mahakamani utaitekeleza kwa nguvu.

Nafikiri nimekujibu ipasavyo mkuu
 
3000 kwa maskini kama mimi ni kubwa sana

kama wewe unayo ni wewe, mimi sina 3000

inaenda wapi hiyo 3000 ninayoitoa, inajaza gari mafuta au?

Wanalipwa hao vijana wanaokulinda ukiwa unakoroma usiku, pamoja na vifaa vyao vidogo dogo watumiavyo kazini.
 

Tumekuelewa Mama Prisca
 
Serikali inafeli sana, tunalipa kodi lakini watu wanapita kudai michango ya ulinzi na kututisha.

Nipo hapa nimetulia natafuta sheria ipi inasema tuchangie ulinzi shirikishi.
Sina mpango wa kuwalipa vibaka wa mtaani.
 
Chief kaa na balozi wa mtaa wako akupe maelezo kuhusu ulinzi wa mtaa wenu kama una maswali atakupa majibu.

Kama hutaki kutoa pesa unaweza kujiunga na walinzi kulinda.
umemfundisha wewe kulinda usiku au unaongea tu bila kufikiria? suala la kukabiliana na wahalifu wamepewa jeshi la polisi sisi wananchi tunachotakiwa ni kuwapa ushirikiano! huyu ndugu yetu anataka haki yake ni ipi na wajibu wake ni upo!? sasa watz tulio wengi tunapenda kurahisisha vitu et kosa nmegoma kutoa elfu Moja ndio unishirutishe kukesha usiku!? Ishu sio elfu Moja ishu ni haki yangu kutoa? Au ni wajibu wangu kulinda mtaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…