Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
chai moto kombe bati!Mboga moto, ugali moto
sokoni inaingia lini hii kituRIWAYA; BAHARIA
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA NANE
Baada ya kusema vile Jay alishangaa akishikwa kwa nguvu na zile njemba mbili ziliokuwa mle chumbani kisha yule aliekuwa amevaa miwani alimfunga na karatasi yenye gundi mdomoni ili asipige kelele,kisha Dr Masimba alisimama na kuchukua sindano iliokuwa kenywe mkebe na ilikuwa na dawa kwenye bomba lake.
Akamfuata Jay ambae alikuwa ameshikwa vyema licha ya kujitikisa kwa uoga bila mafanikio.
Sindano ilizama kwenye nyama na kisha ikasukumwa dawa yote iliokuwa mle na Jay alibaki akiona kizunguzungu huku macho yake yakishindwa kuona vyema, alitamani kuongea ila alishindwa, alitamani kulia napo alishindwa, akajibweteka kwenye kiti baada ya kuachiwa.
Alihisi kichwa kikiwa kizito na mwili mzima ukipitiwa na ubaridi wa ajabu huku maungio ya mifupa yake ikizizima kwa ubaridi ule, ni kama akili yake iliganda mana hakusikia kitu wala kuona kitu,alikaa kama sanamu la ibada. Hakujua amekaa koma muda gani, ila alikuja kupata fahamu na kujikuta akiwa amelala kwenye kitanda cha wagonjwa na mwili wake ukiwa imara ni kama hakujatokea kitu muda mfupi uliopita.
Akainuka kitandani na kukutana na sura za watu wawili wakiwa wamemsimamia.
Walikuwa ni wale wawili wenye kuvaa nguo za kufanana na Dr Masimba pamoja na yule bwana anaevaa miwani hawakuwemo. Akabaki akiwatizama.
“Umeamka na unajisikia vizuri bila shaka” Alihoji jamaa mmoja.
Jay hakujibu.
“Sasa sikiliza,sindano uliochomwa imekuondolea maralia yako ila imekupa ugonjwa wa kansa ya mifupa” Alisema bwana mwingine tena.
Jay alisimama kwa jaziba na kumvaa jamaa yule, ila alitulizwa chini kwa jebu moja na akabaki akilia kwa uchungu na kujibweteka kitandani kama zoba. “Aliekuponza ni Vedi; ila usijali, kuna tiba yake na tutakupatia hadi ukifanikisha yale tunayoyataka na kikubwa zaidi uoneshe kufunga mdomo na ukijaribu kusema lolote, tumekuwekea kifaa kitakachokuwa kinatupa taarifa ya mazungumzo yako popote” Alisema jamaa mwingine aliempiga jebu Juma. Jay aliiunua uso na kuwatazama watu wale na alipojaribu kusema kitu,alijikuta anashindwa kusema na kubaki akilia kwa uchungu.
“Umepandikwa kirusi Flora na kinakula chembe hai nyekundu na ndani ya siku kumi usipopata tiba unakufa, hivyo ni muhimu ufanye tunachokuagiza ili uokoe maisha yako” Alisema tena yule jamaa.
Wakiwa bado wanazungumza mara akaingia yule mtu anaependa kuvaa koti na miwani wakati wote.
“Nadhani mwacheni aende, na maelekezo tutampa kwenye simu” Yule bwana alizungumza na kisha akamgeukia Jay.
“Bwana mdogo;ili usaidike inahitajika utimize tunayoyahitaji na hivi sasa maisha yako yapo kwetu, usiripoti kituo chochote cha polisi na usifanye ujinga wowote ule, nenda kapumzike ujumbe wako utaukuta kwenye simu na endapo Vedi akitokea fanya kile tutakachoakuagiza” Alisema tena bwana yule na punde akaingia mtu mwingine na kumwamuru Jay asimame waondoke pale ndani.
Jay hakuwa mbishi baada ya kugundua yupo kwenye mikono isio salama.
Lakini alijiuliza swali moja!
Kwanini wamtumie yeye kwenye matatizo yao na Vedi?; Vedi kachukua nini muhimu kwa watu hawa?.
Hakupata jibu hata kidogo na alitoka akiwa hana amani ya mwili wake na alihitaji kukaa na kutafakari kuhusu jambo lile.
Hakika alipagawa.
Baada ya kutoka kwenye kile chumba, walibaki watu watatu, ambao ni yule bwana mvaa kofia; koti na miwani pamoja na wale vijana ambao walipenda kuvaa nguo za kufanana wakati wote.
“Sasa Cholo unaamini hii itasaidia?” Alihoji kijana mmoja huku akimtizama yule jamaa anaependa kuvaa kofia na miwani ambae ndie Cholo.
“Panga; tukisema tumuue yule binti hivi sasa kiukwelii, itatupa shida, hatujui hadi hapo kawasiliana na nani baada yakuiona ile maiti, kikubwa ni kufunga mianya yote kisha tutajua cha kumfanya tukiwa na uhakika wa zilipo taarifa za yale alioyaona,kama isingekuwa kadi ya harusi aliodondosha mule na kisha kuchukua kile kitabu nilichokisahau pale, tusingejua lolote kuhusu mtu alieona ile maiti ya Baharia” Cholo alimweleza Panga.
Panga alitikisa mabega na kumwangalia mwenzie.
“Gomba unaonaje hizi mbinu”Cholo alimhoji Muki ambae alikuwa amekaa kimya muda wote.
“Tutazame mienendo yake, akileta utata ile mbinu yetu ya siku zote itamfaa bila shaka” Gomba alijibu na wote wakatabasamu mule ndani na kutoka nje wakikiacha chumba kikiwa kipweke kabisa. **
Jay alijipiga kichwani baada mawazo yale kumpitia kwa kasi na kubaki akiwa amesimama barabarani bila kujua ametumia muda gani kuwaza yaliompata hadi kupelekea kumkana mpenzi wake wakati huu aliohitaji msaada wake.
Akajitazama na kuona alivyopendeza.
“Eti naenda kumzika Vedi niliemwacha ndani kwangu” Alijiwazia kwa uchungu huku akipiga hatua na kuelekea barabara kuu ili apate uber.
Lakini wale jamaa ni kina nani hasa na Vedi kawafanya nini?
Alijuliza tena huku akishindwa kuyazuia machozi yalioanza kumtoka.
Hakufika barabarani, mara mbele yake ikasimama gari nyeusi na vioo vikashushwa.
Walikuwa ni Gomba aliekuwa dereva na Panga aliekuwa nyuma amekaa.
“Bila shaka unahitaji msaada wa usafiri kwenda msibani!” Alisema Panga.
Jay alibaki akitetemeka baada ya kuwaona wale jamaa ambao ndani ya siku mbili waligeuka kuwa waongoza maisha yake.
“Njoo twende na tafadhali kuwa mtu wa majonzi, wewe ni mfiwa ujue” Alisema Gomba.
Jay hakuwa na namna akafungua mlango na kuingia, na hapo akagundua kulikuwa kuna mtu wa tatu na alikuwa ni Cholo.
“Tunaenda msibani; ila jitahidi sana usioneshe tofauti kama unavyofanya hivi hapo njiani bwana mdogo” Cholo aliasa.
“Lakini kwa nini mnatufanyia yote haya?” Alihoji Jay.
“Kwa sasa wewe bado mdogo ila ukikuwa utajua ndevu za wazee hazichezewi na nzi” Alisema Cholo kwa fumbo ambalo linahitaji akili kulifumbua.
Safari yao ilikuwa ni ya kimya kingi kuliko maneno na baada ya foleni za hapa na pale, hatimae walifika.
“Gomba utaongozana na huyu bwana mdogo” Aliagiza Cholo.
“Kwanini msiniache peke yangu aisee” Jay alisema huku akianza kushuka.
Cholo alicheka kidogo.
“Hadi hapo tushakuona una roho ndogo, hivyo hatuwezi kukuamini hata kidogo.” Cholo alisema huku akijiweka sawa bila kuonesha dalili ya kushuka.
Gomba alishuka na waliongozana na Jay kuelekea kwenye nyumba ya Mzee Mashimo.
“Hakikisha mimi na wewe tunakuwa marafiki na mtu asijue tofauti zetu” Gomba alimuonya Jay huku wakidi kusonga.
Walifika hadi getini kulipokuwa na watu wawili kwa ajili ya kuongoza wageni wanaofika na mmoja kati yao alimfahamu Jay na hivyo alimsindikiza hadi ndani na kisha yeye kurudi.
“Kwa hiyo hadi ndani unataka kuingia?” Jay alimgeukia Gomba.
“Ulipo nipo bwana mdogo na usisahau mimi ni rafiki yako” Gomba alijibu huku akitabasamu kama kwamba ni jambo la kawaida tu analozungumzia.
Waliingia ndani na kuona jeneza likiwa limewekwa sebuleni huku wamama wakiwa wamelizunguka na nyuso za majonzi.
Msangu ambae ni dada yake Vedi alisimama baada ya kumuona shemeji yake akiwa ameongozana na mtu mwingine ambae hakumfahamu kabisa.
Msangu aliangusha chozi baada ya kumuona shemeji yake.
Jay nae aliangusha chozi, ila chozi lake lilikuwa lina mengi ndani yake.
Gomba alikuwa akiangaza na alimuona mwanamke mmoja akiwa amekaa sambamba na waombolezaji, mwanamke yule alimpa ishara fulani na Gomba alielewa mambo hayako sawa pale.
Msangu alimshika mkono Jay na akamwongoza kuelekea chumbani kwa wazazi wake na Gomba nae akafuata.
“Tafadhali, kuna muda inabidi utumie akili kuliko nguvu” Jay alimkoromea Gomba kwa sauti ya chini ila iliojaa jaziba. Gomba akasimama na kutafuta sehemu na kukaa pamoja na waombolezaji wengine.
Jay aliingizwa kule chumbani na kumkuta mama yake Vedi akiwa mkavu usoni huku akiwa hana hata chembe ya chozi.
Mama msangu alisimama baada ya kumuona Jay.
“Na wewe unaamini mkeo kafa kweli?” Mama msangu alihoji na Jay alishindwa cha kujibu.
Mama Msangu alianza kuongea kwa sauti huku akionekana dhahiri kutokukubaliana na suala lile la kifo cha Vedi hata pale ambapo Jay alitaka kutetea hoja ya kifo kile Mama yule alikataa kata kata na hatimae alimshika mkono Jay.
“Mwanangu twende nikuoneshe kitu; Mkeo hakuwa na mwanya kabisa licha ya kujitahidi kufanana ila nimemgusa midomo yake japo watu wamenizuia” Alisema Mama msangu huku akimshika akitembea kuelekea sebuleni.
Na walipotoka watu wakawatazama, Mama yule hakujali na akaelekea lilipo jeneza.
Gomba aliona kitendo kile na tayari alishaambiwa na yule mwanamke aliekuwa pale msibani kinachoendelea, haraka akasimama na kushika mfukoni na akapiga hatua ndefu hadi akawafikia na kwa kuwa Mama msangu alikuwa ameshika mfuniko wa jeneza;wamama wengine nao wakaanza kusogea kumkataza mana alishavuruga huko nyuma na hawakutaka kabisa aliguse jeneza lile,lakini kasi ya Gomba ilikuwa ni kubwa na kwa wepesi akamshika mkono Mama Msangu na Mama Msangu hakutaka kuzuiwa hivyo akautoa mkono ule na kutaka kuufuangua mfuniko wa jeneza.
Mara akasita na kujishika kichwa na kuanguka chini.
Haikupita dakika moja akainuka, ila aliinuka kwa mtindo wa ajabu, aliinuka kwa kujikuna huku akicheka na kuunguruma kama simba na kuongea maneno yasiyoeleweka.
Watu walijawa na taharuki na vilio vilianza upya.
Jay aliona tukio lile ila hakujua Gomba kwa nini alimshika mkono mama yake huyo.
“Wewe bwege umemfanya nini huyu mama?” Jay alifoka kwa jaziba licha ya kujizuia sauti isitoke.
Gomba akainua mabega kukataa.
Jay akamshika ukosi wa shati.
Ukaanza mvutano na mparanganyiko ndani ya nyumba ya mzee mashimo.
Mama Msangu anajikuna na kuunguruma hovyo huku Jay akiwa anavutana na rafiki yake wa bandia,watu nao wamebaha kwa yanayoendelea.
Jay alikuwa amegeuka mbogo alijua kabisa kuna kitu kimefanywa na Gomba kwa Mama msangu.
Yule mwanamke aliekuwa miongoni mwa waombolezaji akasogea hadi nyuma ya Jay na kama anaetaka kujifunia kanga aliojitanda akampiga pigo moja la kisogo bila mtu kugundua kilichotokea na akajitandua kanga na kujitanda tena.
Jay akalegea na kwenda chini kama gunia la chawa wa jaani.
Gomba akapaza sauti ya hamaniko huku akiwa amemshika Jay na watu walizidi kuchanganyikiwa zaidi.
Gomba akaomba kupiga simu ya dharura ili watu wale wawahishwe hospitali; Wazo lake liliungwa na wengi waliokuwapo pale ndani na akapiga simu.
***
Dakika thelathini zilipita na gari la wagonjwa lilifika pale na haraka haraka wauguzi wa huduma ya kwanza walishuka na kuwabeba Jay na Mama Msangu na Msangu na Baba yake walikataliwa kuingia ndani ya gari lile kwa kisingizio ni dogo halitoshi msindikizaji.
Mazishi yaliingiliwa na taharuki, ratiba ikabadiliswa hadi ijulikane mstakabali wa afya za walengwa wa marehemu.
Ajabu nyingine ni kuwa; taharuki ilibeba mawazo ya watu kiasi hakuna aliekumbuka kufuatilia gari lile linaelekea hospitali gani.
Watu waliendelea na malumbano yasioyo na tija.
Lakini wangejua yanayoenda kuwapata ndugu zao, hakika wasingebishania ratiba ya mazishi ya maiti bandia.
**
Weka komenti yako ili iwafikie watu wengi zaidi.