Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Hebu maliza hiyo habari. Baada ya kukuta geti limefungwa wamechukua hatua gani? Kwa hiyo mazishi hayakufanyika?
walivunja geti, mlango na hatimaye mumewe Henry Massawe uk
Kutaka kwenda kuzika Kilimanjaro sio kwamba alimpenda sana "mumewe"; bali angezikwa hapo nyumbani ingemwekea kauzibe kuuza au kutumia nyumba na eneo jinsi apendavyo!

Bahati mbaya kwake (mdada) walishamstukia wakaamua kumzika marehemu hapo ili kutibua ill motives zake! Got it?
mke mwenyewe hata huko kilimanjaro hakufahamu, atapendekezaje mume anayempenda akazikwe sehemu ambayo haifahamu?
 
Ni tamaa ya kipumbavu tu bila kuona mbele, mafao ya marehemu kwa muajili wake TBS ni haki ya mke na mtoto, pia mafao yote ya marehemu kwenye social security fund ni ya mke na mtoto, hizo sehemu mbili hakuna mtu yeyote anayeweza kulipwa stahili za marehemu zaidi ya mke, Sasa haya yote hayaoni?

Usikute ni group la Jackline Ntuyabaliwe mke wa Reginald Mengi akili zao zipo kwenye kinyeo.

Waweza kukutana mafao ya marehemu ni pesa nyingi kuliko hata pesa za kuuza hiyo nyumba, unachukuwa mafao mtoto aende shule na nyumba IPO, shida iko wapi?

Kama hauna nia mbaya nyumba zenye kaburi hospitali wanapanga vizuri tu bila shida yoyote.
Kichwa yake imejaa makamasi ukizingatia ana mtoto mmoja tu tena mdogo wa miaka 2.
 
Ni tamaa ya kipumbavu tu bila kuona mbele, mafao ya marehemu kwa muajili wake TBS ni haki ya mke na mtoto, pia mafao yote ya marehemu kwenye social security fund ni ya mke na mtoto, hizo sehemu mbili hakuna mtu yeyote anayeweza kulipwa stahili za marehemu zaidi ya mke, Sasa haya yote hayaoni?

Usikute ni group la Jackline Ntuyabaliwe mke wa Reginald Mengi akili zao zipo kwenye kinyeo.

Waweza kukutana mafao ya marehemu ni pesa nyingi kuliko hata pesa za kuuza hiyo nyumba, unachukuwa mafao mtoto aende shule na nyumba IPO, shida iko wapi?

Kama hauna nia mbaya nyumba zenye kaburi hospitali wanapanga vizuri tu bila shida yoyote.
Akili kisoda hizo, yani hao wasukuma wapuuzi sana
 
Baadhi ya Waombolezaji kwenye msiba wa Kijana Henry Massawe aliyekuwa Mkazi wa Kiaraka Magengeni, Bagamoyo Mkoani Pwani, wamelazimika kuvunja geti la nyumbani kwa Marehemu ili kuingia kumzika baada ya kukuta geti hilo limefungwa huku Mke wake akiwa hajulikani alipo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Mahakama ya Bagamoyo kuamuru Marehemu azikwe Bagamoyo na sio Kilimanjaro kama alivyotaka Mkewe.

Kabla ya kuvunjwa kwa geti hilo Waombolezaji walikuwa wamekaa nje wakati wote na baada ya hapo wakaingia na kuuvunja pia mlango wa nyumba ya Marehemu ili mwili uingizwe sebuleni kama ilivyo taratibu za misiba ya kikristo.

Henry Massawe alifariki January 16, 2023 na mwili wake ulisubiri kuzikwa kwa wakati wote huo kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya Ndugu wa Marehemu waliotaka azikwe nyumbani kwake Bagamoyo huku Mke wa Marehemu akitaka azikwe Kilimanjaro kabla ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Vedatus Mwalia kuamua kuwa Marehemu azikwe Bagamoyo.

Mahakama ya Bagamoyo mkoani Pwani leo January 24 2023 kuamuru mwili wa Henry Massawe kuzikwa nyumbani kwake Kiaraka, Bagamoyo kama watakavyo Ndugu zake na kutupilia mbali hoja za Mke wake aliyetaka akazikwe Mkoani Kilimanjaro.

Ndugu Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwa ajili ya maziko ya Marehemu Henry wamekuta geti la nyumbani kwake limefungwa huku ikielezwa kuwa Mkewe hajulikani alipo.
Kuna mtu mmoja mashuhuri sana jana alikuwa anatupa story hii ila kwa mujibu wake ni kuwa:

Marehemu aliandika wosia kutaka akifa azikwe kwenye compound ya nyumba yake ila mkewe akakataa huku ndugu wakishikilia wosia utimizwe

Basi sekeseke hilo likaenda Mahakamani huko hakimu akaamuru wosia wa marehemu ufanyiwe kazi maana yake marehemu azikwe ndani ya compound yake

Mkewe anakataa hili sababu halisi hatujui ila inadhaniwa kuwa kuzikwa kwa marehemu nyumbani kwake kunaweza kuaffect mambo kadhaa

1. Akizikwa hapo nyumba haiwezi chukuliwa mkopo
2. Akizikwa hapo si rahisi nyumba kupata mpangishaji
3. Akizikwa hapo si rahisi kwa mwanaume atakaekuwa na mahusiano na mjane huo kwenda kuishi kwenye nyumba ile
4. Akizikwa hapo si rahisi kupata mnunuzi

Haya yote ni kwa mujibu wa mtu huyo mashuhuri sana hapa nchini
 
Mbona Wosia wa Marehemu Mengi Mahakama iliuutenguwa!? Siyo kila alichosema Marehemu kipindi cha uhai wake lazima kitimizwe, lazima uhalisia pia uaangaliwe! Je Marehemu angesema mkamzike Marekani mngeenda kumzika huko!!??
Inategemea wosia uliandika ukiwa kwenye hali gani.

Kwa Mengi ule haukuwa wosia.
 
Marehemu alishaacha wosia azikwe Bagamoyo. Mke ndo amegoma kwa sababu za kibiashara. Mahakama imetoa amri mke ametoroka hajazika mumewe. Na hapo awali mke alishafumaniwa na picha zake zilichafua hali ya hewa kwa mange
Kuna wanawake roho mbaya unazionea usoni tu, lile lichawi jamaa sijui alikua anawezaje hata kuishi nalo.

Maskini ukute hata mtoto sio wake, na wamempoteza jamaa. Kuna mtu alipost sura ya huyo mwanamke hapa nikakumbuka nlishaiona kwenye database za connection, naona sikua wrong
 
WOSIA batili.

Wosia ni utashi na maamuzi ya marehemu juu ya mambo aliyo na mamlaka nayo 100% na yanayokubalika kisheria.

Ukifa nyumba inakuwa ya mjane, na mjane hataki kaburi mlangoni. Huna haki ya wosia kutaka kuzikwa hapo.

Na huwezi kusema nikifa mke asiuze nyumba wala asipake rangi ya kijivu wala asiingize ndani ki ben 10. Nyumba si yako tena!

Mjane kata rufaa.
Huu ndio uhalisia japo mchungu sana🤣
 
Back
Top Bottom