Mantiki ni kuunganisha kwa huduma za usafiri ukanda huo ili kukuza utalii, sekta ya madini, uvuvi, afya, biashara na nchi jirani, kufungua uwekezaji wa hoteli za kisasa katika pwani yote ya ziwa victoria inayozu guka maeneo hayo na kuchochea fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo usafiri wa haraka kwa wakaazi zaidi ya 5.6Millioni.
Ningelikuwa mimi ningeliuliza ufanisi wa daraja la kigamboni, fryovers na ujenzi wa viwanja vya ndege nchi nzima.
Daraja la kigongo-busisi umuhimu wake unafanana na daraja la Mkapa.
Kwa hili nami natia hoja hapa;
Ujenzi wa daraja la Busisi-Kigongo sio kweli kwamba hauna umuhimu kama wachangiaji wengi wasemavyo ila tujaribu kuangalia kwa mapana sana huku tukihusianisha gharama, mahitaji na alternatives ya mahali husika.
1. Kwa sasa mradi huu wa Tshs.700b kwa ujenzi wa daraja tena sehemu moja tu mimi naona ni matumizi yasiyokuwa na tija. Hii ni pesa nyingi sana kwa eneo hili ikiishia kwenye mradi mmoja tu huku ikiacha changamoto zingine lukuki za eneo hilo.
Maeneo ya kanda ya ziwa bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi majumbani hasa kwenye maeneo hayo hayo ya Misungwi, Sengerema, Geita, Nyamagana n.k kwanini pesa hii isitatue changamoto hii kwanza?
Maeneo mengi ya kanda ya ziwa bado barabara ni changamoto, ni mbovu na hazina lami ambapo kama inshu ni kuwahisha wagonjwa Bugando bado wengi wanacheleweshwa na barabara mbovu huko watokako kwanini pesa hii isitatue changamoto hii kwanza?
Ni kweli kusubiri vivuko pale ni kero kubwa sana lakini hili linatatulika kwa kuongeza idadi ya vivuko kuendana na mahitaji, hakika pale vikiongezwa vivuko vingine kama viwili au vitatu vyenye ukubwa na speed ya kutosha hakutakuwa tena changamoto ya foleni mahali pale ambapo ujenzi wa vivuko hivyo hauzidi bilioni 5 kwa kila kimoja pesa ambayo ingeweza kutumika haizidi bilioni 15 na kuacha hela zingine zikaingia kwenye hiyo miradi ya maji na ujenzi wa barabara za lami kanda ya ziwa.
Shida ninayoiona mimi ni maamuzi ya nchi hii kuwa ni ya mtu mmoja mwenye madaraka na mamlaka makubwa sana, akiamua tena majukwaani tu bila kutumia vyombo vya ushauri hili linatugharimu kama taifa. Watendaji wengine wamekuwa ni waoga kushauri kitaalamu maana hawawezi kumkosoa boss wao( kushauri maamuzi ya mkuu ni kumkosoa).
Turudi kwenye uongozi unazingatia kanuni za kiuongozi laiti kama ungewasikiliza wanakanda ya ziwa mahitaji yao nadhani daraja hilo si kapaumbele kikubwa kwa sasa japo kwa baadae ni sawa kabisa.