Umepiga story lakini kuna mahali umetoa jibu sahihi bila kujua, Hapo uliposema...
qoute:
Baada ya reli yetu kuwa chakavu, uwezo wake wa kusafirisha mizigo ulipungua sana, kasi ilipungua hadi kufikia chini ya 30Km/ h. Trains zilikua zinaangua Mara kwa Mara kutokana na uchakavu wa vyuma vya reli na trains zenyewe, ilihitajika pesa nyingi ili kuikarabati"
endQuote:
Unajua ile methali ya kati ya yai na kuku nani ndo alikua wa kwanza?????
Reli iliochakaa hadi kufa miaka 10 iliopita mnaifufua tena, Swali kuu ni,
ni reli ilichakaa ndo mizigo ikapungua au ni mizigo ilipungua ndo reli ikachakaa???? manake kama reli ingekua inatengeneza faida kweli, ingekua waliweza kugaramia regular maintenance ambayo ingefanya hio reli isichakae kiasi hicho!!!
FYI reli ya meter guage huku Kenya ina miaka 121 na bado hua inatumika hadi wa leo kupeleka Magadi ash hadi Mombasa, Upande wa Kutoka Nairobi kuelekea kampala ndo hio reli imekufa kabisa.....
Kwahivyo hapo unafaa uwe makini kujua kwanini Central rail ilikufa, manake kama ilikua inatengeneza faida kubwa enzi zile, wangekua na uwezo wa kufanya regular maintenance kila mwaka na ingekua haikuchakaa hadi kufa. Sahii mnafufua reli ambayo ilikosa biashara enzi hizo na mnatarajia eti itagonga ndipo!!!