Bado ni baba yangu daima!!

Bado ni baba yangu daima!!

Ludoby

Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
37
Reaction score
55
Katika maisha yapo mengi ya kujifunza kila uchao. Ni ijumaa moja napata rafiki kupitia instagram ambae ni rafiki wa rafiki yangu mkubwa na kwa kuona kwamba mimi ni rafiki wa rafiki yake pia anakua nwepesi katika kujibu na kutoa mawasiliano ya simu.

Sio kitu chepesi kwa upande wangu kutoa nawasiliano tena kwa wale wa mtandaoni ninajiulizaga sana ili kujihakikishia lengo la mtu kuchat na mimi katika mtandao mana dunia nayo yaenda kasi sana. Aliponipa namba mimi najifanya kama sijaiona na kuendelea kumfahamu zaidi hata kama anahusiana na rafiki yangu.

Binafsi sipendi sana kua na urafiki n marafiki wa marafiki zangu maana mara nyingi hutokea kuhamisha maneno hasa katika story za hapa n pale hata ziwe za kawaida. Basi vipimo vinaenda kusema huyu ni mtu mwema.

Huwezi amin siku hiyo hiyo ananiambia kuhusu kuugua kiharusi baba yake mzazi na mama yake wa kambo kuondoka na yeye pekee ndio anamhudumia baba yake. Ni kipindi kigumu anachopitia lakin sasa imembidi azoee tu ili maisha ya ende.

Mimi naingiwa na tamaa ya kumuona baba yake macho kwa macho maana wote tupo mkoa mmoja japo ni kuna kaumbali kidogo naenda nakutana na tabasamu la nguvu kutoka kwa baba akiwa na furaha nyingi sana.

Ndipo naona maongezi yaliyochangamka kati ya baba na mtoto nafurahi kwa kweli kakutana na mtu ninaependa story ai anafurahi sana. Na kucheka sana badae huyu rafiki ananiuliza umeongea nini na baba nmefirahi sana kuona anacheka sio kawaida kucheka kwa nguvu hivo. Namjibu nmempigia story ambayo nmekutana nayo katika daladala siku iliyopita.

Naona upendo wa baba na mtoto wake ambao ni mkubwa na mzuri sana sana. Ndipo moja ya majibu yake yanifurahisha na kunisukuma kuandika hili bado ni baba yangu daima. HOLLAAAA TO U KAKA.
 
Back
Top Bottom