Habari wadau, naomba msaada wenu kwa kitu kinachonichanganya kidogo. Nyumbani kwangu sijamaliza ujenzi so kwa suala la choo na bafu familia nzima tunatumia kile cha public. Hiki cha masters tayari wameshaweka matoleo ni kiasi tu cha kununua sinki na shower ila tangu mwaka jana mwishoni maji yanatokeo pale kwenye eneo litakapokaa choo chenyewe. Mwaka Jana yalikuwa maji ya kawaida tu hayana rangi wala harufu ila kuanzia mwaka huu yamekuwa na rangi nyeusi na yanatoa harufu japo si Kali
Hapo kutakuwa na shida gani? Wataalamu wa ujenzi, plumbing na wamiliki wa nyumba wenye uzoefu naomba mnisaidie nini cha kufanya. Asanteni
Hapo kutakuwa na shida gani? Wataalamu wa ujenzi, plumbing na wamiliki wa nyumba wenye uzoefu naomba mnisaidie nini cha kufanya. Asanteni