Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Mayanga Construction Company Limited! Tenda nyumbani

IMG_20200807_174533_061.jpg
IMG_20200807_174357_524.jpg
 
Bunge lilihadili wakati wabunge wenu wamejifungia kupigana miti wakisingizia korona.

Mantiki utaijuaje wewe hata hesabu hujui. Muda watu wanapoteza hapo, pesa wanayolipa kuvusha magari na watu, haya kwa uchache kakake pale upige hesabu kisha ukipata jibu utuambie hiyo pesa itarudi baada ya muda gani.
 
Nyie hamna jema katika nchi hii.

Sasa hivi unaleta unafiki wako hapa wa Bora angenunua feri mpya wakati nyie hao hao mlikuwa mna mubeza kukarabati na kujenga meli mpya za ziwa Victoria kwa kusema hivyo siyo vipa umbele vya Tanzania.

Shame on you Wanafiki Wakubwa nyie.
 
Tungechukua tu hapo kidogo tukawanunulia feri za kisasa.

2. Tukatumia hapo fedha nyingine kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo kama kuwapa mikopo yenye riba nafuu kisha mzunguko wao wa hela ukawa mkubwa. Yani kiufupi tungefanya mambo mengine mengi sana na hii hela! Ila kwa kuzitumia kwenye huu mradi ni HAPANA!
Sasa hivi mmegeuka kuwa wachumi elekezi! Mambo ya vivuko yameshapitwa na wakati basi tu hatuna jinsi nchi haijengwi kwa maboksi, kupanga ni kuchagua brother.
 
Uhuru wa mawazo ni mzuri lakini kwa watu wa upande wa mwanza hii ni faida na inaokoa muda sana, kuvuka pale ferry ukikuta dude limetembea unasubiri muda mrefu Sana na like Kuna watu wengi mno na magari, wanalata shida Sana tu sema ndio hivo tunaona shida ya mwenzio soup yako, yaani kwa umuhimu ni bora zaidi kuliko daraja la Kigamboni.
 
G Sam,

Linganisha na daraja la kigamboni, kwani hakuna feri? Linganisha na daraja la MKapa, kwani hapakuwa na feri? Unapita siku moja unakuta Hiace, unatoa maamuzi ya mtu ambaye hakuiona shule. Ni matatizo ya kushinda ofisini na kijiweni ukijadili yanga na simba. Uliza tulioko ktk biashara tukueleze umuhimu wake badala ya kujiandikia na kubandika picha za mtandaoni. Mtu kama wewe ndo munasababisha rais anaamua kupanga matumizi ya bajeti maana ukisikilizwa, tunajikuta tunasumbuliwa na IQ ndogo.
 
Hizi billion 700 zimetumika vibaya kujenga daraja. Mimi naungana na mleta mada, ila nimuongezee point ya 3. Baada ya kujenga daraja watumie hizo hela kuwanunulia watu wanaopita sehemu hiyo vitumbua na maandazi ili kuboresha afya zao! Imagine, kwa hela hiyo si watakula na kuacha kusafiri mara huku mara kule!
 
Kufikiri kwako ni kudogo kuliko jamii ya ng'ambo ya pili kutoka Mwanza mjini kwa maana ya Sengerema, Geita, Bukoba, Kigari, Bunjumbula na Kampala.

Una matatizo kichwani
 
Nyie hamna jema katika nchi hii.

Sasa hivi unaleta unafiki wako hapa wa Bora angenunua feri mpya wakati nyie hao hao mlikuwa mna mubeza kukarabati na kujenga meli mpya za ziwa Victoria kwa kusema hivyo siyo vipa umbele vya Tanzania.

Shame on you Wanafiki Wakubwa nyie.
Nani kabeza kujenga hizo meli?
 
Naomba nieleze umuhimu wa hili daraja japo kidogo. Mimi kwa macho yangu nimewahi kushuhudi watu wawili wakikata roho kisa wameacha nafeli ambayo ilipashwa kuwavusha na kuwapeleka Bugando hospital, kutokuwepo kwa daraja kuna sababisha watu kupoteza takribani SAA moja na zaidi wakisubiri kuvuka. Hivyo kujengwa kwa daraja hili kutawafanya watu wasipoteze muda wao na hivyo kunusuru maisha ya wengi.

Lakini pia kwa sissi wafanyabiashara tunapoteza muda mwingine sana kukaa foleni kusubiri usafiri wa kwenda upande wa pili hivyo kujikuta tunapoteza muda na pesa.

Mungu ambariki sana jpm kwa wazo hili, kati ya miradi yote aliyoinzisha jpm huu ndo umenigusa moja kwa moja hivyo naamini kwa sisi wakazi wa kanda ya ziwa lazima tumpatie ushindi mnono JPM.

Na kwa taarifa yako hili daraja kwa jpm ni turufu kubwa sana kwa wapiga kura wake.

Long live JPM

IMG_20200823_141425_8.jpg
IMG_20200823_141425_8.jpg
 
Nahisi hujawahi kupita njia hiyo kuona wasafili tunavyo pata taabu na hizo feri! Lakini pia kuna ubaya gani mtu Kuchagua mwenyea apande feri au avuke kwa barabara kama ilivyo kigamboni huko dar? Nyie watu hebu acheni wivu, daraja litajengwa, feri zitakuwepo pia! Acheni roho za korosho
 
Lissu alipita hapo kigongo ferry akaubeza huo mradi lakini mhe Magufuli aliusifia na kueleza umuhimu wake. Ngoja tuone tar 28 wananchi watatuambia.

Mimi ninavyofahamu hilo eneo kwa siku linapitisha magari na watu wengi sana. Kuvuka kwa kivuko inakula kama dk 30 mpaka 45.
Mimi mwenyewe ni mkaazi wa Usagara na ninasubiri daraja hilo kinipe faida na wenzangu wa upande wa pili wapate kitu, nina eneo kule Busisi ambalo daraja likipita na kukawa na urahisi wa kwenda na muda mchache wananchi wa kule watanifaidisha na mimi nitawafaidisha, kiufupi mradi huo utatupa maendeleo makubwa sisi tuliopo kama walivyopata irahisi wa maendeleo watu Kigamboni.

Mada zingine ni za watu wajinga wajinga tu wenye roho mbaya za kikaburu.
 
Si kila daraja lipo kwa ajili ya kupata faida. Mwanza kuna hospitali kubwa ya kanda, unapotumia feri wagonjwa wanachelewa kuvuka na kuhatarisha uhai/afya wao/zao.

Pia kivuko cha feri hakiaminiki si tu kwa usalama lakini pia hata utengemano si muda wote kitakuwa kizima.

Na inawezekana hata hata kwa mwaka usiwahi kupita kwenye njia hii.

NOTE: NIMEKUJIBU LAKINI NATAMBUA WAZI UPO MLENGO WA KUPINGA.
Bila shaka na wewe umejibu kama ulivyojibu kwa SABABU UPO KWENYE MLENGO WA KUUNGA MKONO kila kitu hata kama ni cha kijinga!!!!

Kama hoja yako ni ya msingi, mwambie akawajengee daraja watu wa Kitunda, Lindi kwa sababu hata hicho kivuko hawana na wanatumia mitumbwi!

Aende akawajengee daraja watu wa Bwejuu, Jibondo, na Chole Mafia ambao nao wanatumia mitumbwi!
 
Back
Top Bottom