Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Kwa sisis wafanya biashara hii itatusaidia sanaaa,,, tutaokoa Sana mda na kupunguza gharama
 
Unajua watu wengine hawajui faida yake na jinsi litakavojilipa.ikiwa siku mmoja litaingiza sh million 10 kwa siku,kwa mwaka ni siku 365 mara 10,000,000=3,650,000,000 ni Trilion 3.65 kama mapato ya nchi kwa miezi 3.

Basi kwa mapato ya daraja hili miaka 50 litaweza kujenga madaraja nchi nzima bila kutegemea serikali.
Hiyo milioni 10 kwa siku muitoe wapi? Emb acha upuuzi bwana!
 
CCM ni kama malaya ambaye tayari ameshavua nguo,kilichobaki tu ni sisi wananchi Tarehe 28 oktoba tuwachomeke Dudu wakaendelee na biashara zao za Mayanga construction.
 
Hiyo milioni 10 kwa siku muitoe wapi? Emb acha upuuzi bwana!
"The 180-tonne capacity bridge will allow 1600 vehicles to pass at a time. According to Chief Executive Officer of the Tanzania National Roads Agency (TANROADS), Engineer Patrick Mfugale, the bridge will be connected to a 34-kilometre road, with 28.4 metres wide from Mwanza. This will result to Mwanza city being a commercial hub in the Lake zone."

Daraja hili ni 2 ways traffick kuingiza wastani wa shilingi elfu sita na nusu kwa saa wala si tatizo.
Likishakamilika itakuwa short cut ya kuunganisha Kenya kupitia Mwanza kwenda/kwenda Burundi,Rwanda,Uganda,na DRC mashariki.
Pia ni short cut ya kusunguka kanda ya ziwa kwa kutokea/kwenda Mara kupitia Mwanza kwenda mikoa ilio magharibi ya ziwa.
 
Hapa ndipo daraja la Tshs bilioni 700, fedha ambazo hata hazikujadiliwa na bunge zinatumika. Eneo ni Kigongo-Busisi. Kwakweli Bunge la Ndugai litajibu haya mbele za Mungu!

View attachment 1570153
Nawaza tu bilioni 700 Tshs ambazo ni hela nyingi sana yani hata Richmond haioni nusu yake. Kama zingetumika kwa mtu kuona mbali. Kuliko kujenga hilo daraja litakalopitisha Hiace na mbaya zaidi kama tozo zitakuwa kubwa maana hili eneo lina watu wa kipato cha chini sana basi wakaamua kuachana na kulitumia wakaendelea na usafiri wao wa feri.

Embu tuangalie kama tungewaza vyema kwa hii bilioni 700
1. Tungechukua tu hapo kidogo tukawanunulia feri za kisasa.
2. Tukatumia hapo fedha nyingine kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo kama kuwapa mikopo yenye riba nafuu kisha mzunguko wao wa hela ukawa mkubwa. Yani kiufupi tungefanya mambo mengine mengi sana na hii hela! Ila kwa kuzitumia kwenye huu mradi ni HAPANA!

Yani Magufuli alifanya tu ziara hapo akakumbuka kuwa alikuwa anachunga ng'ombe eneo hilo basi hapo hapo akaamua lijengwe daraja na tena akatamka kuwa wajenge chap chap maana kama atakuja Rais mwingine ataufuta huo mradi! Kumbe hata yeye akilini mwake anajua kuwa ni mradi wa hovyo kupindukia!

Naumia maana gharama za mradi huu unazidi ule wa Kigamboni ambao walau ulikuwa na maana ingawa nao ulishavurugwa vurugwa na kweli fedha zinatumika isivyo kabisa!
Unasumbuliwa na wivu na choyo. Na usipobadilika vitu hivyo viwili vitakupa shida sana.
 
yani wote mliotowa mawazo humu, endapo serikali ya magufuli ingefanyia mawazo hayo mlioyatowa bado yangekuja mawazo mengne tena, istoshe mngezema ajenge daraja kuliko kutoa mikopo prngne isirete faida na hizo ferry pengne zinahitaji ukalabat kila baada ya mda, tumien akili daraja ni miaka ming sana tutakusanya pesa pale kuliko hiyo mikopo kukopesha watu na kununua ferry za kisasa ambazo zinatakiwa malekebisho ya kila baada ya mda.
 
Hivi ni kwa nn jamaa anapenda kuwaalika madikteta tu tena kipindi hiki cha uchaguzi?🤔🤔
Zaidi ya hilo nasikia museven asili yake ni mhutu..... 😒😒

Tuendelee kujiuliza pamoja👍👍
 
Hivi ni kwa nn jamaa anapenda kuwaalika madikteta tu tena kipindi hiki cha uchaguzi?[emoji848][emoji848]
Zaidi ya hilo nasikia museven asili yake ni mhutu..... [emoji19][emoji19]

Tuendelee kujiuliza pamoja[emoji106][emoji106]
Kumbe huyo Rais mpya wa Burundi ni dikiteta?
 
Unajua watu wengine hawajui faida yake na jinsi litakavojilipa.ikiwa siku mmoja litaingiza sh million 10 kwa siku,kwa mwaka ni siku 365 mara 10,000,000=3,650,000,000 ni Trilion 3.65 kama mapato ya nchi kwa miezi 3.

Basi kwa mapato ya daraja hili miaka 50 litaweza kujenga madaraja nchi nzima bila kutegemea serikali.
Rudi shuleni kwa mwalimu wako wa hesabu,akakufunze upya
 
Tumeni picha basi tulieone

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app
Tuko hapo mkuu
IMG-20200916-WA0052.jpg
 
Hapa ndipo daraja la Tshs bilioni 700, fedha ambazo hata hazikujadiliwa na bunge zinatumika. Eneo ni Kigongo-Busisi. Kwakweli Bunge la Ndugai litajibu haya mbele za Mungu!

View attachment 1570153
Nawaza tu bilioni 700 Tshs ambazo ni hela nyingi sana yani hata Richmond haioni nusu yake. Kama zingetumika kwa mtu kuona mbali. Kuliko kujenga hilo daraja litakalopitisha Hiace na mbaya zaidi kama tozo zitakuwa kubwa maana hili eneo lina watu wa kipato cha chini sana basi wakaamua kuachana na kulitumia wakaendelea na usafiri wao wa feri.

Embu tuangalie kama tungewaza vyema kwa hii bilioni 700
1. Tungechukua tu hapo kidogo tukawanunulia feri za kisasa.
2. Tukatumia hapo fedha nyingine kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo kama kuwapa mikopo yenye riba nafuu kisha mzunguko wao wa hela ukawa mkubwa. Yani kiufupi tungefanya mambo mengine mengi sana na hii hela! Ila kwa kuzitumia kwenye huu mradi ni HAPANA!

Yani Magufuli alifanya tu ziara hapo akakumbuka kuwa alikuwa anachunga ng'ombe eneo hilo basi hapo hapo akaamua lijengwe daraja na tena akatamka kuwa wajenge chap chap maana kama atakuja Rais mwingine ataufuta huo mradi! Kumbe hata yeye akilini mwake anajua kuwa ni mradi wa hovyo kupindukia!

Naumia maana gharama za mradi huu unazidi ule wa Kigamboni ambao walau ulikuwa na maana ingawa nao ulishavurugwa vurugwa na kweli fedha zinatumika isivyo kabisa!
Nimejiuliza kwa nini akili yako kama binadamu ulifikia hatua ya kulinganisha ubora wa daraja na vivuko. Hebu muulize mtu aliyeshuhudia vifo vya watu kwenye kivuko cha Kigamboni miaka ya 80, wakati tukiwa na waziri bwege kabisa wa ujenzi, Mustafa Nyang'anyi. Linganisha maisha ya watu wakati wa MV Bukoba wakati mwingine pia tulipoonesha ubwege na udhaifu kwenye miundombinu ya majini.
 
Daraja hili ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni jambo la upendeleo. Umbali unaopunguzwa kwa wanufaika ni mdogo sana kulinganisha na sehemu kama Kigoma kutoka Nyakanazi!!

Uwanja wa Chato nao ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Uwanja huo ungejengwa Dodoma au kuimarisha usafiri wa umma wa abiria wa Dodoma.
 
Uwanja wa Ndege wa Chato hauna tija ni kweli JPM alikosea ni miss allocation of public funds kwa sababu hata matumizi au return yake kwenye uchumi haionekani na haitaonekana leo. Daraja kwa mtu aliyewahi pita njia hiyo ataelewa umuhimu wa Daraja. Faida zake kiuchumi si kwa ajili ya Mwanza na Geita.
 
Soma post yangu vzuri...i said km watu wa kigoma na katavi km hatawatutumia hicho kivuko Cha Busisi then alternative yao ni kupitia Tabora...and now niongezee alternative nyingine watumie ya Nyakanazi kahama(hapa wanaweza kurudi tena Geita,Sengerema,busisi then Mwanza) or waendele shinyanga then Mwanza...of which bado ni mbali ukilinganisha na kupitia Geita, Busisi then Mwanza...
Katika alternatives there should be the best alternative. Nikufahamishe tu kuwa njia rahisi kwa Katavi na Kigoma kwenda Mwanza ni kupitia Tabora-Igunga-Tinde- Shy-Mwanza. Hiyo ya kupitia darajani ni usumbufu.

Vv
 
Sasa ngoja hilo daraja likamilike uone watakaopita hapo kama watakuwa wengi kuzidi feri. Hivi unajua kurudisha bilioni 700 wewe! Hizo hela ni nyingi sana kwa kuelekeza kwenye mradi kama ule. Anyway ila Jiulize kwanini hata yeye Magufuli anahisi alifanya kitu kisicho na tija hadi anahimiza waharakishe ili Rais mwingine asije akaufuta huo mradi.

Mkuu sidhani kama there is any need ya hizo pesa kuludishwa kwa serikali, kwa sababu ni pesa zetu Wananchi za kodi tunazolipa ili serikali iweze Kutufanyia maendeleo

huko majuu na nchi kama Hong Kong has a long history as a tax-free city,kwa hivyo madaraja yote wananchi wanalipia ili serikali iweze kuludisha pesa zake , lakini kwa huku kwetu Tanzania tunastaili kupata maendeleo bila ya serikali kuangalia faida kwa Sababu tunalipishwa kodi
 
Back
Top Bottom