Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Uhuru wa mawazo ni mzuri lakini kwa watu wa upande wa mwanza hii ni faida na inaokoa muda sana...kuvuka pale ferry ukikuta dude limetembea unasubiri muda mrefu Sana na like Kuna watu wengi mno na magari wanalata shida Sana tu sema ndio hivo tunaona shida ya mwenzio soup yako, yaani kwa umuhimu ni bora zaidi kuliko daraja la Kigamboni.
Sasa ngoja hilo daraja likamilike uone watakaopita hapo kama watakuwa wengi kuzidi feri. Hivi unajua kurudisha bilioni 700 wewe! Hizo hela ni nyingi sana kwa kuelekeza kwenye mradi kama ule. Anyway ila Jiulize kwanini hata yeye Magufuli anahisi alifanya kitu kisicho na tija hadi anahimiza waharakishe ili Rais mwingine asije akaufuta huo mradi.
 
Ni vizuri kutafakari mambo kwa kina, na wanapouliza watu maswali kama haya wapewe majibu, siyo kuambiwa ni vibaraka wa mabeberu.
 
Ni kutupa fedha za maskini baharini. Bilioni 700 tungejenga barabara kilometer 700 kanda ya ziwa ingeunganishwa wilaya zote kwa barabara safi ya lami.
Bado usingekosa cha kusema pia kama hizo bil 700 zingetumika kujenga barabara kanda ya ziwa pekee tatizo lako naona sio daraja bali ni daraja kujengwa kanda ya ziwa ambako kwa akili yako unaamini halistihili kujengwa kwa hiyo hata barabara ungesema pia na sidhani kama ulishawahi kuitumia hiyo njia ungelikua umewahi kuitumia usingelalama hapa hilo daraja kujengwa.
 
Daraja muhimu sana hilo, litaondoa adha ya kuvuka pale Kamanga ferry, litarahisisha magari ya mizigo toka kagera kuingiza mzigo mjini mfano ndizi, maharagwe etc.

Wakulima wa sengerema, Geita pia ni wanufaikaji wa hili daraja.

Mda mwingi hupotea kusubiri ferry
 
Mantiki ni kuunganisha kwa huduma za usafiri ukanda huo ili kukuza utalii, sekta ya madini, uvuvi, afya, biashara na nchi jirani, kufungua uwekezaji wa hoteli za kisasa katika pwani yote ya ziwa victoria inayozu guka maeneo hayo na kuchochea fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo usafiri wa haraka kwa wakaazi zaidi ya 5.6Millioni.

Ningelikuwa mimi ningeliuliza ufanisi wa daraja la kigamboni, flyovers na ujenzi wa viwanja vya ndege nchi nzima.

Daraja la kigongo-busisi umuhimu wake unafanana na daraja la Mkapa.
 
Unalalamikia daraja kujengwa kwa B700, hivi unajua ile T1.5 ilienda wapi?
 
Sasa ngoja hilo daraja likamilike uone watakaopita hapo kama watakuwa wengi kuzidi feri. Hivi unajua kurudisha bilioni 700 wewe! Hizo hela ni nyingi sana kwa kuelekeza kwenye mradi kama ule. Any way ila Jiulize kwanini hata yeye Magufuli anahisi alifanya kitu kisicho na tija hadi anahimiza waharakishe ili Rais mwingine asije akaufuta huo mradi.

Daraja haliwezi kurudisha gharama kama unavyowaza wewe mfanyabiashara, daraja hata kama linahitaji kurudiaha lakini ni kwa kiasi kidogo sana, lengo ni kuihudumia jamii.

Kwanza unatakaje mtu mjinga awepo Ikulu kisha afanye yale unayo taka wewe tu? Kweni wewe nani mpaka tukubali mawazo yako tu?wale waliojaa pale Kigamboni kushukuru ujenzi wa daraja walikua ni wajinga na wewe peke yako ndo una akili? Maendeleo yatakwenda pote nchini kwa kila wakati na kila kiongozi atakaye kuja.
 
Si kila daraja lipo kwa ajili ya kupata faida. Mwanza kuna hospitali kubwa ya kanda, unapotumia feri wagonjwa wanachelewa kuvuka na kuhatarisha uhai/afya wao/zao.

Pia kivuko cha feri hakiaminiki si tu kwa usalama lakini pia hata utengemano si muda wote kitakuwa kizima.

Na inawezekana hata hata kwa mwaka usiwahi kupita kwenye njia hii.

NOTE: NIMEKUJIBU LAKINI NATAMBUA WAZI UPO MLENGO WA KUPINGA.
Kanda kw asas ani kwa kila Mkoa
 
Watu wengi mnaojadili hili swala mnaweza msifahamu viashiria vya nchi kukua kiuchumi, au pia mnaweza msifahamu uhandisi ujenzi na faida zake, nafikiri pia mppaka mradi huo kuwa executed wataalamu wa kutosha wa kila nyanja walijumuishwa, sio mradi wa bahati mbaya au fikra za mtu mmoja.
 
G Sam,

Utawala wa awamu ya tano awamu ya kidikteta umejaa mapungufu ufisadi wa kutisha na itokee ya Malawi ili CCM ifeli kufanya uchakachuaji wizi wa kura na wapinzani waingie ikulu lazima mtukufu atakuwa akishinda mahakamani kama Jacob zuma wa Africa Kusini.
 
Watu wengi mnaojadili hili swala mnaweza msifahamu viashiria vya nchi kukua kiuchumi, au pia mnaweza msifahamu uhandisi ujenzi na faida zake, nafikiri pia mppaka mradi huo kuwa executed wataalamu wa kutosha wa kila nyanja walijumuishwa, sio mradi wa bahati mbaya au fikra za mtu mmoja.
Kwa vile hilo daraja halipo uchaggani ndo maana anaponda. I bet siku zijazo watu watajua umuhimu wake. Safari za majini si za kuaminika. Mara ngapi hicho kivuko kinazima sababu ya magugu maji, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe.
 
Kwa vile hilo daraja halipo uchaggani ndo maana anaponda. I bet siku zijazo watu watajua umuhimu wake. Safari za majini si za kuaminika. Mara ngapi hicho kivuko kinazima sababu ya magugu maji, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe.
Asante sana!
 
Daraja hili ni maelekezo ya ilani na wananchi waliichagua CCM kwa ilani yake. Huu ni utekelezaji tu .Siyo kila kinachofanyika kanda ya ziwa ni kibaya mnapinga.La hasha. Tulieni wote tupate maendeleo
 
sasa hivi mmegeuka kuwa wachumi elekezi!
Mambo ya vivuko yameshapitwa na wakati basi tu hatuna jinsi
nchi haijengwi kwa maboksi,kupanga ni kuchagua brother
Ila Jiwe ni mpigaji sana, hivi ndiye alinunua kile kivuko kibovu?
 
Back
Top Bottom