Bado unaamini hii kesi ni ya Ugaidi?

Bado unaamini hii kesi ni ya Ugaidi?

Hangaya anatia aibu na ile miwani yake kama bundi
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Komenti za aina hii ndio zimemkatisha tamaa kabisa na kuishia kusema "kama humpendi chifu basi panda nchi yako"
 
Hivi ili kesi iwe ya kigaidi inatakiwa kuwepo na vitu gani ili mahakama ikutie hatiani? Mbona kila ushahidi hueleweki?

KULIPUA VITUO VYA MAFUTA
Sasa mbona Polisi au mashahidi wa Serikali wenyewe wanakiri kua hawakuwahi kuwakuta watuhumiwa na vilipuzi vyovyote yaani hata kiberiti?
Hapo bado itawatia hatiani kwa lipi?

KUPANGA MAGOGO BARABARANI
Hakuna shahidi upande wa jamuhuri tangu waanze kuhojiwa akaji na ushahidi wa gogo lililokatwa ,yaani hata msumeno au panga la kukatia magogo hayo. Wapeleke hata tawi la mti uliokatwa kwa ajili ya maandamano.

KUFANYA MAANDAMANO!
Mpaka sasa mashahidi waserikali hawajaonesha ni wapi maandamano yalipangiwa na uratibu wake ulikuwaje, maana kama ni mikoa ilitajwa ya Kwanza,Dar es salaam,Morogoro,Arusha na Mbeya ni lazima lingekuwepo na coordinators wa maandamano katika kila mkoa? Wenyeviti wa CHADEMA wa kanda na Mikoa Mbowe apange maandamano na walinzi wake wao wasijue?
Basi hawa Polisi walete hata video au picha za hawa magaidi wameketi mahali fulani wanapanga ugaidi?

Basi hata sms kwenye simu walizokamata zikionesha magaidi hawa wakipanga ugaidi wao au maandamano, si walihack mawasiliano yao mbona hakuna ujumbe wowote wenye njama za ugaidi? Yaani wao wana ushahidi wa miamala ya pesa tu ambazo pesa zenyewe haziwezi kusema zilikua za nini, tuseme ni za matumizi kawaida mtu kuwapa posho walinzi wake 😂😂

KUKUTWA NA SILAHA
Watuhumiwa wenyewe wanakana kukutwa Silaha,wanadai kua waliwekewa na ikizingatiwa mashahidi wanajichanganya kwenye ushahidi wao.

Hata kama silaha zingekuwa ni zao, hivi mlinzi hasa mtu ambaye alikuwa ni askari ni kitu cha ajabu? Tuseme silaha labda hazikusajiliwa kwa sababu ni za kihalifu, yaani Walinzi wa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani yaani VIP, KUB kwa miaka 15 atumie walinzi wenye silaha zisizosajiliwa?

KUHUSU KUMDHURU SABAYA
Yaani mtu ambaye mpaka sasa amefungwa miaka 30 kwa sababu ya Ujambazi hata kama ni wewe ni lazima ujihami naye, hatusemi kua Mbowe akijihami na Sabaya kwa vile alikuwa jambazi, laahasha, hakuna ushahidi wowote mpaka sasa toka kwa mashahidi wa Jamhuri kuonyesha kwamba kulikua na njama za kumdhuru Sabaya, kwanza kusikia neno Sabaya kwenye kesi hii ni nadra sana.
Lakini ingekuwa mimi ilikua lazima nijihami na jambazi hili aisee, kwani kuna tatizo kujihami na jambazi?

HITIMISHO
Mimi ningekuwa Jaji ningemuita DPP niwashauri wakajipange upya au waifute kesi hii kuondoa aibu ya taifa waache kupoteza rasilimali za taifa maana ni upotezaji wa muda tu na pesa zinaliwa bure, ni wazi mbele za Mungu siyo kesi ya kigaidi hii.Hata kesi ya Kibaka au Jambazi haiwezi kuwa hivi.

Fundi Madirisha nahitimisha kwa kusema, tuzionee huruma rasilimali za taifa. Hizi pesa za kuendeshea kesi zinazoliwa bure kila siku kuwapanga mashahidi na kumlipa Jaji na watumishi wengine zingeenda kujenga shule.
Toka lini maandamano yakawa ni ugaidi. Only in Tanzania.
 
Wao hawategemei ushahidi wanategemea kumwelekeza jaji a hukumu mbowe
 
Hangaya anazidi kuaibika maana tayari alishautangaZia ulimwengu kwamba mwamba ni gaidi, wanachofanya ni kulazimisha ushahidi ili kuficha aibu
duuh katiba ndo kila kitu. Madaraka ya Rais ni makubwa kiasi anaingilia uhuru wa mihimili mingine bila kujali kabisa
 
Vipi kuhusu matukio yanayoendelea nchini hali yakuwa yupo jela?
Watu wanachinjwa kama kuku?watu wanauana kila uchwao?amani sio mpaka kuwe na vita mzee.View attachment 2091001
Hao hawawezi kujulikana walipo maana Polisi wetu wapo bize wamejifungia Gest na Mashahidi wa uongo wanawamezesha madesa ili wamfunge Mbowe,ndio maana wahalifu wanatamba tu mitaani
 
Hivi ili kesi iwe ya kigaidi inatakiwa kuwepo na vitu gani ili mahakama ikutie hatiani? Mbona kila ushahidi hueleweki?

KULIPUA VITUO VYA MAFUTA
Sasa mbona Polisi au mashahidi wa Serikali wenyewe wanakiri kua hawakuwahi kuwakuta watuhumiwa na vilipuzi vyovyote yaani hata kiberiti?
Hapo bado itawatia hatiani kwa lipi?

KUPANGA MAGOGO BARABARANI
Hakuna shahidi upande wa jamuhuri tangu waanze kuhojiwa akaji na ushahidi wa gogo lililokatwa ,yaani hata msumeno au panga la kukatia magogo hayo. Wapeleke hata tawi la mti uliokatwa kwa ajili ya maandamano.

KUFANYA MAANDAMANO!
Mpaka sasa mashahidi waserikali hawajaonesha ni wapi maandamano yalipangiwa na uratibu wake ulikuwaje, maana kama ni mikoa ilitajwa ya Kwanza,Dar es salaam,Morogoro,Arusha na Mbeya ni lazima lingekuwepo na coordinators wa maandamano katika kila mkoa? Wenyeviti wa CHADEMA wa kanda na Mikoa Mbowe apange maandamano na walinzi wake wao wasijue?
Basi hawa Polisi walete hata video au picha za hawa magaidi wameketi mahali fulani wanapanga ugaidi?

Basi hata sms kwenye simu walizokamata zikionesha magaidi hawa wakipanga ugaidi wao au maandamano, si walihack mawasiliano yao mbona hakuna ujumbe wowote wenye njama za ugaidi? Yaani wao wana ushahidi wa miamala ya pesa tu ambazo pesa zenyewe haziwezi kusema zilikua za nini, tuseme ni za matumizi kawaida mtu kuwapa posho walinzi wake 😂😂

KUKUTWA NA SILAHA
Watuhumiwa wenyewe wanakana kukutwa Silaha,wanadai kua waliwekewa na ikizingatiwa mashahidi wanajichanganya kwenye ushahidi wao.

Hata kama silaha zingekuwa ni zao, hivi mlinzi hasa mtu ambaye alikuwa ni askari ni kitu cha ajabu? Tuseme silaha labda hazikusajiliwa kwa sababu ni za kihalifu, yaani Walinzi wa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani yaani VIP, KUB kwa miaka 15 atumie walinzi wenye silaha zisizosajiliwa?

KUHUSU KUMDHURU SABAYA
Yaani mtu ambaye mpaka sasa amefungwa miaka 30 kwa sababu ya Ujambazi hata kama ni wewe ni lazima ujihami naye, hatusemi kua Mbowe akijihami na Sabaya kwa vile alikuwa jambazi, laahasha, hakuna ushahidi wowote mpaka sasa toka kwa mashahidi wa Jamhuri kuonyesha kwamba kulikua na njama za kumdhuru Sabaya, kwanza kusikia neno Sabaya kwenye kesi hii ni nadra sana.
Lakini ingekuwa mimi ilikua lazima nijihami na jambazi hili aisee, kwani kuna tatizo kujihami na jambazi?

HITIMISHO
Mimi ningekuwa Jaji ningemuita DPP niwashauri wakajipange upya au waifute kesi hii kuondoa aibu ya taifa waache kupoteza rasilimali za taifa maana ni upotezaji wa muda tu na pesa zinaliwa bure, ni wazi mbele za Mungu siyo kesi ya kigaidi hii.Hata kesi ya Kibaka au Jambazi haiwezi kuwa hivi.

Fundi Madirisha nahitimisha kwa kusema, tuzionee huruma rasilimali za taifa. Hizi pesa za kuendeshea kesi zinazoliwa bure kila siku kuwapanga mashahidi na kumlipa Jaji na watumishi wengine zingeenda kujenga shule.
Ushauri wako labda ukaupeleke nje ya nchi. Hii nchi hakuna .wenye akili za kukuelewa. Hasa wale wenye mamlaka.
 
Hao hawawezi kujulikana walipo maana Polisi wetu wapo bize wamejifungia Gest na Mashahidi wa uongo wanawamezesha madesa ili wamfunge Mbowe,ndio maana wahalifu wanatamba tu mitaani
Kweli. Januari 2022 pekee, kumetokea mauaji zaidi ya 10 yaliyotangazwa, huku tukio moja likiwa la polisi kumpora pesa kisha kuua polisi mmoja na raia mmoja.
 
Back
Top Bottom