Baharia; (Ujasusi, Mapenzi na Upelelezi wa kutisha)

RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA TATU

Ndio! Alimuona Gomba akiwa makini na nyendo za Nyamizi na Vedi.

Boneka mwenyewe hakujua ni kwa nini hata yeye alijikuta akimhisi vibaya yule jamaa.

Usiku huu anafanya nini hapa, na kwanini anamwangalia sana mke wangu na rafiki yake? Na kweli anaweza kuwa na urafiki na Jay hadi awe na kazi ya kumfuatilia Vedi?

Boneka aliendelea kuuliza maswali bila kupata jibu.

"mh" aliguna peke yake kisha akajiuliza tena "inawezekana kweli huyu Jay akawa anahusika kwenye hili sakata?"

Boneka akiwa bado anajiuliza hayo, mara akaona Gomba akianza kuondoka pale alipokuwa amesimama. Hakujua ni kwa nini aliamua kuondoka.

Boneka nae alishuka na kuanza kumfuata taratibu bila wasiwasi wowote.

Gomba alikuwa anaongea na simu huku akijisaidia haja ndogo kwenye kigiza mbali na mwanga wa taa.

Alikuwa anaongea kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba haikuwa rahisi mtu wa mbali kidogo walau kusikia walichozungumza.

Boneka alihitaji kujua kitu kutoka kwa Gomba.

Alikuwa na maswali mawili tu kwake.

Alihitaji kujua pale alikuwa anamchunguza nani kati ya Nyamizi na Vedi na pia alihitaji kujua ni kwanini gari la wagonjwa aliloliita halikufika muhimbili na Jay na badala yake lilimwacha kusikojulikana?

Ni hayo tu!

Wakati Gomba anafunga zipu ni wakati huo aliposikia akiguswa bega lake la kushoto.

Taratibu aligeuka bila papara yoyote huku akikata simu yake.

Alikutana na sura ya kijana mtanashati ambae kimwonekano tu alitangaza ukwasi aliokuwa nao.

Gomba aliweka sura ya kazi bila kusema lolote. Ila ajabu mgeni wake wala hakujali zaidi ya kutabasamu tu na hapo ndipo alipoona kijana mwenye sura ya kike na tabasamu la kiume.

Alikuwa anatazamana na Boneka.

"Nikusaidie nini!" Gomba alihoji.

"Ninahitaji kuongea na wewe kidogo" Boneka alijibu huku akiwa ameweka mikono mfukoni.

Gomba alimtazama juu hadi chini na wala hakuhisi kama kijana yule anaweza kuwa na ubaya wowote ule..

"kwa wema au ubaya!" Gomba alihoji.

"Inategemeana na vile utakavyochukulia ila vyovyote sawa tu" Boneka alijibu.

Ebo!!!

Gomba alishangaa,kijana mdogo ambae amekaa kike kike anakuwaje na mikwara tena.

Gomba alicheka.

"Yani wewe wa kunikatia mkwara mimi! You can't be serious young boy" Gomba alichanganya na kimombo kidogo.

Boneka hakustuka alikaa kimya akimtizama Gomba.

"Haya unasemaje.!" Gomba alihoji kwa kebehi.

"Nikikuuliza hapa umefuata nini unaweza kunijibu?" Boneka alihoji.

"Sasa utaanzaje kuniuliza mtoto mrembo kama wewe au na wewe ni Jezabeli nini?" Gomba aliendelea kudhihaki.

"Mwanzo nilikwambia vyovyote utakavyopenda kuulizwa iwe kwa wema au ubaya, naona sasa unataka tena nikuthibitishie ubaya ninao maanisha" Boneka alimwambia Gomba huku akiwa kwenye kiwango cha juu cha hasira.

Gomba hakutaka kuweka maelezo zaidi. Akanyanyua mkono wake ili amsukume Boneka na aendelee na mambo yake.

Kwa wepesi wa ajabu alijikuta akivutwa kwa kasi na kusukumiwa ngumi nzito kifuani na kabla hajaanguka akadakwa tena na kisha akapigwa kichwa maridadi kwenye paji la uso na akahisi dunia ikizunguka na yeye mwenyewe alipoachiwa alijikuta akiyumba huku na huko kama mlevi huku akili yake ikikataa kukubali ya kuwa yule kijana mpole aliesimama imara ndie aliemwadabisha kwa mipigo miwili tu na kumweka hoi namna ile.

Gomba alitikisa kichwa kuweka sawa akili yake ili asisumbuliwe na mawenge.

Akajipanga ili amkabili Boneka.

Kwa pupa akamwendea Boneka huku akiunguruma kama Simba jike aliekosa bwana.

Boneka akahepa kidogo na kufanya ngumi ya Gomba ipite patupu na kisha akamshindilia teke madhubuti mgongoni.

Gomba alienda kuanguka kifudi fudi huku akilia kama msimbe.

Boneka alibaki akiwa amesimama bila papara yoyote.

Wakati akimsubiri asimame, mara akashangaa gari ikimjia kwa kasi nae akaruka na kujiweka pembeni,gari ile ikaenda kusimama karibu na alipoanguakia Gomba; Gomba hakutaka kuuweka, haraka akafungua mlango na kujitosa ndani na kwa kasi gari ikaondoka pale huku Boneka akiuma meno kwa hasira.

***

Ndani ya gari; Gomba na Panga hawakusemeshana. Panga alikuwa bize na usukani huku Gomba akijibinya paji la uso.

"Yule bwege kaniotea sana aisee!" Gomba alilalama.

"Tangu mwanzo niliona umemdharau yule mtoto na ndio mana umekunwa upele jombaa" Panga alimkebehi Gomba.

"Dah! Miaka mingi sana sijawahi kuotewa namna hii aisee." Gomba alisema tena.

"Ndo inatakiwa ujue hata panya akikatisha uwanja wa vita lazima alambwe njiti" Panga alisema.

"Lakini yule bwege ni nani?" Gomba alihoji.

"Kwa kweli sijamjua vizuri ila tuwe makini sana, tunaweza ona tupo salama na tukajikuta tunaokotwa kama vifaranga ujue!" Panga aliatahadharisha.

"Lakini Taiga angeshatupa taarifa kama kuna watu wapo nyayoni mwetu, kukaa kwake kimya kunaashiria hamna jipya na kama kuna askari anatufuata ingejulikana pia" Gomba alipinga mashaka ya Panga.

Panga alikaa kimya na safari iliendelea.

----------------------

Wakati Boneka anarejea kwenye gari ni wakati ambao mkewe Nyamizi alikuwa anamalizia mazungumzo na kuagana na Vedi.

Nyamizi alihakikisha Vedi amepata usafiri wa kumrejesha ndipo na yeye alienda kupanda gari la mumewe.

"Ulikuwa sahihi mume wangu; Vedi anatatizo kubwa tu linalomsumbua" Nyamizi alisema punde tu alipokaa na kufunga mlango.

"Kakudokeza lolote?" Boneka alihoji.

"Hapana hajafunga lolote ila amenambia kuna tatizo lipo kwenye ile meli ya Serengeti Marine na ndio chanzo cha matatizo yake haya" Nyamizi alisema huku akiegemea kwenye kiti.

"Sasa kwanini hajakushirikisha?" Boneka alihoji huku akiwa makini sana kusikiliza kila neno litakalo semwa na mkewe.

"Alichonambia ni kuwa ili niwe salama ni lazima nisijue kwa sasa na hataki niingie kwenye shida wakati huu"

"Sasa kwanini hajaenda polisi hadi sasa?"

"Kasema amejikuta anasita kufanya hivyo na hajui wa kumwamini na pia anaamini watu walioko nyuma ya jambo lile ni watu wenye mitego mingi hivyo anaweza kuishia kubaya na ikizingatia watu wanajua keshafariki"

Boneka alivuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akasema
"Nadhani nahitaji kuongea nae na kama ataniamini basi nitampa askari makini asaidiane nae, nina marafiki wengi ni watu wa usalama watamsaidia" Boneka alisema na Nyamizi hakujibu kitu.

Nyamizi tangu afahamiane na Boneka hajawahi kujua lolote kuhusu Boneka kufanya kazi idara ya usalama, zaidi alijua mumewe ni mfanyabiashara na bilionea kijana.

Boneka akiwa kimya kabisa alimtazama mkewe ambae alikuwa amejilaza pembeni yake huku akiwa amepitiwa na usingizi.

Boneka alisimamisha gari na kwenda kufungua geti la nyumba yake na kisha akarejea na kuingiza gari ndani kisha akamwamsha mkewe.

Nyamizi aliingia ndani na kumwacha Boneka akijishugulisha kufanya hiki na kile kwenye gari.

Boneka alipohakikisha mkewe ameingia ndani alichukua simu yake na kwenda upande wa ujumbe kimtandao yani barua pepe na kufungua.

Alikutana na jumbe ambayo ilitoka kwa mtu ambae alitumia akiwa ofisini kwao.

"Upo bongo, kesho unakazi? Au kimekurudisha?" Ujumbe ule ulisomeka hivyo.

Alijua kabisa mtu yule alijua uwepo wake hapa Tanzania badala ya Nairobi kwenye fungate lake na ndio mana aliuliza "kimekurudisha?" yani nini kimekurudisha na pia aliuliza kama kesho atakuwa na nafasi, hiyo inamaanisha anahitajika ofisini.

Aliujibu!!

"Msitari mwekundu unaelea kwenye kina kirefu" kisha akautuma na ajabu aliona mpokeaji yupo hewani.

Mpokeaji nae alisoma na alielewa ya kuwa "Mstari mwekundu" ni hatari inayoonekana na "Kina cha bahari" ilimaanisha siri kubwa ya wenye nguvu, hivyo mpokeaji nae akatuma tena ujumbe mwingine

"Basi itakuwa ni Tarasi, Tandara kwenye nyuzi moja"

Boneka alipokea na kuusoma akelewa.

"Tarasi" inamaana katika lugha ya kijasusi ni moja na "Tandara" ni mbili na "Nyuzi" ni kazi.

Hivyo alijua mtumaji amemaanisha hiyo hatari alioona ni moja na hatari ya pili ipo ofisini na wanatakiwa wazifanyie kazi zote, hivyo ni kumaanisha kazini kwake pia kulikuwa kuna kazi inaendelea na ikiongezeka ya kwake basi itakuwa ni kazi moja itakayogawanywa..

Ujumbe mfupi wenye mana kubwa.

Boneka akaingia ndani kwake huku akijua ahsubuhi anatakiwa kwenda ofisini kwake.

Ahsubuh hiyo ndio kikawa chanzo cha jambo lingine jipya kwa pande zote.

***

MAONI YAKO TAFADHALI!!!
 
Mambo ni motooo
 
Hadithi za kudo huwa nacheki page za mwisho km kuna neno tamati ndio nianza kusoma. Manake hachelewi kuacha watu na arosto mazima!
 
Back
Top Bottom