Jamani mnabishana wakati tarehe husika inakuja kwanini tuandikie mate?
Madai ya wanaotaka kuandamana yanaweza kuwa ya haki au kinyume chake.Muhimu hapa ni kila mmoja anautashi wake ni mbaya Sana kutoa hoja kama vile wote tumekubaliana kuandamana au kutokuandamana.
Ni kweli nchi hii kwa muda mrefu kuna mambo hayaendi vizuri na sababu kubwa ni kutokana na kuwa asilimia 90 ya watu wake hawana uzalendo Sasa swali linalotusumbua tukiandamana baadhi ya waandamanaji watapata shida na mengine yote yatakayotokea tutakwepa kuwaweka hawa asilimia 90 ya wachumia tumbo?
Tutapigana Sawa na yeyote anaweza kushinda Je,hiki kidogo tulicho nacho kitapotea au tutakilinda?
Kwakuwa dhuruma,ufisadi na ubadhilifu unatamalaki kila sector ni vema tukatafuta njia ya kupunguza watu wasio na uzalendo kwa nchi kutoka asilia 90 mpaka 10 na Wala haiitaji maandamano tunachotakiwa ni kuamua kufichua maovu yote kwa KUTUMIA nguvu ileile inayofanana na Maandamano tuachane na kusubiri Waziri mkuu KWENDA kufichua uozo.