Bado sehemu kubwa ya watu wetu wamenga'ng'ania vijiji kichwani mwao (waporipori)

Bado sehemu kubwa ya watu wetu wamenga'ng'ania vijiji kichwani mwao (waporipori)

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Wanasema unaweza ukamtoa mtu kijijini lakini ukashindwa kutoa kijiji kichwani mwake

Maana yake nini, watu wetu wengi bado ni washamba sana (wapori-porii), bado wanatambaa na mawazo ya kale vichwani mwao.

Haijalishi huyo mtu amesoma shule mpaka levels gani, au amekuwa exposed kiasi gani au ameishi mjini kwa muda gani. Japo saa nyingine watu wanadhani kuzaliwa tu mjini peke yake ni elimu kubwa au kinga ya ushamba.

Hapa sina nia ya kumsema mwendazake na genge lake (sukuma gang) au watu wa mikoani, la khasha, hii ni kwetu sote, ata wa mjini.

Wanafanya matendo au wanatekeleza mila na tamaduni bila kujali athari zake au kuhoji uhalali wake, faida zake na relevance yake katika maisha ya sasa. Wengi ni watu walio kariri kwamba yale yote ya vijijini kwao ndiyo sahihi bila kuzingatia kwamba dunia inakwenda kasi sana

Ninatoa mifano midogo katika haya yanayofanyika:

1. Kusalimia salimia watu hovyo;
2. Kulaumu watu wengine wasipo shiriki misiba au sherehe:
3. Ku force force kujuana juana tunakoishi au mitaaini kwenye hustle nakasirika zaidi nikiwa safarini, sikujui hunijui unaniongelesha nini?;
4. Kulamba viatu vya viongozi na watu matajiri au wenye umaarufu (uchawa)
5; Kusengenya watu makazini, majumbani, kwenye nyumba za ibada na kwenye siasa;
6. Ulozi, kuloga watu wasifanikiwe au kujihusisha na ushirikina na kufanya matambiko;
7. Kufuatilia mambo ya watu wengine, udaku na umbeya mambo ya kishamba sana;
8. Kuongea ongea kwa nguvu kwenye public places, hii ikiwa ni,pamoja na kuongea kwa nguvu ukitumia simu na kujiongelesha mambo yako au kuwasha simu na kusikiliza audio au kutazama video zenye sauti kali kwenye hadhara ya watu, huu ni ushamba mwingi sana;
9. Kuwasha maredio kwa sauti kubwa, majumbani, kwenye gari au boda boda, au kwenye pubs au bar huu ni ukenge sana;
10 Kutembea na wake au wapenzi wa watu ili usifiwe, huo ni ukenge mwingi sana;
11. Code za kilokole, kuvaa masuruali ya vitambaa yenye celebration au turn-ups na mashati oversize, yaani ni ushamba mwingi sana;
12 Kuwa na chuki na watu waliofanikiwa au kabila fulani au watu wa kanda fulani hizo ni code za kishamba sana;
13 Kukaa kwenye fast lane (upande wa kulia wa barabaara huku unaendesha gari taratibu na unaongea na simu ni ushamba mwingi sana;
14 Kupiga piga honi nyingi barabarani bila sababu za msingi au kupiga honi getini kwako ili ufunguliwe ni ushamba sana(weka motor kwenye geti yako acha kusumbua majirani);
15 Ku park hovyo gari barabarani kama mtu wa dala dala ni ushamba mwingi sana.

Kuna mambo mengi sana ya kijinga zaidi haya bado yanendelea kufanywa na kuaminiwa na watu ambao ukiwaona utashangaa.

Kuna baadhi ya nyuzi nimejaribu kutoa humu JF nakupata uhalisia wa watu wetu na mitazamo yao na hiili limenifanya nitafakari uzi huu.

Hii ni sehemu ndogo tu ya reflection ya uhalisia wa watu wetu unaojitokeza kwenye comments zao

Hoja hupingwa na hoja iliyo bora na si vinginevyo
 
Wanasema unaweza ukamtoa mtu kijijini lakini ukashindwa kutoa kijiji kichwani mwake

Maana yake nini, watu wetu wengi bado ni washamba sana (wapori-porii), bado wanatambaa na mawazo ya kale vichwani mwao...
Umechanganya viti vingi kwenye sehemu moja........sio kua na ukijiji au uporini hapana, kuna ujinga, ulimbukeni, uchawa, ushamba na umasikini hivyo vyote huleta tabia ya ajabu katika jamii zetu.
 
Nakubali, lakini sehemu kubwa still ni reflection ya background ya mtu hukoalipotoka
Hapana ebu ni kupe mfano, jana Raisi wakati wa kupokea ndege ya mizigo alikaa kwenye kiti cha pilot wandege eti wanapokea ndege, haliakua yeye sio pilot na hana ujuzi huo..........sasa huo ni ushamba au limbukeni?
 
Hapana ebu ni kupe mfano, jana Raisi wakati wa kupokea ndege ya mizigo alikaa kwenye kiti cha pilot wandege eti wanapokea ndege, haliakua yeye sio pilot na hana ujuzi huo. sasa huo ni ushamba au limbukeni?
Naomba nisitoe comment kwenye hili. Tuna safari ndefu, washauri wanapaswa ku benchmark yale wanayoshauri
 
Hapana ebu ni kupe mfano, jana Raisi wakati wa kupokea ndege ya mizigo alikaa kwenye kiti cha pilot wandege eti wanapokea ndege, haliakua yeye sio pilot na hana ujuzi huo..........sasa huo ni ushamba au limbukeni?
mwulize mamako, alivyokaa yule mshamba wenu ulijiuliza? Kwa akili ya hovyo hivyo hata mtoto wako huwezi kumsaidia
 
Huu ni Uwendawazimu huu.

Hakuna anayetaka mambo ya Kizungu. Hatahivyo Mnalazimisha sana uongo aisee
Neanderthals, please!😌
e4a13a935e607fa4f23dfb80ec995d36.jpg

Neanderthal_1-768x586.jpg

A tribe of Neanderthals in France
29269a9afe62e76c85b16f916bfe2998.jpg

Courtesy of Pininterest.
 
Lazima uncomment wewe ndo ulileta mada kutusema sisi tulio kulia kijijini au polini, sasa Raisi wetu hajawahi kukaa kijijini au polini ni mtu wa mijii mikuu tu?
Raisi ni taasisi siyo mtu binafsi, pengine amezungukwa na wapori-pori wanaompa code za kishamba. Na hili mkaliangalie
 
Kikubwa serikali iwekeze katika kuwapa elimu raia wote angalau Kila raia awe amemaliza chuo kikuu. Bila hivyo ujinga na ushamba hautaisha hata Yesu akikuja Leo .
Hakika, Lowassa alisema, elimu, elimu,elimu
 
Raisi ni taasisi siyo mtu binafsi, pengine amezungukwa na wapori-pori wanaompa code za kishamba. Na hili mkaliangalie
Aaah hapo tuambie alie mzunguka wapoli na kumshauri afanye mambo ya kishamba ni nani hapo unapo ona? Wengi hapo ni mission town tu.
 
Aaah hapo tuambie alie mzunguka wapoli na kumshauri afanye mambo ya kishamba ni nani hapo unapo ona? Wengi hapo ni mission town tu.
Mbona wapori-pori ni wengi na makaunda suti yao ya kishamba kama watu wa magerji
 
Kikubwa serikali iwekeze katika kuwapa elimu raia wote angalau Kila raia awe amemaliza chuo kikuu. Bila hivyo ujinga na ushamba hautaisha hata Yesu akikuja Leo .
Kigezo cha kupata degree haimuondoleee mtu ushamba kabisa hamna watu washamba kama wasomi siku hixi wakipata pesa au vyeo, mwendazake alikua na PhD ila alikua bonge la mshamba.....
 
Kigezo cha kupata degree haimuondoleee mtu ushamba kabisa hamna watu washamba kama wasomi siku hixi wakipata pesa au vyeo, mwendazake alikua na PhD ila alikua bonge la mshamba.....
Ni kweli,,ila angalau ndiyo sehemu ya kuanzia
 
Back
Top Bottom