Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Mimi nishadate na mchaga wa old moshi nikawa namtania alikuwa anachukia japo alinicheat akabeba mimba uko

Hila mwanamke wa kimachame muogope sana akishajua hapa pesa hipo kifo kinakuhusj
Dooh, me wanawake wanaonibamba ni wa pwani kama kule kwetu Tanga mjini, Pangani, Mafia na Bagamoyo, Kisarawe na kusini, hawa wa kaskazini siwaelewi kabisa
 
Haiko hivyo mkuu, mume akifa ukisikia anaenda kuzikwa kwao ujue anaenda alikozaliwa ambako mke hana uhalali nako, hivyo ndugu wa mume watahusika mwanzo mwisho, na mke siku zote anazikwa na mume wake(hapo mwanaume ndiye anaamua mke wake azikwe wapi) hapo mambo ya haki au gender balance hayapo
Ndio maana nasema Ndoa Ni Utapeli mtupu na Ubinafsi mkubwa sana
 
WAFIWA WAMEONA ISIWE TABU WAMEMUWEKEA MKE UA LAKE MLANGO AKIJA AMALIZIE KUZIKA. WAKAMUINGANISHIA NA BANGO[emoji119][emoji22] “MTAKA NYINGI NASABA HUPATA MINGI MISIBA”
Screenshot_20230124_190348_Instagram%20Lite.jpg
Screenshot_20230124_190404_Instagram%20Lite.jpg
 
Baadhi ya Waombolezaji kwenye msiba wa Kijana Henry Massawe aliyekua Mkazi wa Kiaraka Magengeni, Bagamoyo Mkoani Pwani, wamelazimika kuvunja geiti la nyumbani kwa Marehemu ili kuingia kumzika baada ya kukuta geiti hilo limefungwa huku Mke wake akiwa hajulikani alipo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Mahakama ya Bagamoyo kuamuru Marehemu azikwe Bagamoyo na sio Kilimanjaro kama alivyotaka Mkewe.

kabla ya kuvunjwa kwa geiti hilo Waombolezaji walikua wamekaa nje wakati wote na baada ya hapo wakaingia na kuuvunja pia mlango wa nyumba ya Marehemu ili mwili uingizwe sebuleni kama ilivyo taratibu za misiba ya kikristo.

Henry Massawe alifariki January 16, 2023 na mwili wake ulisubiri kuzikwa kwa wakati wote huo kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya Ndugu wa Marehemu waliotaka azikwe nyumbani kwake Bagamoyo huku Mke wa Marehemu akitaka azikwe Kilimanjaro kabla ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Vedatus Mwalia kuamua kuwa Marehemu azikwe Bagamoyo ,
Mahakama ya Bagamoyo mkoani Pwani leo January 24 2023 kuamuru mwili wa Henry Massawe kuzikwa nyumbani kwake Kiaraka, Bagamoyo kama watakavyo Ndugu zake na kutupilia mbali hoja za Mke wake aliyetaka akazikwe Mkoani Kilimanjaro, Ndugu Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwa ajili ya maziko ya Marehemu Henry wamekuta geti la nyumbani kwake limefungwa huku ikielezwa kuwa Mkewe hajulikani alipo,
Kwa mujibu wa mashuhuda mkewe alisema ana mpango wa kuipangisha nyumba hiyo kwa wazungu, hivyo uwepo wa kaburi la mumewe tena mbele ya nyumba hiyo utazuia mipango yake. Hivyo akaamuru mwili usafirishwe akazikwe kwao Moshi.

kwa hali hiyo, nashauri jeshi la Polisi limshikilie huyo mke kuchunguza chanzo cha kifo cha mumewe hata kama amefia hospitali. inawezekana alimwekea dawa iliyommaliza taratibu.

Wanawake wengine wana tamaa ya mali kuliko shetani mwenyewe.
 
Back
Top Bottom