Hakuna visionary leader kama JPM aliwapose kwanza ili aimarishe bandari ya Dar pamoja na nyingine sasa bandari zote zipo kwenye matengenezo kabambe ili zikikamilika ziweze compete na hii ya Bagamoyo ila watu hilo hawalioni.
Tungewekeza nguvu zetu zote Bagamoyo ambayo kwa asilimia kubwa itamilikiwa na muwekezaji sisi tunachukua kodi tu na kuziacha bandari zetu kwenye hali ya umauti bado Dangote nae alikua anataka apewe bandari binafsi huu ni upumbavu uliotukuka
In fact bandari ya Tanga itakua ndio bandari kinara katika mapato mengi hivyo serikali itanufaika na bandari zake Bagamoyo itakuwa zaidi na export cargo sababu ya heavy industries capacity itakayokua nayo.
Mkuu bila shaka unaeongelea nadharia na si uhalisia wa hizo bandari unazozisema..
Tunapojadili haya mambo tujaribu kujadiri, kushauri pasipo ushabiki au kusifia sifia pasipo hata kujifikirisha..
Ukweli bandari zetu zooote nazijua kwa macho na uhalisia wake naujua, hakuna bandari yenye hali nzuri hata moja kwa sasa Tanzania, tena afadhari hiyo ya Dar es salaam kuliko hiyo Tanga mpaka leo ninavyoongea na wewe iko taabani kabisa pamoja na ile ya mtwara, Achana na theory na maneno ya kuambiwa jaribu hata mwenyewe kufanya weekend tour kwenye hayo maeneo ujionee hali mubashara.
Mombasa port iko na shughuli nyingi naweza sema mara 20 kuliko bandari zetu zote hapa Tanzania, kwanini hii Bandari ipo bize kuliko? Jibu ni rafiki kwa wafanya biashara kuanzia quality ya kazi, speed ya kazi, eneo la kutosha kwa meli kupark na kina kizuri, Maintenance na service za meli ikihitajika na wako na dry dock kubwa pale, hali hii imeifanya hata Mombasa airport kuwa bize na international flight + local flight nyingi kutokea Nairobi nyingi zikiwa zimebeba wageni, Jiji la Mombasa limekuwa bize pia kibiashara na mzunguko mkubwa kwasababu tu ya ubize wa bandari..
Tuache siasa na ubinafsi wa kisiasa ili tusonge mbele, Bandari ya Bagamoyo ilitakiwa iwe kipaumbele cha kwanza kwa serikali kwa yenyewe kuweka hela pale na kumpa mtu afanye operation zoote chini ya usimamizi wa TPA, Bandari ya Tanga ifanywe special port for Tanker zoote za mafuta na ile bulk storage yoote ya dar ihamie kule na reli kutoka Tanga kwenda dar, Arusha, Kahama, rusumo na Mwanza iwe efficient ikiunga mpaka bagamoyo, Bandari ya Dar es salaam ibaki kuwa backup ya Bagamoyo na Tanga ikiwa zimezidiwa na pipeline ya mafuta Tanga - dar iwepo.. Bandari ya Tanga itahitaji matengenezo makubwa kwa meli kubwa kupaki na kuweza kuhandle big operation na sio hizi theory tunazodanganywa na wanasiasa. Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sukari Bagamoyo na kuweka mashamba ya miwa maeneo fulani ya mkoa wa pwani na Plant ya kuzalisha 250MW kwa kutumiwa mabaki ya miwa ilikuwa na faida kubwa.
Project hizo zingekamilika tayari DAR,PWANI na TANGA zingekuwa zimeunganika na kuwa moja ya nguzo kubwa kiuchumi na watu wake wangekuwa na kipato kizuri na hata flight pale JKIA zingekuwa zinapishana..
Mtwara kungejengwa viwanda vitatu vya kusindika samaki na serikali kupitia mifuko ya hifadhi za jamii ikanunua meli nne za uvuvi zitakazovua deep sea na samaki wengine ikanunua kwa wavuvi wetu wadogo wadogo na kuifanya Mtwara port kama eneo la meli, majahazi na uvuvi baharini na pia eneo la meli zoote zitakazotumiwa kama supply kwenye oil/gas rigs baharini... Pia kungejengwa viwanda viwili vya kubangua korosho Mtwara na Lindi bila shaka huu mkoa na bandari yake ungekuwa bize ajabu maana hata mandege ya kirusi yangetua kila siku kuchukua fresh fish, na processed one to europe.
LOW PRODUCTION, LACK OF VISIONARY AND INNOVATIVE LEADERS NDIO TATIZO LA UMASIKINI WA TANZANIA.