Bado najifunza ila zifuatazo ni baadhi ya chachu zinazopelekea mafanikio kwa mtu.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
 BAHATI
Mfano: Kuzaliwa katika familia ilio na mafanikio kupelekea kupatiwa mtaji, kurithi mali au kujiungana na biashara ya familia.

Mfano: Mara paap unachimba kisima eneo la nyumbani kwako unakutana na ukanda wa dhahabu.

KUKUTANA NA WATU SAHIHI KATIKA WAKATI SAHIHI NA MAHALI SAHIHI.
Mfano: Kuna watu tunao mtaani ambao kila mtu anawasifia upeo wao kutokana na skillset maalum waliyonayo ila upeo wao huo unaishia kuwa wasted mtaani bila kunafaika nao. Sio kwamba hawakupambana ila ni basi tu "watu, muda na mahali" havikulandana perfectly kwa ajili yao.

Mfano: Kuna watu walio katika nyadhifa fulani hawako productive ila wanaendelea tu kuwa katika system hata akitolewa katika posts zake mara kwa mara.

PERSEVERANCE (HALI YA MUENDELEZO LICHA YA UGUMU WA SWALA UNALODEAL NALO)
PERSISTENCE (HALI YA KUWA NA MUENDELEZO LICHA YA VIKWAZO NA CHANGAMOTO VYA KUKURUDISHA NYUMA)

Yani kuna wana ambao ni kama safari ya kutafuta mafanikio kwao ndio pumzi yao. Yani wako dedicated hata kama wasipopata return on investment kwa muda mrefu. Kwa hio unakuta katika safari hii ya muendelezo ndio anajifunza kutokana na makosa, anakutana na watu sahihi, anakutana na fursa mpya, anatengeneza uzoefu zaidi, anakuwa mbunifu zaidi na msimamizi mzuri wa fedha.

KUIKABILI HOFU, DUKU DUKU NA AIBU
Watanionaje?
Ila sijasoma.
Mimi sio wa hadhi ya kazi hii.
Sina uzoefu nalo.
Ila kila mtu alifeli hapa.
Bila kwa mganga hauwezi tusua.
Mbona wakulima wote ni masikini.

DISCIPLINE (NIDHAMU)
Discipline ndio itakufanya uheshimu mpangilio na asili ya pesa.

Discipline ndio itakufanya ufanye kazi huku ukiheshimu kazi yako.

Discipline ndio itafanya uaminike.

Discipline ndio itakufanya uwe na fikra pevu na utulivu katika maamuzi

Discipline ndio itakufungulia milango ya mbinguni.

MUNGU ABARIKI KAZI ZA MIKONO YENU
 
PERSEVERANCE (HALI YA MUENDELEZO LICHA YA UGUMU WA SWALA UNALODEAL NALO)
PERSISTENCE (HALI YA KUWA NA MUENDELEZO LICHA YA VIKWAZO NA CHANGAMOTO VYA KUKURUDISHA NYUMA)

Yani kuna wana ambao ni kama safari ya kutafuta mafanikio kwao ndio pumzi yao. Yani wako dedicated hata kama wasipopata return on investment kwa muda mrefu. Kwa hio unakuta katika safari hii ya muendelezo ndio anajifunza kutokana na makosa, anakutana na watu sahihi, anakutana na fursa mpya, anatengeneza uzoefu zaidi, anakuwa mbunifu zaidi na msimamizi mzuri wa fedha.
Hiki kipengele ni muhimu sana. Kuna jamaa namfahamu ni rafiki yangu amekomaa na biashara yake tangu 2015 kwa mtaji mdogo sana. Imemchukua zaidi ya miak 8 sasa hivi amekuwa na jina kariakoo la mali kauli, ana cash in bank ya zaidi ya milioni 50 na iliyo kwenye mzunguko bidhaa anazouza zaidi ya milioni 80. Na ana assets nyingine. Huenda bado hajafikia mafogo lakini ile safari ya mtaji wake mdogo na magumu aliyopitia kwangu mimi nikishuhudia juhudi zake na kutokata tamaa wakati tukimpa deals nyingine yeye anasema aaah mimi nababaki na jambo hili hili tu.
Alianza na mtaji wa milioni 1.8. Kweli usiache safari yako hata siku moja.
 
Aiseeee kweli watu wapo focuses
 
Back
Top Bottom