Bagamoyo Port construction set to kick off in January 2018. China and Oman to fund the project

Bagamoyo Port construction set to kick off in January 2018. China and Oman to fund the project

->KWA SABABU HAUTUMII MAPATO YETU YA NDANI,BADALA YAKE UTAKAPOKAMILIKA UTATULETEA MAPATO MAKUBWA / TAFADHALI ULILETEWE WIVU AU FIGISU YOYOTE.
 
Huu ni mradi mzuri sana, viwanda 700 vitakavyojengwa ni kitu kizuri.
Kama Wachina walimwachia Muingereza mji wa Hong Kong kwa miaka 100 lakini eventually muda ulipofika mwaka 1997 hongkong ikarudi kwa wachina, basi na sisi kumuachia mchina bandari kwa miaka 50 sjyo ishu. Miaka 50 kwa nchi siyo mingi itafika tu. Cha msingi kodi zetu za imports ziendelee kupatikana!
 
Hakuna visionary leader kama JPM aliwapose kwanza ili aimarishe bandari ya Dar pamoja na nyingine sasa bandari zote zipo kwenye matengenezo kabambe ili zikikamilika ziweze compete na hii ya Bagamoyo ila watu hilo hawalioni.

Tungewekeza nguvu zetu zote Bagamoyo ambayo kwa asilimia kubwa itamilikiwa na muwekezaji sisi tunachukua kodi tu na kuziacha bandari zetu kwenye hali ya umauti bado Dangote nae alikua anataka apewe bandari binafsi huu ni upumbavu uliotukuka

In fact bandari ya Tanga itakua ndio bandari kinara katika mapato mengi hivyo serikali itanufaika na bandari zake Bagamoyo itakuwa zaidi na export cargo sababu ya heavy industries capacity itakayokua nayo.

Mkuu bila shaka unaeongelea nadharia na si uhalisia wa hizo bandari unazozisema..
Tunapojadili haya mambo tujaribu kujadiri, kushauri pasipo ushabiki au kusifia sifia pasipo hata kujifikirisha..

Ukweli bandari zetu zooote nazijua kwa macho na uhalisia wake naujua, hakuna bandari yenye hali nzuri hata moja kwa sasa Tanzania, tena afadhari hiyo ya Dar es salaam kuliko hiyo Tanga mpaka leo ninavyoongea na wewe iko taabani kabisa pamoja na ile ya mtwara, Achana na theory na maneno ya kuambiwa jaribu hata mwenyewe kufanya weekend tour kwenye hayo maeneo ujionee hali mubashara.

Mombasa port iko na shughuli nyingi naweza sema mara 20 kuliko bandari zetu zote hapa Tanzania, kwanini hii Bandari ipo bize kuliko? Jibu ni rafiki kwa wafanya biashara kuanzia quality ya kazi, speed ya kazi, eneo la kutosha kwa meli kupark na kina kizuri, Maintenance na service za meli ikihitajika na wako na dry dock kubwa pale, hali hii imeifanya hata Mombasa airport kuwa bize na international flight + local flight nyingi kutokea Nairobi nyingi zikiwa zimebeba wageni, Jiji la Mombasa limekuwa bize pia kibiashara na mzunguko mkubwa kwasababu tu ya ubize wa bandari..

Tuache siasa na ubinafsi wa kisiasa ili tusonge mbele, Bandari ya Bagamoyo ilitakiwa iwe kipaumbele cha kwanza kwa serikali kwa yenyewe kuweka hela pale na kumpa mtu afanye operation zoote chini ya usimamizi wa TPA, Bandari ya Tanga ifanywe special port for Tanker zoote za mafuta na ile bulk storage yoote ya dar ihamie kule na reli kutoka Tanga kwenda dar, Arusha, Kahama, rusumo na Mwanza iwe efficient ikiunga mpaka bagamoyo, Bandari ya Dar es salaam ibaki kuwa backup ya Bagamoyo na Tanga ikiwa zimezidiwa na pipeline ya mafuta Tanga - dar iwepo.. Bandari ya Tanga itahitaji matengenezo makubwa kwa meli kubwa kupaki na kuweza kuhandle big operation na sio hizi theory tunazodanganywa na wanasiasa. Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sukari Bagamoyo na kuweka mashamba ya miwa maeneo fulani ya mkoa wa pwani na Plant ya kuzalisha 250MW kwa kutumiwa mabaki ya miwa ilikuwa na faida kubwa.
Project hizo zingekamilika tayari DAR,PWANI na TANGA zingekuwa zimeunganika na kuwa moja ya nguzo kubwa kiuchumi na watu wake wangekuwa na kipato kizuri na hata flight pale JKIA zingekuwa zinapishana..

Mtwara kungejengwa viwanda vitatu vya kusindika samaki na serikali kupitia mifuko ya hifadhi za jamii ikanunua meli nne za uvuvi zitakazovua deep sea na samaki wengine ikanunua kwa wavuvi wetu wadogo wadogo na kuifanya Mtwara port kama eneo la meli, majahazi na uvuvi baharini na pia eneo la meli zoote zitakazotumiwa kama supply kwenye oil/gas rigs baharini... Pia kungejengwa viwanda viwili vya kubangua korosho Mtwara na Lindi bila shaka huu mkoa na bandari yake ungekuwa bize ajabu maana hata mandege ya kirusi yangetua kila siku kuchukua fresh fish, na processed one to europe.

LOW PRODUCTION, LACK OF VISIONARY AND INNOVATIVE LEADERS NDIO TATIZO LA UMASIKINI WA TANZANIA.
 
..utawala wa JK walisaini mkataba utakaowezesha Tz kuwa na kiasi cha hisa ktk bandari mpya.

..hisa hizo zingepatikana kama serekali ingetoa fedha kulipa wananchi waliopoteza ardhi zao ili kupisha mradi.

..serekali ya Magufuli imeshindwa ku raise pesa za kufidia wananchi na hivyo kupelekea kupoteza hisa za Tz ktk mradi.

..Wachina watamiliki bandari ya Bagamoyo kwa miaka 30++ kabla hawajaikabidhi kwa Tz.

..nina wasiwasi mbele ya safari tutaanza kulalamika kwamba tunaibiwa kutokana na kusaini mkataba mbaya.

NB.

..kama sijakosea aliyeleta mradi huu ni Waziri Mkuu Pinda alipofanya ziara China.

Cc Richard, Nzi
huo mkataba umeuona au ni hesrsay tu
 
Nchi haiendeshwi kama vicoba.huwezi kuniambia nishike linalonihusu kama wameshindwa kuongoza wakae pembeni.
CCM imechokwa nchi nzima
Nyinyi ndo tumewachoka na ukigeugeu wenu bola hawa kijani at least wanajitambua sio nyinyi mnatapatapa kwa kujiharishia na kulamba matapishi
 
Hapa kuna tatizo: Ni mzigo kiasi gani unatarajiwa kushushwa kwenye bandari hii mpya ya Bagamoyo wakati tukijua uwepo wa bandari bora za Mombassa na Dar es salaam, ambazo ziko tayari kwenye ushindani ?. Ufukwe wa bahari yetu una bandari za Tanga na kuna kibwagizo chake; bandari ya Mwambani,Kuna Mtwara ambayo upanuzi unaendelea na ile ya Kilwa inayopigiwa ndogo ndogo.

Huu mlundikano wa bandari na hasa tukizingatia uwepo wa uwekezaji unaofanana na huu wa kwetu kwa nchi jirani (Zanzibar ikiwemo) za Kenya na Mocambique kwa maana ya Malindi na Beira, siamini kama kweli uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo utakuwa na tija. Ningeshauri: 1. kama itawapendeza watunga sera, mradi huu wa bandari ya Bagamoyo uhamishiwe mkoani Kigoma.
2. Bandari ya Dar es salaam iboreshwe kama ilivyo kwenye mpango wake endelevu kufikia gati 20+
3. SG reli ijengwe kuanzia Kigoma ije kukutana Tabora na hii inayojengwa sasa ya Dar-Isaka-Mwanza.

Soko lililoko mashariki mwa DRC maeneo ya Goma, majimbo ya Kivu Lubumbashi na Kisangani yangeweza sana kufaidika na mradi huu kwa kuwa upande ule wa magharibi mwa DRC kuna bandari chache za Cabinda na Lobito ambazo haziwezi kufua dafu kwa wakati huu, katika ukanda wetu wa bahari ya hindi.
 
Port of Dsm bado hatujaweza ku-utilize it to the max. na mizigo tunaambiwa imezidi kupungua kutokana na sera zetu.
Tunakimbilia kujenga nyingine wakati tungeweza kupanua zile za tanga na mtwara kwa fedha kdg. Anyway kikwete alikuwa akisaini mikataba ya hovyo kabisa ktk Nchi hii.
 
huo mkataba umeuona au ni hesrsay tu

..iliripotiwa na gazeti linaloaminika kuwa tumeachia hisa zetu zote.

..MSEMAJI WA SEREKALI hajajitokeza kukanusha.

..vilevile kwanini umkataba unafichwa?
 
..utawala wa JK walisaini mkataba utakaowezesha Tz kuwa na kiasi cha hisa ktk bandari mpya.

..hisa hizo zingepatikana kama serekali ingetoa fedha kulipa wananchi waliopoteza ardhi zao ili kupisha mradi.

..serekali ya Magufuli imeshindwa ku raise pesa za kufidia wananchi na hivyo kupelekea kupoteza hisa za Tz ktk mradi.

..Wachina watamiliki bandari ya Bagamoyo kwa miaka 30++ kabla hawajaikabidhi kwa Tz.

..nina wasiwasi mbele ya safari tutaanza kulalamika kwamba tunaibiwa kutokana na kusaini mkataba mbaya.

NB.

..kama sijakosea aliyeleta mradi huu ni Waziri Mkuu Pinda alipofanya ziara China.

Cc Richard, Nzi
Hata sasa hivi una wasiwasi?
 
Back
Top Bottom