Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Kila jambo na wakati wake.nimepanda scandinavia zaidi ya mara kumi,miaka 90 mwishoni hadi 2000s.

Huduma zilikuwa nzuri kwa wakati ule,pia aina ya washindani wake wakati ule walikuwa wa kawaida.

Miaka ile soda ilikuwa " kitu cha maana" au video ilikuwa kitu adimu,kwahiyo ukihudumiwa hayo mambo unajiona mfalme,nilikuwa natunza tiketi za ukumbusho.

Miaka ile hata magari binafsi yalikuwa ya kawaida,corola,cresta,datsun n.k

Saivi mambo yamebadilika kila kitu kimekuwa cha kawaida,kwamba mtu unaweza kujitosheleza kwa kila kitu na kila siku kwenye maisha ya kawaida,kwahiyo unapokwenda kupanda basi unaona kila huduma ni ya kawaida hadi unaona kama ni usumbufu.

Haya ma yutong mazuri,yanajitosheleza kulingana na maisha ya sasa yalivyo.

Miaka ile ushamba ulikuwa mwingi ndio maana tulishoboka na hayo mabasi,lakini yalikuwa ya kawaida tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa alikuwa na route nyingi kutokana na bus alizokuwa nazo. Je service iliyokuwa inatolewa kipindi Cha safari ndani ya bus hakuna kampuni yoyote inaitoa Sasa.?
Kwasasa sio msafiri sana ila nahisi nacharo, ratco na shabiby luxury wanaweza wakawa na huduma nzuri kama scandinavia au hata zaidi
 
Mkuu hii mada ninakubaliana nawe 100%,Scandinavian Express ilikua super inakuondoa Dar 06:00am to Tunduma, saa 17:00ndani ya border, 20:00hrs from nakonde by 05:00am,ni good morning Lusaka Bus Terminal, hii bus ilikua hadi ndani ya zambia hakuna bus ilikua inaikamata(elewa buses zingine zilikua zinaondoka nakonde by 18:00!,lakini Kapiri Mposhi bus ya kwanza kupiga hodi pale ni Scandinavian iliyoondoka 20:00),salute salute kwa Scandinavian Express
...Na ilikuwa haikimbii Ovyo kama tunavyoona Sasa hivi! Kikubwa ni kuwa haisimami sima ovyo kuokoteza okoteza Abiria!
Niliwahi kutoka nayo Tanga on time tukiwa Abiria 17 TU! Na hatukusimama popote Hadi Dar!
 
...Na ilikuwa haikimbii Ovyo kama tunavyoona Sasa hivi! Kikubwa ni kuwa haisimami sima ovyo kuokoteza okoteza Abiria!
Niliwahi kutoka nayo Tanga on time tukiwa Abiria 17 TU! Na hatukusimama popote Hadi Dar!
Top class service
 
Akikujibu pls tag me, na atoe facts sio blah blah, Scandinavian Express walikua na top class systems ya tickets, top class boarding lounge, ALWAYS ON TIME,they never ever cancel a trip, well serviced buses, well trained staff,no RUSH njiani,mkisimama sehemu ya mapumziko it's more than 30mins,ndani y bus ni smile tupu, binafsi nilipenda bcs always no 1
....Walikuwa Mpaka na MainSpectaNjiani wanapanda manjiani kukagus Tiketi!
 
Kati ya yeye na dar ex Nani Bora Sasa ..huyo mnaemsifia gari zake ziliuzwa Kama nyanya
...We bwana inaelekea unataka Ubishi TU!... Scandnavia ilikuwa Bora Kwa Huduma Zake! Kufa ni Mambo ya Kibiahara TU lakini yalikuwa Bora kwenye HUDUMA!
 
Natumia sana usafiri wa mabasi, bado sijaona mbadala wa Scandinavian kwa kweli. Hawa akina Sauli, Shabiby, sijui ABC bado sana aisee.

Scandinavian ilikuwa bora kuanzia kwenye vyuma vyenyewe yaani Scania tupu hakuna Layland hadi kwenye huduma. Ligi ya sasa ni vyuma vya mchina aka kambi popote

Mungu wa mbinguni mbariki mzee Abdullah na Bob Said pale Iringa
Ina maana hujaiona reli ya kati?
 
Back
Top Bottom