Kafrican
JF-Expert Member
- Jan 26, 2015
- 7,251
- 7,037
Ningependa kushirikisha mawazo yangu ili kuibua mjadala kuhusu bandari ya Kisumu ambayo punde tu itakusanya marais 5 kuizindua. Nimefikiria sana kuhusu hii bandari umuhimu wake kwa sasa, bado sijapata muunganiko wake.
Bandari ya Kisumu iliacha kufanyakazi zaidi ya miaka 12 iliyopita, sababu kubwa iliyosababisha kudorora pamoja na mambo menigine, ni kutokana na wafanyabiashara wengi wa Uganda kutumia usafiri wa reli na barabara, ambao ukipakia "cargo", hazishushwi hadi Uganda, yaani gharama za upakiaji na ushushaji ni Mara mbili tu.
Kwasababu hiyo, reli ya kuelekea Kisumu ilikosa mizigo na kuachwa ikajifia kabisa, kutokana na naekezo ya James Macharia, reli kuelekea Kisumu inahitaji kujengwa upya sio kukarabatiwa. Swali ninalojiuliza, kama hakuna reli inayoelekea Kisumu, je bandari ya Kisumu inaungana vipi na Mombasa, au Kisumu Port haitegemei mizigo ya Uganda na DRC?.
Bila shaka "Kisumu port" lengo lake ni hizi nchi za Uganda na DRC, je itatumia mfumo upi wa usafirishaji ambao utakua ni bei nafuu na ni haraka. Tumeambiwa bandari ya Mwanza itatumia mfumo wa "Railway - Marine - Railway", ambao ni " integrated ", yaani mabehewa hayashushi mizigo kutoka Dar- hadi Kampala au Jinja Uganda, Kisumu port itatumia mfumo upi kama hakuna reli inayofika Kisumu?.
Alafu haka kabandari kanakupatia tabu sana, ni ukarabati unafanyiwa tu, gharama yake ni only $30m
Shida ni kwamba unajifanya kuuliza maswali lakini ushafunga akili na kujiamulia yako bila hata kungoja jibu. Dakika chache baada ya kuanzisha hii mada ukatoa hii comment
Kenya na wakenya kwa ujumla, wanauwezo mdogo sana wa kufikiria mambo makubwa, uwezo wao wa kufikiria ni " below average". Subiri usikie majibu watakayotoa katika huu uzi ndio utagundua ninachosema.
Sasa wewe ni mtu unafaa kujibiwa lolote kweli kama ulishajiamulia na haya ndo maoni yako????
Unafaa ujiulize kama tuna uwezo mdogo wa kufikiria kwa mambo makubwa, iweje sisi ndo tunapokea mizigo mingi kuwashinda? inakuaje sisi ndo tunaongoza kwa logistics?, inakuaje sisi ndo tuko na airport kubwa.. etc..... Nyinyi mlio na akili kubwa mbona tume wawacha mbali sana ikijja kwa haya mambo???
World bank ilishawaambia bandari yenu kuu iko inneficient , yaani hata bila kutumia hela zozote kufanya expansion, mkitia bidii na kufanya bandari yenu iwe efficient kama ya Mombasa, Tanzania itaongeza $1.8Billion kwa GDP kila mwaka
Badala ya kutia juhudi kuleta hii efficiency kwa bandari yenu, mmenda kupanua bandari zenu zote ilhalii hamjafika maximum potential ya bandari mlizo nazo, sasa ni nani ndo ana uwezo mdogo wa kufikiria??
Alafu hapo unaposema sababu ya Bandari ya Kisumu kufa ni ni kutokana na wafanyabiashara wengi wa Uganda kutumia usafiri wa reli na barabara.... Ulikua unaelewa unachosema? Ni reli gani hio ulikua unaongelea ilouwa bandari ya Kisumu? Reli ya meter guage ilijengwa hadi Uganda, wakati huohuo bado pia ilifika Kisumu.. Kumbuka wakati ule Kenya ndo ilikua na meli kubwa zaidi hapo L.Victoria, wakati huo huo bado reli ya kuelekea Uganda ilikua inafanya kazi.... Kwahivyo kulikuana route zaidi ya moja kwenda Uganda...
Hapo unaposema "Kwasababu hiyo, reli ya kuelekea Kisumu ilikosa mizigo na kuachwa ikajifia kabisa" Hebu nikuulize, Kama Bandari ya Kisumu ilikosa kazi kwasababu ya Reli na barabara ya kuelekea Uganda.... Nini ilifanya reli ya Central-line ya kutoka Dar-Mwanza kufa??? kulingana na maelezo yako, si sababu itakua ni ile ile???? Northern-Corridor ya Mombasa-Kampala ndo ilichukua mizigo yote ya kuelekea Uganda kusababisha reli yenu ya central line na bandari ya Mwanza kufa kupindukia....
Sasa ni nini kimegeuka??? Ni nini kimewasababisha kufufua safari za Mwanza-Port-bell wakati Kenya ilisha wapiga kichapo enzi zile? Sasa naona mmerudi tena kwa Round two tuwanyorroshe vizuri ehh?
Alafu huo mfumo wa "Railway - Marine - Railway" jina lengine la huo mfumo ni ro-ro ambayo inamaanisha Roll-on/roll-off ships .....
Hii ndo definition ya ro-ro
Roll-on/roll-off
Kwahivyo huo mfumo una support utumiaji wa rail-marine-rail, road-marine-road, Trailer-ship-Tailer etc, Usifikirie ni reli tu, hata malori yanaweza faidika sana, Bara bara ya kuelekea kampala ni ndefu, lori likipita na Kisumu hadi port bell itakua ni shortcut kubwa sana.....(RORO or ro-ro) ships are ferries designed to carry wheeled cargo, such as cars, trucks, semi-trailer trucks, trailers, and railroad cars, that are driven on and off the ship on their own wheels or using a platform vehicle, such as a self-propelled modular transporter.
Enzi zile kisumu ilikua na viwanda vingi sana, viwanda vilivyokua vinatengeneza bidhaa tofauti, mizigo ya Kutoka Mombasa ilikua inapita na reli hadi kampala, lakini mbali na hilo, mji wa Kisumu wenyewe ulikua unazalisha bidhaa zake ambazo zinasafirishwa hadi Mwanza, Bukoba, Port-bell etc, na kutokana na hizo biashara, pia watu walikua wanasafiri sana ili kufanya biashara.....
MV Uhuru enzi hizo, Ilikua inabeba Rail wagon lakini pia magari yaliobeba mizigo
Hata kama SGR itafika kisumu na Kampala, inatajiwa kubeba 40% ya mizigo yote, hio 60% bado itapitia barabara, kwanini isipitia na L.Victoria ambayo itakua ni cheaper kuliko kuenda na barabara??
Unafaa ujue viwanda vya Kisumu vilipokufa, bandari nayo iliacha kutumika na Kisumu ikaacha kua logistical hub, Hio central corridor ya Tanzania ilikua imeshakufa kitambo hata kuliko meter guage ya Kenya...
Alafu pia unafaa ujue Port inayopanuliwa na serekali ni old port , hii ni tofauti na new port itakayo jengwa na SGR
The new port is expected to be constructed near Korando. However, ongoing expansion of the old port may see the Government use the funds to improve the existing port.
Projects that could propel Kisumu as EAC's commercial hub in 2019
The investments are being funded by the national government.
Usifikirie tu mizigo kutoka nje kuelekea Uganda na DRC, fikiria Viwanda kati ya Mwanza, Jinja, Port-Bell, Kisumu..... Hii ni miji ambayo ikifanya biashara kati ya hii miji itaboresha maisha ya watu wanaozunguka L.Victoria, hio haiwezi fanyika kama hakuna miundombinu kabambe... Hatuwezi kua na the biggest lake in Africa alafu tumekaa tu hata hatuitumiii....
Kwahivyo acha kua kama mwafrika mnafik na mchawi ambae hataki kuona jirani yake anajenga nyumba kwasababu anataka yeye pekee ndo awe anajenga nyumba kwa kijiji... Kisumu port ikifanya kazi hakuna litakalo zuia Tanzania kuuzia bidhaa zake kwa wakaazi wa Kisumu, Eldoret, Bungoma kupitia Mwanza..
Kwa mfano, Coca cola iko na Kiwanda cha kutengeneza Chupa hapo Kisumu, Imagine kaakue na Kiwanda cha kutengeneza Soda kule Mwanza alafu vifuniko vya Soda vitoke Kampala...
Kampuni ya EABL ilifungua kiwanda cha $150m cha kutengeneza bia hapo Kisumu, wanahitaji Sorghum kwa wingi, Kama wakulima wa western Kenya watashindwa kutosheleza, wakulima wa miji ya L.Vitoria wanaweza kuanza kujaza hio order... Hayo ndo mawazo unafaa uwe nayo akilini, si kuwa na fikra za Kimaskini..