Bado nawasiwasi na utekelezaji wa huu Mradi. Sijamsikia Rais akigusia chochote juu ya mipango ya mradi huu hata alipokuwa katika ziara yake ya uzinduzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani. Kwa manufaa ya Mradi huu, Rais wetu kamwe asingesita kuelezea chochote juu ya Mradi huu. Bila shaka kuna mengi nyuma ya pazia.
Binafsi naunga mkono Mradi huu hasa kwa upande wa ajira, mapato kwa serikali, kupanuka kwa uzalishaji katika kilimo, viwanda na masoko, ukuaji wa mji wa Bagamoyo na Dar es Salaam, kuongeza ushindani wa utoaji huduma kwa bandari zetu na pengine kupunguza msongamano katikati ya mji wa Dar es Salaam.
Kwa ujumla, iwapo hii mikataba ingeweza kutazamwa upya na kuondoa mapungufu yaliyopo, bado sisi kama Taifa ni wanufaika wakubwa katika mradi huu!