Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Kwa lipi? Je zilikuwa zinapaa? Au mwisho wa safari alikuwa anarudisha nauli? Kipi kilikuwa ni special ambacho mabus mengine hayakifanyi?
Alikuwa na huduma ya "loyal customers" au twaweza ita "frequent traveller service".
Yaani ukisafiri na bus zake mara kadhaa kwa kipindi cha muda fulani, unapata tiketi ya bure.
 
Biashara ya mabasi ni kama biashara ya ndege ni pasua kichwa. Ni mwendo wa hasara tu.

Makampuni ya mabasi kila siku yanakuja na kufa, ambayo yanadumu kiasi ni yale ambayo mmiliki anaingiza pesa kwenye mabasi toka kwenye vyanzo vingine ambapo napo eventually hufa natural death.

Same applies kwa makampuni ya ndege, sio bahati mbaya makampuni makubwa ya ndege ni state owned from Qatar, emirates, KLM, Ethiopia nk. Nchi zina-inject pesa kuyaendesha toka kwenye vyanzo vingine ila yenyewe kama yenyewe hayaingiza faida yeyote. Serikali zikiacha kuyaruzuku yanajifia faster. Biashara ya usafirishaji isikie tu.
 
Kumbe umezeeka sana ila bado unafanya uchimvi wa wakora jukwaani !
 
Kuna bus ni mbovu sana

Kuna bus moja huwa laanzia sehemu hadi nilifike mkoa ulipo seat yako ishakatiwa mara mbili unapanda unakuta mtu kakaa huwa sielewagi unamuuliza anakwambia Ana ticket mnamuita konda sasa
 
Have you ever feel the power of f360 going uphill?
 
Siyo mabenki

Wakubwa waliingiza mabasi yao wakawa wanajaza diesel ya Serikali

Route za wakubwa:

Dar - Nairobi

Dar - Kampala

Dar - Mombasa

Dar - Tunduma

Dar - Kyela
Sasa yakafa je? Eleza hapa yalikufa je?
 
Nakazia aisee nimezipanda sana enz za miaka ya 2003 iringa_ dar,tena zilikua zinatufata shule kabisa boarding ruaha sec iringa ,dar_ Nairobi to Musoma,zilikua ndege za chini zile, very express ,miss those days !!time flies
 
Royal?
Hakuna kampuni bora tena.
Ukaribu wa kuiga.
Huduma za kuunga unga tu.
Ubabaishaji mwingi sana
 
Miaka hyo hakukua na smartphone wal wifi
Wewe ndio haukuwa na smartphone, mimi nilikuwa na Blackberry curve.

Kama umeanza kutumia smartphone kizazi cha Tecno ni wewe, kipindi hicho internet wireless inaitwa WLAN, nimetumia sana Kilimanjaro hotel free wireless internet.
 
Mwenyekiti wako hapo Ufipa alikuwa Dj wetu kwenye hotel ya babake pale Posta

Wewe ulikuwa bado uko viunoni
Hotel ya Baba yake ilikuwa mtaa gani na ilikuwa inaitwaje?

Ulikuwa kijijini kwenu unalima Uyoga, tueleze Hotel ya baba yake Mbowe ilikuwa wapi?
 
Alitengeneza reputation yake nzuri ila msipate upofu Bado Kuna kampuni zinatoa service nzuri za mabasi kushinda hizo gari mseme mmezimiss hizo basi tu.

Ile quality ya service bado haijafikiwa. Wanajitahidi lakini ile kampuni ilikua na huduma nzuri sana, mabasi mazuri nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…