Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimelipia Mpesa bossRIWAYA; BAHARIA
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA TISA
Mazishi yaliingiliwa na taharuki, ratiba ikabadiliswa hadi ijulikane mstakabali wa afya za walengwa wa marehemu.
Ajabu nyingine ni kuwa; taharuki ilibeba mawazo ya watu kiasi hakuna aliekumbuka kufuatilia gari lile linaelekea hospitali gani.
Watu waliendelea na malumbano yasioyo na tija.
Lakini wangejua yanayoenda kuwapata ndugu zao, hakika wasingebishania ratiba ya mazishi ya maiti bandia.
***
Gari ile ya wagonjwa iliishia kwenye nyumba ya kifahari na kisha wakashuka watu wawili waliojifanya kuwa ni wauguzi na baada ya kushuka mmoja akaelekea ndani na punde akarudi akiwa na jamaa wengine wawili waliokuwa wameshiba miili yao na maumbo makubwa yalionasibisha wingi wa mlo wao.
Watu wale wakawashusha na kuwaingiza ndani kisha wakawekwa kwenye chumba cha pamoja na punde mtu mmoja akachukua sindano na kumchoma Jay na kisha alimchoma na Mama Msangu.
Hazikupita dakika tano wote wawili walizinduka na kushangaa wakiwa kwenye chumba kimoja na wamesimamiwa na watu wengine watano ambao walikuwa kimya muda wote.
“Juma mwanangu kwani imekuwaje tena!?” Mama Msangu alihoji kwa woga baada ya kuonekana hayaelewi mazingira waliopo.
Juma akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akamjibu.
“Sina la kusema ila nadhani tupo kwenye mikono mibaya”.
Akivyokwisha kusema hivyo haikuchukua hata sekunde akajikuta akinyayuliwa kwa nguvu na kupigwa kichwa matata na kisha akaonywa asirudie kusema hovyo kabla hajaruhusiwa.
Akiwa bado anaugulia maumivu akabebwa kwa nguvu na kutolewa kwenye chumba kile na hata Mama Msangu alipojaribu kutetea aliishia kupigwa makofi mazito yaliomwacha akiwa hajui cha kufanya.
Baada ya kutolewa kwenye kile chumba; Jay alipelekwa kwenye gari ambalo lilikuwa nje ya uzio wa nyumba ile waliokuwamo.
Alikutana na Gomba akiwa na mwanamke ndani ya gari.
“Panda tukurejeshe nyumbani kwako!!” Gomba alisema huku akimtizama Jay.
Jay alipanda na gari ikaondolewa.
“Yani sikuwahi kudhani kama kuna mtu mjinga kama wewe aisee!!” Gomba alifoka huku akiwa makini na usukani wa gari.
Jay alikaa kimya.
“Huna kifua kabisa bwana mdogo na utakuwa tatizo badae” Gomba alizidi kufoka.
Wakati Gomba akiendelea kufoka kwenye gari; ni wakati huo ambao Mama Msangu alikuwa ameshikwa kwa nguvu na hakujua wale vijana waliokuwa wamemzunguka walitaka kumfanya nini.
Walimbana vizuri na hakuweza kufurukuta kabisa na ndipo kijana mmoja alichukua kamera na kuiwasha kisha mmoja wa vijana wale akavua nguo zake zote na kusalia na mtupu, kijana mwingine nae alivua nguo zake zote na kisha wakaenda kumvamia Mama Msangu na kumvua nguo zake zote nae akabaki mtupu kama alivyozaliwa.
Mama Msangu alijionea aibu kuwa vile mbele ya vijana wadogo rika sawa na wanae, alilia kwa uchungu mana akili yake ilimwambia ni kitu gani hasa kilikuwa kinafuata kwake wakati huo.
Kwa uchungu na mapigo ya moyo yakaenda mbio kuliko kawaida na taratibu akalegea na kupoteza fahamu.
“Ooh shit!! Hatuwezi kupiga picha akiwa hivi labda tungoje azinduke” Alisema kijana aliekuwa na kamera na wale vijana waliokuwa wamevua nguo wakavaa nguo zao na kisha mwenye kamera alianza kupiga picha mwili wa Mama Msangu uliolala chini bila fahamu.
Aliporidhika akaomba avalishwe nguo zake na kisha wakamchoma sindano nyingine tena kisha wakakubaliana apelekwe Muhimbili kwenye wodi za watu wenye matatizo ya akili, mana waliamini kabisa akiamka hataweza kuwa kwenye utimamu wake tena kulingana na dawa aliochomwa.
Alikuwa ni kichaa mtarajiwa huku picha zake za uchi alizopigwa akiwa amelala zikihifadhiwa kwa kazi waliojua vijana wale.
Vedi alifika hadi kwenye mkahawa wa Hard Rock na kutafuta sehemu nzuri na kukaa kisha akaagiza maji ya baridi na kunywa huku akingojea dakika chache ili kufika saa moja ya usiku, muda ambao walikubaliana na Mamu kukutana hapo.
Akiwa ametulia mara simu yake ikaita.
Namba zilikuwa ni za Mamu.
Akapokea.
“Upo wapi wewe” Mamu aliuliza kwa mashaka kidogo.
“Nipo mashariki mwa mgahawa huu” Vedi alijibu.
Simu ikakatwa.
Akiwa bado anashangaa kukatwa kwa simu, mara mbele yake alisimama mwanamke mzuri wa sura na umbo la kuvutia, ila hakuonekana kuwa na furaha na kila mara alikuwa akiangaza huku na huko kama anaehofia jambo.
“Wewe ndie binti Mashimo?” Mamu alihoji huku akimakinika kumtazama Vedi.
Vedi alitikisa kichwa kukubali.
Mamu alikaa kwenye kiti kilichokuwa kwenye meza aliokuwa anatumia Vedi.
“Wewe ulipata wapi namba yangu” Mamu alihoji huku akimtizama Vedi usoni.
“Samahani kama nitakuwa nimekukwaza ila nimeipata sehemu ambayo ilinishawishi nikupigie” Vedi alijibu huku akikwepa kujibu mahali alikoipata hiyo namba.
“Sawa! Na ulijuaje inanihusu mimi na Banzi” Aliuliza Mamu kwa sauti ya chini kidogo.
“Niliipata kwenye vitu vya Banzi na pale nilikuwa nabahatisha tu baada ya kuona kuna ujumbe unakuhusu” Vedi alijibu.
“Vitu gani! Begi lake ama simu zake?” Mamu alihoji kwa papara.
“Hapana,sio vyote hivyo” Alijibu Vedi.
“Sasa vitu gani labda!?”
“Kitabu!!” Vedi alijibu.
“Ooh shit!! Hilo ni kosa litakalokugarimu binti” Mamu alisema kwa wasi wasi huku akitizama pande zote kwa makini.
Vedi alitumbua macho kwa kutokuelewa ni vipi hicho kitabu kiwe kina matatizo upande wake.
“Hicho kitabu kidogo kimepeleka wengi kuzimu na yawezekana hata mume wangu nae ameshafariki kwa sababu ya hicho kitu!” Mamu alisema kwa huzuni huku dhahiri akionekana chozi linamtoka.
Eh makubwa,inamaana hajui kama mume wake ameshafariki? Na hicho kitabu kina shida gani hadi kichukue uhai wa watu kiasi hicho hadi Mamu aogope na Mamu anajua nini kuhusu mkasa wa mumewe?
Yalikuwa ni maswali yaliopita kwa kasi ndani ya kichwa cha Vedi.
“Kwani kuna nini katika mambo haya? Alihoji Vedi.
“Trust me kama wanajua una hiko kitabu, watakuhangaisha sana watu wale na kama uliwahi kuonana na Banzi; basi wewe ni sawa na maiti inayotembea.”
Vedi alitumbua macho kwa maneno yale.
“Banzi nilimuonya hakusikia, ona sasa…..anyway hakikisha unaubeba msalaba wa roho zote zilizotoka kwa ajili ya mambo yaliomo humo na pia pigana kwa ajili yetu sote na aamini utavuka majaribu yaliotushinda sisi” Mamu alisema na kusimama ili aondoke; Vedi alimshika mkono.
“Dada unaniachia mafumbo bila utatuzi na peke yangu siwezi, pigana juu ya mumeo tafadhali. Mumeo ameuwawa” Vedi alisema kwa hisia.
Mamu akigeuka na kujibweteka kwenye kiti kama mgonjwa, ilikuwa ni ngumu kukubaliana na hiyo hali ya kusikia kifo cha mumewe kwenye masikio yake, alifuta machozi yalioanza kumtiririka kwa fujo.
“Hapa si pahali salama na wamejaa Jezebeli wenye masikio ya popo,tafadhali fanya niliokwambia, nilipambana kuokoa uhai wake ila nimeshindwa, nawe tumia njia zako kutafuta uhuru wako” Mamu alisema huku akijifuta machozi.
Vedi kuna kitu alikitilia maanani kwenye maelezo ya Mamu.
Neno Jezebeli!
Akajiuliza; Jezebeli ni nini na kama ni watu ni kina nani na kwenye kile kitabu cha kumbukumbu alichonacho Jezebeli alitajwa na alitajwa kupatikana kwenye hilo eneo la Hard Rock Café.
“Jezebeli ni kina nani au ni nani?” Vedi alihoji.
Mamu aliangaza tu kisha akaelekeza macho yake upande wa pili kulikokuwa na wahudumu wa mgahawa ule; Vedi nae alitazama kule ila aliishia kuona wahudumu wakipishana huku na huko.
Hakujua iliashiria nini na zaidi alichogundua ni kuwa miongoni mwa wahudumu wale baadhi hawakuwa wanaume wa kawaida kwa kuwaona tu, walikuwa ni wanaume waliozidiwa na homoni nyingi za kike na kujikuta wakifanya matendo kama ya wanawake.
Wanaume jina tu.
Vedi akarudisha macho kwa Mamu.
“Sijaelewa lolote!!” Vedi alisisitiza
Mamu hakumjibu, akasimama na kuchukua mkoba wake na kuondoka na kumwacha Vedi akiwa aezubaa na chupa ya maji mkononi.
“Hapa kuna kitu sio bure” Vedi alijisemea huku nae akisimama na kutoka ndani ya mgahawa ule.
Alihitaji kurejea nyumbani kwa Jay ili apumzike na asubiri siku ya kesho itakavyokuwa.
Jay alifikishwa nyumbani na Gomba kisha Gomba yeye akapanda gari na kuondoka bila kusema jambo lingine lolote.
Jay alipiga hatua chache na kufikia lango la nyumba yake, akafungua na kuingia ndani.
Nyumba nzima ilikuwa ni kiza kizito na hakuhofia mana alijua ni yeye anaepaswa kuwasha taa ili nuru ipate kutamalaki ndani.
Akavua viatu vyake kuvitupia karibu na sofa kisha akaenda ukutani na kuwasha taa.
Nusura apige mweleka kwa alichokiona.
Kwenye sofa walikuwa wamekaa watu wawili bila wasiwasi; Jay akatazama mlango na kuhakikisha ni yeye alieufungua na si mwingine. Imekuwaje watu hawa wapo ndani tena?
Hakukuwa na wa kumjibu.
Walikuwa ni Panga na Cholo.
“Aisee ninyi mmeingiaje humu?” Jay alihoji kwa wasiwasi.
“Kwa hiyo unahisi sisi ni majini au?” Panga aliuliza kwa kebehi.
“Inabidi mniheshimu hata kama mnaniongoza tafadhali, hapa sio pa kuingia kila mnapotaka aisee!!” Jay alifoka akiwa bado amesimama kwa wasiwasi.
“Shida yetu alikuwa ni mkeo ila kwa kuwa umetangulia wewe, basi haina shida mana hata wewe tunashida na wewe” Cholo alijibu huku akijipapasa kwenye paji la uso bila wasiwasi.
“Unajua dogo leo umetuudhi sana kwa kile ulichoonesha pale msibani, yani kama si ujanja ungeharibu kila kitu aisee!” Panga alilalama.
“Sasa mimi nimefanya nini labda.” Jay alihoji.
“Hujui?” Cholo alishangaa kisha akajichekesha kidogo.
“Kwa hiyo ulivyomkwida Gomba si kuharibu mambo kule? Au unadhani kungekuwa na askari kanzu si angefuatilia kujua kinachoendelea?” Cholo alihoji huku dhahiri sauti yake ikiwa imetawaliwa na jaziba kubwa.
“Lakini alipaswa kunishirikisha kabla hajafanya lolote jamani, akili yangu haipo sawa kabisa mjue!” Jay alilalama.
“mh! Eti akili haipo sawa” Panga alisema huku akimgeukia Cholo.
“Si unaona? Nilikwambia huyu sio njia ya kutufikisha tunakokutaka, ila ni janga hili, sasa akikutana na mwela(polisi) itakuwaje? Panga aliendelea kufoka huku akimlaumu Cholo.
“Sasa tumfanyeje labda,kumuua sasa ni tatizo jipya na kubwa zaidi” Cholo alisema kama vile wanaemeongelea hayupo pale.
Jay aliyasikiliza vyema maongezi yao na hapo aliona kabisa kinachofuata kwake ni kifo bila huruma. Hakutaka hilo limtokeaa.
Haraka akaundea mlango ili atoke nje na awakimbie wale jamaa, ila wakati anafungua mlango alikutana na sura ambayo hakuitarajia kuikuta pale mlangoni na ni kama walijua atafanya hicho kitendo.
Wakati anafungua, alikutana na Gomba akiwa amesimama na kisu mkononi bila wasiwasi.
Jay alistuka kwa sababu aliachana na Gomba akigeuza gari na yule mwanamke ambae hakuwa muongeaji kabisa, sasa vije tena yupo mlangoni kwake? Jay alipagawa na jasho likamtoka mfululizo.
“Dogo; Hivi unadhani unaakili kutuzidi?” Cholo alisema huku akisimama kumfuata Jay ambae alikuwa ameganda kama sanamu asijue cha kufanya.
“Yaani bwana mdogo, tumekuzidi kila kitu, Pesa; mademu; umri; akili na hata dhambi tumekuzidi aisee!” Cholo aliendelea kusisitiza kwa hasira.
Jay aligonganisha viganja vyake ishara ya kuomba radhi kwa wale jamaa watatu ambao aliamini kabisa sio watu wazuri kabisa katika maisha yake wakati huo. Alijiuta kumfahamu Vedi ambae ni dhahiri ndie aliemuingiza kwenye mauzauza yale. Jay aliangusha chozi la uchungu kwa kuona uhai wake unaenda kupotea hivi hivi; Jay hakutegemea kusamehewa na baradhuli wale.
Jay alipiga magoti na kusihi aachiwe huku kimoyo moyo akiomba Mungu wake amuokoe na dhahama inayomfuata.
**
Maoni yako tafadhali