G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Hapa ndipo daraja la Tshs bilioni 700, fedha ambazo hata hazikujadiliwa na bunge zinatumika. Eneo ni Kigongo-Busisi. Kwakweli Bunge la Ndugai litajibu haya mbele za Mungu!
Nawaza tu bilioni 700 Tshs ambazo ni hela nyingi sana yani hata Richmond haioni nusu yake. Kama zingetumika kwa mtu kuona mbali. Kuliko kujenga hilo daraja litakalopitisha Hiace na mbaya zaidi kama tozo zitakuwa kubwa maana hili eneo lina watu wa kipato cha chini sana basi wakaamua kuachana na kulitumia wakaendelea na usafiri wao wa feri.
Embu tuangalie kama tungewaza vyema kwa hii bilioni 700
1. Tungechukua tu hapo kidogo tukawanunulia feri za kisasa.
2. Tukatumia hapo fedha nyingine kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo kama kuwapa mikopo yenye riba nafuu kisha mzunguko wao wa hela ukawa mkubwa. Yani kiufupi tungefanya mambo mengine mengi sana na hii hela! Ila kwa kuzitumia kwenye huu mradi ni HAPANA!
Yani Magufuli alifanya tu ziara hapo akakumbuka kuwa alikuwa anachunga ng'ombe eneo hilo basi hapo hapo akaamua lijengwe daraja na tena akatamka kuwa wajenge chap chap maana kama atakuja Rais mwingine ataufuta huo mradi! Kumbe hata yeye akilini mwake anajua kuwa ni mradi wa hovyo kupindukia!
Naumia maana gharama za mradi huu unazidi ule wa Kigamboni ambao walau ulikuwa na maana ingawa nao ulishavurugwa vurugwa na kweli fedha zinatumika isivyo kabisa!